Dunia inabadilika sana: Lowassa wa leo siyo yule wa 1995-2010

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
18,418
2,000
Hadi leo na kesho mzee wa Chato anamuogopa Edward Ngoyai Lowassa, sijui lile jaribio la kumnunua lilifikia wapi!!! Je, ukimya wake ni matokeo ya kile kikao pale magogoni?? Au ameamua tu kupumzika??

Lowassa anaogopwa kweli na wanasiasa wengi sana hapa nchini na Raisi wetu akiwemo.
Nguvu yake ni kubwa sana, lakini kibaya ni kwamba kipindi hiki ALLIANCE aliyouinda Raisi Magufuli na viongozi fulani fulani hivi imefanikiwa sana kumzorotesha Lowassa. Sidhani kama Lowassa anaweza kuwashinda wakina Raisi Magufuli akiwa na CHADEMA peke yake. Raisi Magufuli na genge lake wamevuka hadi mipaka na kwenda kutafuta marafiki nje ya mipaka ya Tanzania. Kama Lowassa atawashida hawa kwa kipindi hiki, basi nitamvulia kofia zote, kwasababu mpaka sasa kambi yake ina mejeraha mazito yasiyoweza kutibika leo wala kesho....
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
18,418
2,000
Tatizo ni kwamba yeye hakujua kuzichanga karata zake vizuri wala fitina hakuzijua kijana wa msoga akamtumia kama ngazi 2005-akaukwaa urais muda si mrefu akamfanyia ile vijana wanaita kumuua nyani akasukiwa zengwe jumba bovu likamwangukia ndiyo ukawa mwanzo wa kukata pumzi mdogo mdogo

Kuna msemo wa Kiingereza unasema hivi: THERE IS NO HONOUR AMONG THIEVES.
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
18,418
2,000
Lowassa kiukweli.. Is truely an extra ordinary politician hasa za hapa nyumbani..!!

What makes an extraordinary politician? - Quora
https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjAMegQICRAB&usg=AOvVaw0ZXrT9BwMvVKdnCPi_A6RX

Hiki ndicho naweza sema kwa sasa, ingawa now namsapoti JPM, but heshima yake kwa wengi sana CCM na nje ya CCM iko bado kubwa sana..!! Mungu amjalie kila jema kwake Mzee Lowassa..!!

Lowassa ndiye mwanasiasa aliyewahi kuwa maarufu hapa nchini bila kuwa na maneno mengi.
His actions spoke volumes, japo mimi binafsi nilikuwa simuamini sana kwasababu naifahamu michezo yake.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
46,706
2,000
Huwa ninajiuliza Lowassa lini aliwahi kuwa na nguvu za kisiasa zaidi ya mikakati ya chinichini. Nguvu zake zilikuzwa na vyombo vya habari, lakini hakuwahi kuwa mwenye siasa za ushawishi wa hoja. Sana sana tulikuwa tunasikia wapambe wake wakisema ni mtu wa maamuzi magumu.

Propaganda zile zile ndio mpaka leo zinamchanganya Magufuli na kumfanya kujitungia sheria yake ya mfukoni jinsi ya kufanya siasa hapa nchini. Halafu mleta uzi unasema kweli mambo yanabadilika na mfano wako ni Lowassa!! Ulitarajia mtu mwenye umri wa 60+ afanye jipya lipi kwenye siasa za aina ya Magufuli ambapo wapinzani wanaishia jela na udhalilishwaji mwingine ikiwepo hatari ya maisha yao?
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
15,017
2,000
Lowassa ndiye mwanasiasa aliyewahi kuwa maarufu hapa nchini bila kuwa na maneno mengi.
His actions spoke volumes, japo mimi binafsi nilikuwa simuamini sana kwasababu naifahamu michezo yake.

IMG-20180523-WA0024.jpg
 
soine

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,113
2,000
Huyu mtu siasa zake za kabla ya 2015 zilinifanya nisimkubali, ila kuanzia 2015 alibadilika sana kufanya siasa nzuri.

Naweza sema anaweza kurudi ingawa nguvu ya kimfumo haiko imara kwa sasa, mfumo aliouweka kwa muda mrefu umesambaratishwa sana na rivals wake.

Ila kutokana na hali halisi kwenye sekta binafsi kwa sasa, akiuza wazo litanunulika haraka sana, na huenda akapata support ya kutosha. Tatizo ama changamoto kubwa ni kukosa uhuru kwa wale watakaomsupoti kwa kuogopa kuingia kwenye tafrani na wenye rungu kwa sasa.
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
18,418
2,000
Huwa ninajiuliza Lowassa lini aliwahi kuwa na nguvu za kisiasa zaidi ya mikakati ya chinichini. Nguvu zake zilikuzwa na vyombo vya habari, lakini hakuwahi kuwa mwenye siasa za ushawishi wa hoja. Sana sana tulikuwa tunasikia wapambe wake wakisema ni mtu wa maamuzi magumu.

Propaganda zile zile ndio mpaka leo zinamchanganya Magufuli na kumfanya kujitungia sheria yake ya mfukoni jinsi ya kufanya siasa hapa nchini. Halafu mleta uzi unasema kweli mambo yanabadilika na mfano wako ni Lowassa!! Ulitarajia mtu mwenye umri wa 60+ afanye jipya lipi kwenye siasa za aina ya Magufuli ambapo wapinzani wanaishia jela na udhalilishwaji mwingine ikiwepo hatari ya maisha yao?

My friend kama huifahamu nguvu ya Mzee Lowassa ndani ya CCM na Serikali basi wewe huenda huzifahamu Siasa za Tanzania au Unafahamu lakini umeamua kupinga tu. Sehemu kubwa ya SIASA za Tanzania na Afrika kwa ujumla haziendeshwi kwa nguvu ya hoja. Kama zingekuwa ni za nguvu ya hoja basi leo hii Chama cha Mapinduzi kingekuwa kimeshatoka madarakani muda mrefu sana, Au hata watu kama Dr. Salim Ahmed Salim au Prof. Mark Mwandosya wangekuwa maraisi wa nchi lakini bahati mbaya haipo hivyo.

Pili, mwanasiasa yoyote mkubwa hawezi kuwa na nguvu bila kuwa na wapambe (Dunia nzima iko hivyo).
Yeya pale anakuwa anawakilisha maslahi ya makundi mbali mbali ya kiuchumi, kidini, kisiasa, kikabila au kiitikadi ambayo hutegemea kupata fadhila fulani pindi huyo mgombea atakaposhinda. Sasa kama ungeufahamu mtandao wa Edward Lowassa na watu waliokuwa POWER BROKERS wake usingesema haya unayoyasema na ungeelewa kwanini watu wengi walikuwa wanamwogopa na kumpinga sana atoke kwenye uwaziri mkuu na asiwe Rais wa nchi.

NB: Sawa na Raisi Magufuli leo hii, kama angekuwa peke yake basi sidhani hata kama angeweza kufika hata hapa alipo. Lakini Magufuli yeye pale alipo ni SYMBOL ya wale ambao anawawakilisha. Ni kundi moja la watu wenye nguvu sana ya kiushawishi hapa nchini, Afrika Mashariki na Ukanda wa SADC: Wale ndiyo wanambeba Raisi Magufuli kwasababu wananufaika kwa namna moja au nyingine na uwepo wake pale Ikulu. (Usiyachukulie haya mambo juu juu tu)
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
18,418
2,000
Naweza sema anaweza kurudi ingawa nguvu ya kimfumo haiko imara kwa sasa, mfumo aliouweka kwa muda mrefu umesambaratishwa sana na rivals wake.

Hapa umeongea kitu kikubwa sana. Siasa ni mfumo wa mahesabu na mikakati mizito, lakini bahati mbaya sana mtandao wa Edward Lowassa ulioitesa sana Serikali ya Rais Mkapa na Rais Kikwete umevunjwa mifupa na kupona siyo leo wala kesho. Mtandao wa Raisi Magufuli unahusisha makundi ya watu wenye nguvu sana hapa Nchini, Ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
 
BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,294
2,000
T
Roho mbaya za kina Kikwete ndio zilisababisha kutuletea balaa la sasa,
Mtu mwenye vision ambae angetuvusha na kupanda ngazi alikuwa Lowasa,
NB usione Kobe kainama jua anatunga sheria
Tuna Bahati sana kuwa na wazee kama mkapa, kikwete, mangula, n.k bila wao, nchi ingekuwa wamegawana yote. Ila Kwa kumleta mzee magu, nchi inaendelea kupona vidonda. Kikwete aliona atubu Kwa kumleta Magufuli.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,144
2,000
Nimemsikia, Nimemwona, nimesikia na kuona nguvu zake ndani ya CCM, niliona gia ilivyobadilishwa hewani, lakini sijui ndani ya CDM/UKAWA anasimamia nini. Je atanitoa nyumbani nikapige kura? Hilo namwachia yeye na upinzani wafanye kazi yao.
 
St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,401
2,000
Ameshajiishia huyo. Hana umakini wowote na nawashangaa wanaompamba .Angekuwa mwanasiasa wa kweli asingefikiria kuingia Ikulu kwa kuwanunua watanzania. Na kama angekuwa na huo mtandao mnaousema basi angeshashtuka wakati anawekewa mtego wa Richmond na angeweza kushtukia wakati mikakati ya kukata jina lake ikipangwa. Mwisho naweza kusema kuwa huyu jamaa ni wa kawaida sana ila alizungukwa na watu waliokuwa wanataka hela yake tu.
 
Alikuwa Overrated sana siyo ???
 
theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,791
2,000
Kwenye vyombo vya usalama na ulinzi Lowassa alikuwa amevikamata kwelikweli....

Ila kwa sasa sidhani kama hivyo vyombo husika amevikamata kama hapo awali mkuu....

Hakika jamaa alikuwa ana ushawishi mkubwa sana hakuwa wa kubezwa kabisa....
 
kipyola

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
281
500
Mlifanya kosa kubwa sana kulipeleka jiwe magogoni siasa za awamu hii zinaongozwa na mtu mmoja tu ambaye ni mwoga wa siasa za kukosolewa anataka kurudisha ufalme na umwinyi.
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
18,418
2,000
Kwenye vyombo vya usalama na ulinzi Lowassa alikuwa amevikamata kwelikweli....

Ila kwa sasa sidhani kama hivyo vyombo husika amevikamata kama hapo awali mkuu....

Hakika jamaa alikuwa ana ushawishi mkubwa sana hakuwa wa kubezwa kabisa....
Yaani Raisi Magufuli amempiga sana na kila mti aliokuwa anashikilia unakatika. Dunia inabadilika, zamani ulikuwa huwezi ingia kwenye bifu na Lowassa bila kuumia
 
hopaje

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
1,730
2,000
Daa nilimpanga kumpa lowasa kura yangu popote pale alipo leo hii lowasa angekuwa raisi mambo yasingekuwa hivi mambo ni hovyo hovyo tu
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
19,861
2,000
Hapa umeongea kitu kikubwa sana. Siasa ni mfumo wa mahesabu na mikakati mizito, lakini bahati mbaya sana mtandao wa Edward Lowassa ulioitesa sana Serikali ya Rais Mkapa na Rais Kikwete umevunjwa mifupa na kupona siyo leo wala kesho. Mtandao wa Raisi Magufuli unahusisha makundi ya watu wenye nguvu sana hapa Nchini, Ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Nilijua ni wa kimataifa tu...! Kumbe umejidhatiti hadi kwenye kona hii !!
====
Mkuu ebu fafanua kwa undani juu ya hili."....makundi ya watu wenye nguvu sana hapa Nchini, Ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika". Ukilejerea, tifu la Utawala Afrika Kusini, sokomoko la Zimbabwe, tua ni kutue ya Zambia, mieleka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwingine, Sudan Kusini, Kenya na siasa zake, Burundi Rwanda, kimue mue cha Msumbiji, Mchakamchaka wa Madagascar, Upinde na shale wa Visiwa vya Komoro...! Ebua anzia hapo...maana nilipopataja, nimejaribu kuunganisha 'dots' zangu jinsi ndugu zetu hawa (wenye nguvu kubwa) wanaweza kuwa moja ya wale wanao 'remotely' control masuala ya huko.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom