Duh! Ghafla wife huyu hapa!!!

Duh! Ghafla wife huyu hapa!!!

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,211
Reaction score
35,863
Kimemkumba kisa rafiki yangu mmoja ofisini kwake,ilikuwa hivi;

Receptionist na wadada wengine wote hawakufika ofisini, Managing director (mtu wa makamo) akawa anataka chai basi huku na huku hakuna mdada hata mmoja wa kumtuma ikabidi ampigie mshkaji wangu (ambaye ni Internal Auditor) akamuomba kwakuwa kakosa wa kumtuma anaomba amtengenezee chai (huku akimtaka radhi kwa usumbufu).

Mshkaji kiroho safi akaenda akatengeneza chai akawa anampelekea ofisini kwa bosi lakini kabla ya kufika kwa bosi unapita reception.

Basi ile anafika reception hamadi Wife wake huyu hapa!!!!! (alikuwa town akaona amsalimie Mr fasta) Duh mshkaji ikabidi aanze kuinywa ile chai kuzuga!!!

Baada ya kuondoka wife jamaa mbio jikoni kutengeneza nyingine!!!!! Duh!!! hizi ofisi hizi!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom