MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,783
- Thread starter
- #21
Hadi leo na kesho mzee wa Chato anamuogopa Edward Ngoyai Lowassa, sijui lile jaribio la kumnunua lilifikia wapi!!! Je, ukimya wake ni matokeo ya kile kikao pale magogoni?? Au ameamua tu kupumzika??
Lowassa anaogopwa kweli na wanasiasa wengi sana hapa nchini na Raisi wetu akiwemo.
Nguvu yake ni kubwa sana, lakini kibaya ni kwamba kipindi hiki ALLIANCE aliyouinda Raisi Magufuli na viongozi fulani fulani hivi imefanikiwa sana kumzorotesha Lowassa. Sidhani kama Lowassa anaweza kuwashinda wakina Raisi Magufuli akiwa na CHADEMA peke yake. Raisi Magufuli na genge lake wamevuka hadi mipaka na kwenda kutafuta marafiki nje ya mipaka ya Tanzania. Kama Lowassa atawashida hawa kwa kipindi hiki, basi nitamvulia kofia zote, kwasababu mpaka sasa kambi yake ina mejeraha mazito yasiyoweza kutibika leo wala kesho....