eyetyna
Senior Member
- Jun 24, 2011
- 148
- 17
Habari wana JF,
Kheri ya mwaka mpya wana jukwaa pendwa lenye maendeleo kwa kila anayepita hapa.
Mwaka huu nimedhamiria kufungua duka/fremu la vitu vya kila aina kwa jinsi zote( ke/me), lakini pia vitu vingi vitakuw dukani kwa order za wateja na vingine vitabaki dukani.
Tatizo linakuja pale ambapo nitaka kulifanya duka liwe la tofauti na maduka mengine tuliyoyazoea, natamani nifanye kitu kidogo lakini kiwe kikubwa kwangu na kwa wateja wangu.
Huwa naagiza vitu kutoka nje, UK, ENGLAND, JAPAN, CHINA,SOUTH AFRICA etc,inategemea na mteja anataka kitu gani, kama ni nguo, viatu, saa, perfume, power bank,i pad cover, phones cover, etc) .
Biashara hii nilianza rasmi mwaka jana kwa kununua vitu kwenye mitandao na kuwauzia wanaonizunguka, lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda nikawa napata matokeo mazuri kutoka kwa wateja na kunilazimu kujibana na kuona umuhimu wa kuwa na sehemu(fremu) ili iwe ni biashara inayoeleweka.
Naomba mnisaidie wana JF, kwenye mawazo,
Sitaki nifanye biashara hii iwe ni kama maduka mengine (boutique) nyingine.
Kuanzia designing ya vitu ndani, rangi za ukutani, utoaji wa huduma, na mpaka bidhaa inapomfika mteja, au anapokuja dukani ajisikie amefika sehemu ya kipekee.
Ni vitu gani unategemea kukuta vitu gani ukienda kwenye maduka haya ya nguo?
Ni vitu gani huvipendi kuviona au kuvisikia pindi unapoingia kwenye duka la nguo?
NI wapi huwa tunakosea sisi wamiliki wa maduka ya nguo/vitu mbalimbali kwnye biashara hii?
Nini kifanyike ili biashara hii iweze kuwa bora na sio kuona kwa mazoea?
Karibuni kwa mawazo.

Last edited by a moderator: