comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Watafiti kutoka Shirika la Wanyama la London, Shirika la Uhifadhi wa Wanyama pori wa Familia ya Paka la Panthera na Shirika la Uhifadhi wa Wanyama pori nchini Uingereza wamefanya utafiti na kutoa ripoti kwenye Gazeti jipya la Proceedings of the National Academy of Sciences la Marekani, wakitoa onyo kwamba idadi ya duma ambao ni wanyama wanaokimbia kwa kasi zaidi duniani ni 7100 tu, wapo hatarini kutoweka katika uso wa dunia.
Watafiti wamesema licha ya kupungua kwa idadi ya duma, maeneo wanakoishi pia yamepungua na kuwa asilimia 9 tu ya maeneo ya zamani. Duma wanaoishi barani Asia wanaathiriwa zaidi, hivi sasa idadi ya duma wanaoishi nchini Iran ni chini ya 50. Idadi ya duma wanaoishi nchini Zimbabwe imepungua kuwa 170 kutoka 1200 katika miaka 16 iliyopita.