GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,772
Wakuu; Ama hakika Mungu anajua kuumba... Naogopa kusema kuna watu
Amewapendelea lakini nisema tu kuna aliowapa zaidi kuliko wengine.
Nilikuja huku kijijini lushoto ndani ndani kumsindikiza Rafiki yangu ambaye amekuja
kuoa. Kuna mwanamke nimemuona ama kwa hakika sijawahi kuona mwanamke
aliyetimia kama huyo. Nilipanga kukaa huku siku moja tu lakini nililazimika kuongeza
siku 2 zaidi.
Ana weupe fulani ambao ulitaka kwenda kwenye maji ya kunde,amesuka mafungu
matatu tu ya nywele, ana mwanya ambao umenichanganya kwelikweli, mashavu yake
yamejengwa kwa vishimo vidogo 'dimples ' ambavyo akicheka vinashabihiana kabisa
na mwanya ambao unaleta mvuto si wa kawaida. Macho yake makubwa mazuri sijui ndio
yale wanayosema kama vikombe!!!!!!!
Kwa mwanaume mwenye shinikizo la damu huyu Mwanamke si vema akacheka mbele
yake, HAKI YA MUNGU NAAPA mimi tu ambaye sina tatizo hilo nimejikuta kama linataka
kunianzia sasa huyo mwenye hilo tatizo si itakuwa balaa, NASISITIZA ANAWEZA KUFA.
Umbo lake sasa, yaani amegawanyika inavyotakiwa. Ni mrefu wa wastani, si mwembamba
ana afya kiasi lakini hajaingia kwenye orodha ya watu wanene. Yaani huyu amekaa kabisa
kama namba nane... yaani haki vilee hii ndiyo namba nane hasa. Ana vidole vizuri virefu
vya mikono, huku urembo wake ukikamilishwa na miguu ambayo imejaa wastani. Kama
isingekuwa ni maneno ya kufuru ningesema huyu binti kapendelewa.
Akitembea sasa.... Ah! hapo sisemi sana.
Nimalizie tu kuwa nimejaribu kutafuta hata mtandaoni sijaona sura ya mfano wake hata hii
picha niliyoiweka haifikii hata Robo ya jinsi mwanamke huyu alivyokamilika.
NASEMA NITARUDI TANGA...... NITARUDI TU...!!! Labda waniwahi wajanja......