Huko Moshi na Arusha hivyo vitabu vya sheria viuzwe ili wanunuzi wakasome sheria chuo gani?!.
Kwa kukusaidia tuu, wauza vitabu ni wafanya biashara hivyo wataweka vitabu vitakavyo nunulika na wateja wao.
Kwa vile Watanzanzania hatuna utamaduni wa kujisomea, maduka ya vitabu hawaweki professional books sehemu ambako hakuna chuo cha sheria.
Wanunuzi wakubwa wa vitabu ni wanafunzi wa somo husika, ambapo Arusha hakuna chuo.
Nenda Case Bookshop Uhuru Rd pale jirani na Meru Pharmacy utaweza kupata Law Reports ila wana catalog ukilipia wanakuagizia special order, hivyo ndivyo wafanyavyo mawakili wa Arusha.
Its cheap ukija Dar, maduka kibao. Duka kubwa la vitabu vya sheria ni liko pale kona ya Nkurumah na Mnazi Mmoja opposite na Co- Cabs.