BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,370
- 8,106
Kwa sasa, vifaa vingi ambavyo vinatumia port ya USB Type C ambazo ni latest, zinatumia aina ya USB Type-C 3.2 ambayo ina Max speed ya 20GB kwa sekunde. Teknolojia inazidi kubadilika na dunia imeingia katika mfumo mpya wa USB 4 na sasa ni toleo la 2.0.
The USB Promoter Group ni kikundi cha wasimamizi wa umoja wa port ya USB (ni muunganiko wa kampuni ya Apple, Microsoft, HP, n.k); zimetambulisha aina mpya ya USB4 ambayo ina uwezo mkubwa mara mbili ya USB4 ya kawaida na kuizidi speed Thunderbolt 4 ambayo ndio port ya USB iliyokuwa inaongoza katika speed.
► Mabadiliko makubwa ya USB4 toleo la 2.0 ni speed kubwa kuliko port za USB-C 3 za kawaida na Thunderbolt 4. Speed yake ni mara mbili ya speed kubwa iliyokwepo.
► Pia cable na port zote za USB 4 version 2.0 zitaendelea kukubali cables za USB 3, USB 3, USB 1 bila matatizo lakini speed yake haitakuwa kama ya USB4.
⚡️ Aina hii mpya ya USB itaanza kuingia katika vifaa mbalimbali kuanzia mwezi wa 11 mwaka huu. Hivyo tutegemee itawekwa katika simu kubwa za 2023.
#Tetesi zinaonyesha Apple ni miongoni mwa kampuni ambazo zimeshiriki katika kuunda aina hii mpya ya USB Type-C; inawezekana iPhone 15 ambayo itatoka mwakani itakuwa na aina hii mpya ya USB-C.