Dulla Mbabe amtandika mchina Knockout raundi ya kwanza, Msauzi agoma kuzipiga na Cheka

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,667
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ ameonyesha hataki mchezo baada ya kumchakaza Mchina, Chengbo Zheng katika raundi ya kwanza tu.

Pambano hilo la raundi 10 limefanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kwa kuwa kila bondia alijitapa awali.

Wakati watu walikosa burudani ya pambano la utangulizi la Cosmas Cheka dhidi ya Jason Bedemen raia wa Afrika Kusini ambaye aligoma akidai amebadilishiwa bondia na pambano lake kuondolewa ubingwa, hivyo nguvu zote zikaelekezwa kwenye pambano la Dulla Mbabe na Mchina huyo.

Wakati wengi waliamini pambano litakuwa na ushindani mkali, Dulla alishambulia kwa kasi na kumuangusha Zheng ambaye alijikongoja na kuendelea.

Lakini ikionekana kama atatulia, Dulla alimsogeza kona na kupeleka ngumi nne mfululizo ambazo zilimbaliza na kumaliza pambano kwani baada ya Zheng kwenda chini, hakuweza kuinuka tena na ikawa kwaheri.
=======

Yale ya Mike Tyson na Francois Botha.
 
Akaze zaidi, atafika mbali! Asibweteke na huyo mchina..

Mchina anaonekana hata boxing hajui... promoter amtafutie mabondia professional
 
Dulla mbabe hakucheleweshi mwisho raund 3 tu ndo historia yake. Jamaa atafika mbali sana ana uwezo mkubwa wa kupambana na nidhamu ya kutosha mchezoni
Pia yupo mwingine anaitwa Alphonce Mchumia Tumbo na yeye yupo vizuri sana
Kipindi cha nyuma kulikuwa na jamaa anaitwa Awazi Tamimu sijui kaenda wapi huyu kijana
 
Mchina muuza viatu wa kariakoo na uzalendo wapi na wapi.. Au mkuu hujaelewa tunachoongea?
Uzaelendo ninaouzungumzia ni kuwa tujifunze kupenda vya kwetu sio kila siku tukiona watanzania wenzetu wakifanikiwa tunaanza majungu kama wewe hapo uliposema "wameleta muuza viatu wa kariakoo"
 
Uzaelendo ninaouzungumzia ni kuwa tujifunze kupenda vya kwetu sio kila siku tukiona watanzania wenzetu wakifanikiwa tunaanza majungu kama wewe hapo uliposema "wameleta muuza viatu wa kariakoo"
Utakuwa hujanielewa. Hapo mbongo kampiga mchina.. Hata jana kwenye pambano watu walikuwa wanasema kuwa huyu mchina gani kaletwa kapigwa sekunda ya 48. Anatoka china kweli au ni muuza viatu wa kkoo.
Mkuu we kichwa ngumu sana ee
 
Back
Top Bottom