Duka la mangi: Tunduma/Kahama

Mr_S

Senior Member
Apr 2, 2022
108
88
Habari za muda huu wanachama wa jukwaa la Biashara.

Nimekuja kwenu leo hii nikihitaji dira ya wapi ni pazuri zaidi kwa biashara ya duka la mangi kati ya Kahama au Tunduma.

Kwa kifupi nimefanya ajira Arusha kwa muda mrefu sana, takribani miaka miwili nikaacha na kuanza kuuza duka la Mangi hapa Usariver. Kwa ujumla biashara ilikuwa ya kawaida, ilikuwa na siku nzuri na siku zilizokwenda tofauti. Lakini nimefikia mkataa wa kwamba nataka kutafuta changamoto MPYA na kubadili mazingira. Nataka kuondoka hapa Arusha na kwendA KAHAMA au TUNDUMA.

Nimechagua hizo sehemu mbili kutokana na kusifika kuwa na mzunguko wa biashara. Hata hivyo ni ngumu kwangu kuamua wapi HASA pa kwenda kutokana na ukweli kwamba SIJAWAHI kufika popote kati ya sehemu hizo, sijui gharama za maisha na aina za biashara ambazo zinakubali sana huko. Lakini pia maamuzi yangu yanatiwa ukakasi na mambo yafuatayo ambayo yamesemwa sana na watu kuhusu sehemu hizo.

1. Nikisema ntaamua kwenda Tunduma basi napata ukakasi kila nikikumbuka mambo ambayo watu wanasema kuhusu mahali hapo kwamba kwanza hakuna maji, miundombinu duni na ni "sehemu ambayo biashara pekee inayokubali ni MAGENDO tu! eti biashara nyingine zote zinafeli labda uwe na mtaji mkubwa".

2. Nikisema niende Kahama basi wazo langu litatiwa ukakasi na uvumi kwamba eneo hilo lina mzunguko kutokana na mgodi wa buzwagi. Kwamba siku ambayo mgodi huo utafungwa sehemu hiyo itapoteza kila kitu kutia ndani watu na mzunguko uliopo hapo. Ukizingatia hivi karibuni kumekuwa na seke seke la kwamba siku inakuja ambapo wachimbaji wadogo wataondolewa na migodi itafungwa. Nawaza vipi nikifika pale nikajiwekeza na kabla biashara haijachanganya "migodi ikafungwa ?", Ntakuwa nimeangukia pua.

Wataalamu, wenyeji na wajuzi wa haya maeneo naomba muongozo wenu ili nifanye maamuzi yenye 'low risk', nataka nifanye shughuli ya duka la mangi na mipango yote ya kuhama ilishaanza, nipo mbioni kukata tiketi pia.

Special request kwa moderators, tafadhali msiunganishe uzi huu na ule uzi wa Kahama vs Tunduma. Nimeusoma ule uzi na nimekosa maelezo ya msingi ninayoyahitaji.

Natanguliza shukrani kwa yeyote atakaejitoa kunipa dira.
 
😂😂😂😂aiseee watu weusi ni janga kubwa
Sasa umeshindwa kutumia hizo changamoto kuzigeuza fursa kwako?kama maji ya tabu peleka maji au itumie fursa hiyo.kwahuo uandishi wako nakushaur bakia hapo hapo usariver
 
Asante sana kwa ushauri wako. Hapa usariver nimeshaamua kuondoka. Nishaishi sana hapa nataka nibadili mazingira na nikutane na changamoto mpya.
 
Sijui kwann unatamani mahali na hujafika..

Ukisikia story na kupeleka ela zako huko mkukumkuku utaambulia patupu ndugu.

Kama una mtaji jaribu kwenda Tunduma then Kahama... panda bas huko kasafishe macho, angalia mitaaa yenye watu wengi, mzigo unavotoka( kakae kwenye biashara ya mtu.. yani asubuh had usiku) then jipime wewe na matamanio yako.

Nikitakie kila la kheri
 
Asante sana kwa ushauri wako kaka!
 
Asante sana kwa ushauri wako kaka!
Usijal Kiongozi... usipeleke huko hela na usifunge biashara Arusha kabla hujapaelewa huko...

Ila ningekuwa wewe ningefikiria zaid Dar..... au Miji mipya kabisa Dodoma...
Tatizo ndio hilo gharama ya kufanya survey hayo maeneo kws upande wako

Mungu akuongoze ipasavyo ndugu.
 
Buzwagi si ilifungwa ile?, Anyway,, kule khm labda ufungue duka specialised,, yaani liwe na upekee fulani,, mfano unaweza amua kuuza chupi za kike tu, jumla na rejareja,, utawapata wateja wa wilaya za pembezoni,uza urembo tu na vitu vya gift,keki etc,,,
Uza vifungashio dizaine zote kwa jumla, 😁,pipi, choklet, juices, etc.
Lakini duka la mangi labda uotee sana location,, maana yako kila kona, ushindani mkali
 
Pamoja boss!
 
Kaka asante sana. Nitazingatia ushauri wako. Wauzaji wa jumla wa hivyo vitu huwa wanapatikana wapi ? Mwanza ?
 
Duka la mangi haliangalii mkoa,popote tu kikubwa location,we sema umeichoka arusha,ukifikiria kuhamisha hiashara mtaji chini xa milioni 5 ni kujidanganya komaa hukohuko arusha kama usa river haposomeki tafuta mitaa mingine
 
Wazo la kubaki Arusha sina kabisa. Hapa nawaza kuhama tu. Asante kwa ushauri hata hivyo
 
Habari za muda huu wanachama wa jukwaa la Biashara.

Nimekuja kwenu leo hii nikihitaji dira ya wapi ni pazuri zaidi kwa biashara ya duka la mangi kati ya Kahama au Tunduma.

Kwa kifupi nimefanya ajira Arusha kwa muda mrefu sana, takribani miaka miwili nikaacha na kuanza kuuza duka la Mangi hapa Usariver. Kwa ujumla biashara ilikuwa ya kawaida, ilikuwa na siku nzuri na siku zilizokwenda tofauti. Lakini nimefikia mkataa wa kwamba nataka kutafuta changamoto MPYA na kubadili mazingira. Nataka kuondoka hapa Arusha na kwendA KAHAMA au TUNDUMA.

Nimechagua hizo sehemu mbili kutokana na kusifika kuwa na mzunguko wa biashara. Hata hivyo ni ngumu kwangu kuamua wapi HASA pa kwenda kutokana na ukweli kwamba SIJAWAHI kufika popote kati ya sehemu hizo, sijui gharama za maisha na aina za biashara ambazo zinakubali sana huko. Lakini pia maamuzi yangu yanatiwa ukakasi na mambo yafuatayo ambayo yamesemwa sana na watu kuhusu sehemu hizo.

1. Nikisema ntaamua kwenda Tunduma basi napata ukakasi kila nikikumbuka mambo ambayo watu wanasema kuhusu mahali hapo kwamba kwanza hakuna maji, miundombinu duni na ni "sehemu ambayo biashara pekee inayokubali ni MAGENDO tu! eti biashara nyingine zote zinafeli labda uwe na mtaji mkubwa".

2. Nikisema niende Kahama basi wazo langu litatiwa ukakasi na uvumi kwamba eneo hilo lina mzunguko kutokana na mgodi wa buzwagi. Kwamba siku ambayo mgodi huo utafungwa sehemu hiyo itapoteza kila kitu kutia ndani watu na mzunguko uliopo hapo. Ukizingatia hivi karibuni kumekuwa na seke seke la kwamba siku inakuja ambapo wachimbaji wadogo wataondolewa na migodi itafungwa. Nawaza vipi nikifika pale nikajiwekeza na kabla biashara haijachanganya "migodi ikafungwa ?", Ntakuwa nimeangukia pua.

Wataalamu, wenyeji na wajuzi wa haya maeneo naomba muongozo wenu ili nifanye maamuzi yenye 'low risk', nataka nifanye shughuli ya duka la mangi na mipango yote ya kuhama ilishaanza, nipo mbioni kukata tiketi pia.

Special request kwa moderators, tafadhali msiunganishe uzi huu na ule uzi wa Kahama vs Tunduma. Nimeusoma ule uzi na nimekosa maelezo ya msingi ninayoyahitaji.

Natanguliza shukrani kwa yeyote atakaejitoa kunipa dira.
Nenda tunduma ila Kuna uchawi Sana hapo jipange maji Ni tabu na uwalifu Ni muda wote

Nina jamaa angu Apo anauza eltronic amekuwa tajiro sna ukifika niambie ili akupokeew
 
Daah! Boss umeanza kwa kunitisha. Nashkuru sana kwa ushauri wako lakini kwanini Tunduma na si Kahama licha ya changamoto za Tunduma ambazo wewe pia umezitaja
 
Back
Top Bottom