ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Tukiwa katika hali nzuri kimaisha, tunapokula milo zaidi ya mitatu kwa siku na kusaza, ltunapo lala kwenye mahekalu ya zaidi ya lile la Mfalme Suleiman, tunapougua kidogo lakini tunajitibu kwa gharama kubwa, watoto wetu wanaposoma kule ambapo ada inazidi ile ya chuo kikuu, wake au waume zetu wanapoenda kwenye saloon ambazo huduma ya kuremba nywele inazidi ya kodi ya nyumba ya mwezi kwa baadhi ya wanadamu wenzetu, tushukuru Mungu na katika hilo tutumie fursa na Baraka ambazo Mungu ametujalia na tuwakumbuke na wale walio kama hawa!!!