Si kosa lako Mzee mwenzangu Mtambuzi... tatizo hawa wajukuu zetu siku hizi wanauliza maswali magumu sana...Najuuta kusoma shule za Ngumbaru!
Jana usiku mwanangu Ngina kanistukiza na swali, akitaka kujua eti Senene wanaitwaje kwa kiingereza.
Nilijifaragua, kisha nikamwambia nitamjibu baadae, hata hivyo nikamtoroka nikaenda kulala, leo alfajiri nimewahi kuondoka bila hata kumuaga, maana nilijua atanikumbusha swali lake.
Najua nikirudi jioni nitapambana na hili swali, hebu wana JF niondoleeni hii fedheha!
Najuuta kusoma shule za Ngumbaru!
Scientific name: Grasshoper bukobeae
Common name; Senene
Jibu ndo hilo katoa Babu wa Loliondo.Kiingereza cha nsenene ni cricket, jina kama ule mchezo wapendao wahindi na watu wa australia. sawa sio Mtambuzi?