Dubai: Kiongozi wa Hamas alibanwa pumzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dubai: Kiongozi wa Hamas alibanwa pumzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Kamera ya usalama inaonesha Mahmoud al-Mabhouh kiongozi wa Hamas yanafatwa na watu wawili Mkuu wa polisi Dubai anasema kikosi cha siri cha majasusi wa Israel, Mossad, hakina "hata aibu" kutokana na mauaji ya mwezi Januari ya kiongozi wa Hamas katika hoteli moja ya Dubai.
  "Sasa nina uhakika wa asilimia 100 kwamba Mossad walihusika katika mauaji" ya Mahmoud al-Mabhouh, alisema Luteni Jenerali Dahi Khalfan Tamim. "Nilikuwa nasema asilimia 99 lakini sasa naweza kusema asilimia 100."
  Al-Mabhouh, mjumbe mwanzilishi wa tawi la kijeshi la Hamas, alikutwa amekufa katika chumba chake cha hoteli Dubai Januari 20. Polisi wanaamini aliuawa usiku uliopita, na wametambulisha washukiwa 26 katika mauaji hayo.
  Israel ina kawaida ya kutokanusha wala kuthibitisha tuhuma zozote katika maswala ya usalama. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Liberman, hata hivyo, alisema mwezi uliopita kuwa hakuna sababu yoyote nzuri ya kufikiria kuwa Mossad walihusika katika mauaji hayo.
  Mapema Jumapili polisi wa Dubai walisema matokeo ya vipimo yameonyesha kuwa al-Mabhouh alipigwa sindano ya kumlaza kabla ya kubanwa pumzi.


  http://www.voanews.com/swahili/2010-02-28-voa1.cfm
   
Loading...