Duh... Netanyahu kayakanyaga aisee!

Watakupiga sana lakini huo ndo ukweli wakati Iran yupo kwenye mazungumzo ghafla Israel inaenda kumshambulia Iran ule kulikua ni Zaidi ya Ujinga sasa
Israel imevunjwa vunjwa vibaya na Iran. Siku nyingine Netanyahu hawezi kuanzisha tena vita na iran.
 
Sasa unajua lengo la Israel lifetime?
 
Ningeshangaa sana iran kupigwa na hayo mapapai ya kizayuni😄
Baada ya Marekani kuonesha nia ya kumsaidia Israel mapambano, Russia ikataka kuingia nayo imsaidie Iran. Ayatollah akamwambia Putin we tulia usiwe na shaka, hawa wote wawili nawamudu vizuri sana. Putin akatulia, na kweli Ayatollah kawamudu wote wawili.
 
Sawa, mleta mada hebu niambie Israel ameshaharibu sehemu zote alioona zilikuwa zikichangia kwa asilimia nyingi kumsaidia iran kukamilisha mpango wake wa Nuclear, na watu muhimu kawaondoa.

Sasa nakuuliza ulitaka apige makazi ya watu maana hicho ndicho kilichobakia! Mimi sioni kingine...

Na Labda hapa ungesema wameshindwa kumuondoa Ayatollah.

Na labda pia waIran hawakuwa na utayari kufanya mapinduzi.

Hayo mawili nafkiri yangeeleweka zaidi, yani Israel kucheza kwenye Anga la Irani akipiga kila anachotaka, na sijaskia kuna ndege ya Israel imedondoshwa, na huku Iran akimpiga Israel na kupiga anachopata nafasi ya kupiga, na unasema Iran mshindi?

Unafikiri Israel ingeenda kwa mfumo wa kubutua chochote anachokutana nacho huko Iran pangebaki salama?
 
Iran sio Palestina tuliwaambia nyie hamkusikia, Kilichompata Netanyau anajutia ujinga wake, hana hata lengo moja alilofanikisha, Ila Iran amekamilisha malengo yote, ndio maana Trump anataka hii vita isimame maana Israeli inaenda kuangamizwa na Iran.
 
Iran sio Palestina tuliwaambia nyie hamkusikia, Kilichompata Netanyau anajutia ujinga wake, hana hata lengo moja alilofanikisha, Ila Iran amekamilisha malengo yote, ndio maana Trump anataka hii vita isimame maana Israeli inaenda kuangamizwa na Iran.
Kwanza mimi sishabikii hii vita, ila nachoongelea hapa ni kuwa mfano mimi nilitaka kuingia ndani kwako kukunyang'anya silaha ambayo umekuwa ukiitengeneza kwa muda mrefu na unaelekea kuikamilisha, na umekuwa ukiniahidi kuwa ukishaikamilisha basi utanimaliza nayo, mimi nikafanikiwa kuingia ndani kwako nikaharibu kila mfumo wako wa kuitengeza hiyo silaha.

Je, wewe unaona kuna kitu kingine umebaki nacho cha kunitisha mimi?

Hebu assume katika makombora yote yaliyotua Israel ingekuwa ni bomu moja tu la Nuke, hapo Israel pangekuwa na maafa kiasi gani?
 
Ushahidi uliotolewa na shirika la nguzu za atomic mitambo ya Iran ya nyuklia ipo sama, hakuna dalili yoyote kua mitambo hiyo imeathirika, America mwenyewe ameshindwa kuleta madhara yoyote katika shambuluo lake, achana na huyo Israeli uwezo wake kwa Iran umedhihirika ni mdogo sana, hata Iran mwenyewe haihofii tena Israeli na ndio sababu Trump anataka hii vita isimame, maana Israeli hana uwezo tena wa kabiliana na Iran kwa hali yoyote. Msilolijua Iran hii vita amejiandaa nayo kwa muda mrefu, kitu ambacho Israeli hawezi kwenda nayo hata mwezi mmoja atakua amesha tepepeta vibaya sana
 
Unaongea kitu gani hapa?
Umeelewa post yangu nilokujibu?

Nimekuambia vile Israel ilikuwa inalenga, sasa Yeye anaona amekamilisha, wewe unasema vita ya mwezi, kwani alikuambia anataka kupigana au anataka kukomesha mambo ya Nuclear?

Elewa tofauti hapo...!!!
 
Mimi nakumbuka walisema hivyo baada Israeli kushambulia na hawajasema hivyo baada ya US kushambulia.
 
Hilo la kukomesha nyuklia ameshindwa, pamoja na US kumsaidia lakini pia nae kashindwa.
 
M
Mkuu usituumbue sisi Wairan wa Maneromango.
 
Mimi nakumbuka walisema hivyo baada Israeli kushambulia na hawajasema hivyo baada ya US kushambulia.
Alienza kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran ni US, baada taarifa kuzagaa kua hakuna madhara ndio na Israeli akenda kushambulia.
 
Hilo la kukomesha nyuklia ameshindwa, pamoja na US kumsaidia lakini pia nae kashindwa.
Unaongea nini wewe? Wenzio waajemi wanalia kilio cha mbwa mdomo juu, halafu wewe unaongea hivyo hovyo.
 
Hivi Kwa akili Zako Iran ni mijnga kiasi Gani kupiga bomu la nyuklia Israel ambayo ni Palestine? Wewe unafikiri ni kwanini Iran hajapiga kinu Cha nyuklia Cha Israel wakati yeye amepigwa kinu chake? Lakini alipga TU research center? Tumia ubongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…