Dunia imeniacha kinywa wazi!

Dunia imeniacha kinywa wazi!

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,602
Reaction score
1,864
Ni mimi wako UWESUTANZANIA 🌍

Kusema ukweli sina siku nyingi sana tokea nimefika katika hii dunia, nina jumla ya wastani wa siku 10,800 sawa na miaka kama 30 hivi au 29.,
Kwenye kipindi chote nimekuwa hapa kuna mambo yameniacha kinywa wazi sana, naamini hata na wewe ndugu msomaji yapo mambo yamekushangaza kama itakupendeza utashiriki na mimi.

Jambo la kwanza (DINI)
Asilimia kubwa ya watu hufata mamlisho na sheria na vikwanzo kutoka kwenye Kiumbe kisichojulikana,.
Wanakiogopa na kukitii.
Wamekijengea majumba na kusema ni yake, wanakusanyika humo na kuzungumza naye aliyakuwa hawamuoni wala hawasikii sauti yake.
Kama wewe ni mgeni hapa duniani unaweza hisi ni wachache wenye kufuata hayo ila cha kushangaza ni wengi ndio wenye kufuata hayo na wachache sana ndio huwa hawafuatishi kwa yalio huko, na wenyewe wakisema huonekana watu wa ajabu sana.
Wanatumaini hupata chakura kutoka kwake, hupata mafanikio na hata pumzi waliyonayo ni kutoka kwake, wengine hufika mbali zaidi na kudai hata wakifa wataenda keti pamoja naye.,

Jambo la pili ujenzi (MAJUMBA)
Nimeona hili la kushangaza pia,
Watu wa duniani wamekuwa ni wenye kujenga majumba makubwa na yenye uimara wa wastani wa miaka 500 aliyakuwa wenyewe huishi miaka 90 na 100,. Wengi wao hufanya hivyo na wachache wasio fanya ujenzi huonekana ni watu wa ajabu na wasio na maana,.
Wengine hujenga kwa kusema ni kwa ajili ya vizazi vyao, ila cha kushangaza hata wasio zaa pia HUJENGA, je wajengea nini sijui.?

Jambo la tatu PESA ( FEDHA)
Hapa kwanza ncheke,
Duniani kuna vitu vyaitwa pesa. Viko vya kama vichuma chuma na viko vya mfananio na makaratasi.
Naam ni makaratasi kabisa, hayana maana yeyote wala faida.
Huwezi fanya andazi ukanywia chai wala huwezi tia kwenye mboga kama kitunguu,.
Ila cha kushangaza watu wamekuwa wakitoa macho mpaka kuuana hili nitaenda kukumbuka sana na nitaenda simulia haya maajabu ikiwa nitaondoka kwenye hii dunia.

Mwisho
Kwangu mimi DUNIA ni kama kisiwa nimeanguka na ndege baada ya ndege kupata ajali.
Jambo langu kubwa nafanya ni kutafuta msaada wa wavuvi na ndege za Hanga iliniweze kuondoka katika kisiwa hiki.
Siwezi kujenga wala kununua ardhi. Maana wakati wowote nikipata msaada basi nitakuwa ni mwenye kuondoka (KIFO)
 
Ngoja nami niongeze maajabu yangu:

Ajabu la 1 ni watu kupigania ardhi ambayo wanauana na kuiacha kama walivyoikuta. Kama Israel na Palestina wakikubaliana "hiki kieneo kidogo sote tutakiacha kama tulivyokikuta, ninyi kaeni pale nasi tukae hapa, au hata tuchangamane" hakuna shida yoyote itawakumba, ila wao wameamua kuishi wakiuana kwa miaka na miaka.

Ajabu la 2 ni utaratibu wa majeshi. Majeshi yamekuwapo toka enzi na enzi. Eti unaambiwa mwanajeshi hahoji, haandamani wala hagomi akipewa amri au akifanyiwa ujinga wowote na aliye juu yake. Matokeo yake ni kutumika vibaya kwa maslahi ya watu wengine. Ukiambiwa ua yule ni kutii, nenda vitani (hata kama adui yupo strong mara 10 zaidi) wewe ni kuchanganya mbariga bila kujali usalama wako wala sababu ya vita hivyo, yaani hata kama ni wakuu wa nchi/mamlaka ya kwenu na ya adui wametusiana kibinafsi wakaamua kuzichapa hawaingii ulingoni wao ni ninyi mnaoitwa 'wajeda'. Halafu mkishinda vita mnapokea vizawadi kiduchu then wahuni waliokuwa wamekula kishoka maofisini wakipanda vyeo na kupokea minyota. Mkiuawa ni faraja kwa familia wao wanaendelea kugonga glass. Unavikwa taji la uzalendo unarisk maisha yako kupambania maslahi ya wanasiasa. Na mengine mengi kwenye jeshi.
 
KIFO... umesema utaenda simulia huko unakoenda baada ya kifo, unaamini kuna maisha baada ya kifo IMANI. imani ni nini?
 
KIFO... umesema utaenda simulia huko unakoenda baada ya kifo, unaamini kuna maisha baada ya kifo IMANI. imani ni nini?
Siamini kama kuna maisha baada ya kifo, ila kama ikitokea nikawa sehemu nyingine tofauti na hii dunia basi nitawaweka chini wajukuu zangu na kuwasimulia mambo ya kushangaza ya duniani
 
Ngoja nami niongeze maajabu yangu:

Ajabu la 1 ni watu kupigania ardhi ambayo wanauana na kuiacha kama walivyoikuta. Kama Israel na Palestina wakikubaliana "hiki kieneo kidogo sote tutakiacha kama tulivyokikuta, ninyi kaeni pale nasi tukae hapa, au hata tuchangamane" hakuna shida yoyote itawakumba, ila wao wameamua kuishi wakiuana kwa miaka na miaka.

Ajabu la 2 ni utaratibu wa majeshi. Majeshi yamekuwapo toka enzi na enzi. Eti unaambiwa mwanajeshi hahoji, haandamani wala hagomi akipewa amri au akifanyiwa ujinga wowote na aliye juu yake. Matokeo yake ni kutumika vibaya kwa maslahi ya watu wengine. Ukiambiwa ua yule ni kutii, nenda vitani (hata kama adui yupo strong mara 10 zaidi) wewe ni kuchanganya mbariga bila kujali usalama wako wala sababu ya vita hivyo, yaani hata kama ni wakuu wa nchi/mamlaka ya kwenu na ya adui wametusiana kibinafsi wakaamua kuzichapa hawaingii ulingoni wao ni ninyi mnaoitwa 'wajeda'. Halafu mkishinda vita mnapokea vizawadi kiduchu then wahuni waliokuwa wamekula kishoka maofisini wakipanda vyeo na kupokea minyota. Mkiuawa ni faraja kwa familia wao wanaendelea kugonga glass. Unavikwa taji la uzalendo unarisk maisha yako kupambania maslahi ya wanasiasa. Na mengine mengi kwenye jeshi.
Hapo kwenye majeshi, ni kweli hii ni maajabu pia.,

Yaani kuna watu wanatumika na watu wenzao kijinga sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom