Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Mwandishi: Asalam Aleykum Kaka Dullah, habari ya uzima wako?
Dullah: Waleykum Salam Dada yangu, tunamshukuru Allah kwa neema na rikizi zake.
Mwandishi: Kwanza kabsa napenda kuweka wazi kuwa wewe ni kati ya mabondia ambao wameipatia sifa kubwa sana Tanzania katika sekta ya michezo ya masumbwi.
Dullah: Nashukuru sana kwa heshima hiyo.
Mwandishi: Naomba kufahamu je msukumo wako mpaka ukaingia kwenye mchezo huu ulikuwa ni nini haswa?
Dullah: Dada yangu nadhani unanifahamu mimi ni mtu ambaye nina hofu ya Allah hivyo huwa sioni kama kuna faida wala umuhimu wa kuongea uongo. Binafsi maisha ya ujana tu ndo yalinifanya niingie kwenye mchezo huu, ingawa kipato ni kidogo ila tunapambana na kumshukuru Allah, kwa sasa familia yangu ndo msukumo mkubwa.
Mwandishi: Je isingekuwa ngumi, wewe Dullah ungecheza mchezo gani?
Dullah: Ukitoka ngumi sidhani kama kuna mchezo mwingine ambao upo kwenye damu, zamani sana nilipokuwa mtoto nilipenda kucheza mpira wa miguu ila ngumi ndo zipo moyoni.
Mwandishi: Unazungumziaje nafasi ya Tanzania katika mchezo huu haswa katika kipindi hiki ambacho ni kama hakuna tena promo kama za wakati wa USIKU WA VITASA?
Dullah: Kiukweli kuna makundi mawili ndani ya jamii yetu, kuna watu wanaotumia nguvu kubwa kwenye kuukuza mchezo wetu kupitia motisha na kutoa maoni chanya kwa mabondia ila pia kunaa kundi kubwa la watu ambao hawapendi kuona Dullah ninapata mafanikio ama Twaha ama Mwakinyo. Tukiwa kitu kimoja tuna uwezo wa kuipatia sifa kubwa Tanzania kupitia mchezo wa ngumi.
Mwandishi: Poleni sana, je ukipata wasaha wa kuzungumza na kamisheni ya ngumi za kulipwa, una kipi cha kuwashauri?
Dullah: Kuna mengi ya kuwashauri ila yapo mambo matatu makubwa. Kwanza ni kutengeneza mifumo bora ya kukuza vipaji, huku mitaani kuna vijana wazuri sana, tunaweza kuwatumia kwenye mashindano makubwa kadhaa wakiwakilisha Tanzania.
Pili ni kuhusu masilahi, kamisheni ya ngumi za kulipwa ishirikiane na BMT na kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa mabondia wanapewa stahiki zao kwa muda unaotakiwa. Mwisho ni kuhusu suala la afya, dada yangu afya ndo mtaji wa msingi wa maisha ya binadamu, kamisheni pamoja na BMT wawe mstari wa mbele kutazama afya za wanamichezo wote sio ngumi tu.
Mwandishi: Inaonyesha wewe kweli ni mwanamasumbwi haswa, safi sana Kaka Dullah, sasa unamuona Dullah Mbabe miaka 10 akiwa kwenye nafasi gani?
Dullah: Miaka kumi ijayo namtazama Dullah akiwa mfano kwa vijana wengi Tanzania, natamani kuwa msaada mkubwa kwanza kwa familia yangu pamoja na mabondia chipukizi, kukiwa na nafasi nitasomea ualimu ili nifungue njia zaidi kwa vijana wanaotaka kupata mafanikio zaidi kupitia mchezo wa ngumi.
Mwandishi: je una neno lolote la kuwaambia Watanzania, wapenzi, mashabiki na marafiki zako kote duniani?
Dullah: nawapenda sana, mmekuwa daraja kubwa sana kwangu toka nimeanza kucheza ngumi, mmenipongeza pale ambapo nilikuwa nikishinda mapambo yangu lakini pia nashukuru kwa pole na maneno ya faraja katika nyakati ambazo walikuwa wakinifumua ulingoni. Shukrani sana!