Unafikiri kuwa Tanzania ndiyo kuipenda Tanzania?
I wish Lowassa na kundi lake la Mafisadi wangelikuwa wanaishi nje.
Anyway, Utanzania uko moyoni mwa mtu na siyo kwenye JF au kurudi Tanzania. Hata Boss wa Marks and Spencer aitwaye Stuart Rose ambaye alishawahi kuishi zamani Dodoma, alirudi huko na kusaidia shule ambapo zamani walikuwa wanakaa. Huyu ingawa si Raia wa Tanzania (na wala hahitaji) anaweza kuwa Mtanzania zaidi ya akina Lowassa, Mkapa, Liyumba, Mgonja, Mramba na wengine wengi tu.
Mwisho niseme kimoja. Nashindwa kufahamu unachokisema hapa wewe ni kuipenda Tanzania au Uraia wa nchi mbili? Je mtu mwenye uraia wa nchi mbili, ina maana haipendi Tanzania? Mwenye wa nchi moja na anaishi Tanzania ina maana anaipenda sana Tanzania?
Kwangu mie kuipenda Tanzania ni kama ule mfano wa tembo na vipofu 7. Kila mtu anagusa kipande fulani na anaonyesha mapenzi yake. Ukianza kuwacheka wanzako kwa kuonyesha mapenzi kwa Tanzania kwa njia nyingine tofauti na unazotaka wewe ndiyo hiyo ninasema kuwa Mkuu wewe una UMIMI SANA. Kwa nini unapoteza muda kwenye nchi za watu? Kaa Tanzania hadi uje ufie hapa. Una Passport yenye kukuruhusu kutembea dunia nzima na mwisho unakuja kudai watu WARUDI Tanzania. Wewe hiyo Passport na hizo VISA zilizomo ndani za nini?
http://www.youtube.com/watch?v=t3vJ...E50EFE27A&playnext=1&playnext_from=PL&index=6