Duh, huyu mwizi Mandara alikuwa kiboko kwa kweli kila kesi BOT yumo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duh, huyu mwizi Mandara alikuwa kiboko kwa kweli kila kesi BOT yumo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 17, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,167
  Likes Received: 5,592
  Trophy Points: 280
  Nora Damian
  KADA wa CCM, Rajabu Maranda anayetumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh1.8 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa), jana aliunganishwa kwenye kesi nyingine ya wizi wa Sh5.9 bilioni, mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Wengine waliounganishwa kwenye kesi hiyo ni wafanyakazi wawili wa BoT, Ester Komu, ambaye wakati wizi huo unadaiwa kufanyika alikuwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Madeni na Bosco Kimela, ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa Benki.

  Kabla ya washtakiwa hao kuunganishwa, kesi hiyo awali ilikuwa ikiwakabili washtakiwa wawili, Ajay Somani na ndugu yake Jai Somani. Wakili wa Serikali, Frederick Manyanda alidai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama na kutenda makosa hayo kati ya Desemba 2004 na Mei 2005, Dar es Salaam.

  Alidai kuwa Maranda anakabiliwa na mashtaka manne ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa udanganyifu, wakati wafanyakazi wa BoT wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kuisababishia hasara benki hiyo ya Sh5.9 bilioni. Wakili huyo alidai kuwa Maranda alighushi hati za uongo na kuziwasilisha Benki ya Baroda Dar es Salaam akionyesha kuwa Thabit Mapunda ni mwanahisa wa Kampuni ya Liquidity Services Ltd wakati akijua ni uongo.

  Ilidaiwa kuwa kati ya Septemba 2 na Desemba 13, 2005 washtakiwa Maranda, Ajay na Jai walijipatia Sh3,975,820,000 kutoka BoT baada ya kudanganya kuwa Kampuni ya Liquidity imepewa deni na Kampuni ya M/S Societe Alsacienne De Construction De Machines Textiles ya Ufaransa.
  Wakili huyo alidai kuwa kati ya Septemba 2 na Desemba 13,2005 Maranda alijipatia Sh1,937,081,643 kutoka BoT baada ya kudanganya kuwa Kampuni ya Liquidity imepewa deni na Kampuni ya M/S Societe ya Ufaransa.
  Washtakiwa Komu na Kimela, wanadaiwa kuwa Agosti 30, 2005 wakiwa waajiriwa wa BoT waliisababishia hasara ya Sh5.9 bilioni ya benki hiyo. Baada ya kusomwa mashtaka hayo, upande wa utetezi uliomba dhamana kwa washtakiwa Komu na Kimela.

  Mshtakiwa Maranda alisema mahakamani hapo kuwa ametokea jela hivyo hajui chochote kinachoendelea na hata wakili wake alikuwa hajawasiliana naye. Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana anayesikiliza kesi hiyo alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa Komu na Kimela ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kila mmoja kwa kusaini bondi ya Sh1.5 bilioni na wao pia wasaini bondi ya Sh2 bilioni kila mmoja.

  Komu na Kimela walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Desemba Mosi, mwaka huu. Washtakiwa Ajay na Jai tayari wana dhamana katika kesi hiyo. Maranda na nduguye Farijala Hussein wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh1.8 bilioni za Epa. Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na kesi nyingine tatu za aina hiyo ambazo zinawakabili pia Komu na Kimela.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,167
  Likes Received: 5,592
  Trophy Points: 280
  Pamoja na hilo mungu anisamehe alipita siku moja ofisini aisee akawa anaongea na kabinti akamwachia laki tatu sie wa pemben tukapewa laki laki tulisikia kama mtu anataka kututoa utumbo nikamwambia mwenzangu aku mi situmii mpaka baada ya siku tatu asije nidai..masikini nakukja kumkuta kwenye gazeti kasheni miaka 5 nkasema yalaaaaaaahhhh sasa nazitumia kwa amani kabisa
   
 3. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,959
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Zirudishe BOT au zipeleke polisi
   
Loading...