Dudubaya asamehewa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Dudu B.jpg

Serikali ya Tanzania imemsamehe msanii, Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya baada ya kumfungia kwa muda usiojulikana kujihusisha na kazi za sanaa. Alifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) baada ya kukataa wito kuhojiwa kuhusu tuhuma alizozitoa katika mitandao ya kijamii kuhusu sanaa. Baraza hilo limeeleza kuwa Dudubaya alitumia lugha zisizo na maadili.

Hata hivyo, Januari 23, 2020 Dudubaya alijisalimisha Basata na kuomba msamaha lakini baraza hilo halikutoa uamuzi wowote kwa kuwa mamlaka ya kufanya hivyo ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Jana Jumanne Februari 11, 2020 msani huyo alikwenda katika ofisi za Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe kuweka mambo sawa.

Leo Jumatano Februari 12, 2020 katibu mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema Dudubaya amesamehewa baada ya kusikilizwa na Dk Mwakyembe.

Amesema Basata haikuwa na mamlaka ya kumfungia na aliandika barua ya kukata rufaa kwa waziri, “sheria ya baraza namba 23 ya mwaka 1984 na marekebisho yake yaliyofanywa mwaka 2006 inaeleza mtu yeyote akipewa adhabu na Baraza, sheria inampa nafasi ya kwenda kumuona Waziri na anachosema Waziri ndicho kitakachotekelezwa.”

Mngereza amewataka wasanii kuzingatia sheria kanuni na taratibu, “wasanii wana nguvu kubwa, wanapaswa kuishi kwa kufuta maadili kwani watu wengi wanawafuatisha wakiwemo watoto, pia haileti picha nzuri katika sanaa ikizingatiwa kuwa ni moja ya kipengele kinachoitambulisha nchi.”

CHANZO: Mwananchi
 
Angalau sasa amepata kiki nyingine, na media zitamtafuta ili ahojiwe ni jinsi gani alivyoathirika na ban, huku yeye akijua bila ban watu wasingemsikia baada ya konki master ku expire.
 
sasa hivi anatangaza matangazo ya firimasoni kwenye ukurasa wake wa instagram wale matapeli wanaorusha video kuwa wamepata mafanikio kutoka kwa wakala wa firimasoni
 
Safi sana. Makosa yake yamemfanya aonane na waziri.Kila lenye Kheri wa kwetu kaka Tumaini.
 
Hizo shughuli za sanaa alizofungiwa ni zipi mbona kila siku namuona kwenye shoo za wasafi huko mikoani? au shughuli za sanaa ni kutoa nyimbo mpya?
 
Naona mlezi wa WCB ameshamkingia kifua.

Shida hata akiruhusiwa kuendelea kufanya shughuli zake za sanaa haijulikani anafanya shughuli gani.

dodge
 
Konkiii.....hivi wale wasanii waliotajwa hawana vizibo walipima na kututhibitisha wabongo vizipo vipo imara?...l
 
Back
Top Bottom