Alichoongea Dude ni uongo wa dhahiri.
Kama jeshi letu la polisi lingekuwa linafanya kazi yake kwa weledi, ilibidi mara tu gazeti hilo lillipoanza kusambazwa kwa wasomaji, huyo jamaa awe keshakamatwa na polisi, kufanya formality ya kukamilisha upelelezi wao, ili ifuate hatua ya kumburuza mahakamani.
Upo ushahidi usio na mashaka yoyote kuwa Dude alishirikiana na huyo mtu ambaye hakutaka kumtaja jina, kuuvusha huo 'unga' toka Kenya kuja TZ, hasa hasa ushahidi wenye nguvu hapo ni yeye mwenyewe anakiri kuwa alipewa pesa elfu 50 ya Kenya na akakaa kimya.
Nitawashangaa sana polisi wetu, hasa kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya, kama wataamua kulikalia kimya suala hili, bila kumkamata Dude, wala kuitolea ufafanuzi stori hii, ambayo ameitoa mwenyewe Dude kwa hiari yake, bila kulazimishwa na mtu yeyote!!