MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
- Thread starter
-
- #21
Hadi leo na kesho mzee wa Chato anamuogopa Edward Ngoyai Lowassa, sijui lile jaribio la kumnunua lilifikia wapi!!! Je, ukimya wake ni matokeo ya kile kikao pale magogoni?? Au ameamua tu kupumzika??
Tatizo ni kwamba yeye hakujua kuzichanga karata zake vizuri wala fitina hakuzijua kijana wa msoga akamtumia kama ngazi 2005-akaukwaa urais muda si mrefu akamfanyia ile vijana wanaita kumuua nyani akasukiwa zengwe jumba bovu likamwangukia ndiyo ukawa mwanzo wa kukata pumzi mdogo mdogo
Lowassa kiukweli.. Is truely an extra ordinary politician hasa za hapa nyumbani..!!
What makes an extraordinary politician? - Quora
https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjAMegQICRAB&usg=AOvVaw0ZXrT9BwMvVKdnCPi_A6RX
Hiki ndicho naweza sema kwa sasa, ingawa now namsapoti JPM, but heshima yake kwa wengi sana CCM na nje ya CCM iko bado kubwa sana..!! Mungu amjalie kila jema kwake Mzee Lowassa..!!
Lowassa ndiye mwanasiasa aliyewahi kuwa maarufu hapa nchini bila kuwa na maneno mengi.
His actions spoke volumes, japo mimi binafsi nilikuwa simuamini sana kwasababu naifahamu michezo yake.
Huwa ninajiuliza Lowassa lini aliwahi kuwa na nguvu za kisiasa zaidi ya mikakati ya chinichini. Nguvu zake zilikuzwa na vyombo vya habari, lakini hakuwahi kuwa mwenye siasa za ushawishi wa hoja. Sana sana tulikuwa tunasikia wapambe wake wakisema ni mtu wa maamuzi magumu.
Propaganda zile zile ndio mpaka leo zinamchanganya Magufuli na kumfanya kujitungia sheria yake ya mfukoni jinsi ya kufanya siasa hapa nchini. Halafu mleta uzi unasema kweli mambo yanabadilika na mfano wako ni Lowassa!! Ulitarajia mtu mwenye umri wa 60+ afanye jipya lipi kwenye siasa za aina ya Magufuli ambapo wapinzani wanaishia jela na udhalilishwaji mwingine ikiwepo hatari ya maisha yao?
Naweza sema anaweza kurudi ingawa nguvu ya kimfumo haiko imara kwa sasa, mfumo aliouweka kwa muda mrefu umesambaratishwa sana na rivals wake.
Tuna Bahati sana kuwa na wazee kama mkapa, kikwete, mangula, n.k bila wao, nchi ingekuwa wamegawana yote. Ila Kwa kumleta mzee magu, nchi inaendelea kupona vidonda. Kikwete aliona atubu Kwa kumleta Magufuli.Roho mbaya za kina Kikwete ndio zilisababisha kutuletea balaa la sasa,
Mtu mwenye vision ambae angetuvusha na kupanda ngazi alikuwa Lowasa,
NB usione Kobe kainama jua anatunga sheria
Nani angeigawanya nchi ???T
Tuna Bahati sana kuwa na wazee kama mkapa, kikwete, mangula, n.k bila wao, nchi ingekuwa wamegawana yote. Ila Kwa kumleta mzee magu, nchi inaendelea kupona vidonda. Kikwete aliona atubu Kwa kumleta Magufuli.
Ameshajiishia huyo. Hana umakini wowote na nawashangaa wanaompamba .Angekuwa mwanasiasa wa kweli asingefikiria kuingia Ikulu kwa kuwanunua watanzania. Na kama angekuwa na huo mtandao mnaousema basi angeshashtuka wakati anawekewa mtego wa Richmond na angeweza kushtukia wakati mikakati ya kukata jina lake ikipangwa. Mwisho naweza kusema kuwa huyu jamaa ni wa kawaida sana ila alizungukwa na watu waliokuwa wanataka hela yake tu.
Yaani Raisi Magufuli amempiga sana na kila mti aliokuwa anashikilia unakatika. Dunia inabadilika, zamani ulikuwa huwezi ingia kwenye bifu na Lowassa bila kuumiaKwenye vyombo vya usalama na ulinzi Lowassa alikuwa amevikamata kwelikweli....
Ila kwa sasa sidhani kama hivyo vyombo husika amevikamata kama hapo awali mkuu....
Hakika jamaa alikuwa ana ushawishi mkubwa sana hakuwa wa kubezwa kabisa....
Nilijua ni wa kimataifa tu...! Kumbe umejidhatiti hadi kwenye kona hii !!Hapa umeongea kitu kikubwa sana. Siasa ni mfumo wa mahesabu na mikakati mizito, lakini bahati mbaya sana mtandao wa Edward Lowassa ulioitesa sana Serikali ya Rais Mkapa na Rais Kikwete umevunjwa mifupa na kupona siyo leo wala kesho. Mtandao wa Raisi Magufuli unahusisha makundi ya watu wenye nguvu sana hapa Nchini, Ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Kimya kingi kina mshindo mkuu...Kwani Lowassa bado ana nguvu kama zamani ??