Dual citizenship | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dual citizenship

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TingTing, Dec 25, 2009.

 1. TingTing

  TingTing Member

  #1
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hili suala la dual citizenship limefikia wapi huko nyumbani? Mwenye habari kuhusu hili suala tafadhali tujuliane maendeleo kuhusu hili jambo.
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  bongo hawatambui dual citizenship!
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Lakini nimemuona Mhe Bernard Membe akisema kuwa uraia wa kuzaliwa hakuna anaeweza kuufuta na hivyo ndivyo inavyotambulika na hao dunia ya kwanza, sasa wale wenzetu waliochukua uraia wa nchi nyengine kwa kuandikisha si raia wa Tanzania kwa kuzaliwa? Moja na moja ni mbili au vipi?
   
 4. M

  Mwanaluguma Member

  #4
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Rudi nyumbani uwasaidie watanzania wenzako,uraia wa nchi mbili kwangu ni upuuzi mtupu,tutaiga wazungu kila kitu? wao wanafanya hivyo ili wapate nafasi ya kuhujumu.
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Acha roho korosho, LOOSER.

  Ukisoma maneno ya Membe ni kuwa Mzaliwa wa Tanzania na abaki kuwa Mtanzania. Hii inaweza kuwa ni kama One direction Valve. Mgeni hawezi kuchukua uraia wa nchi mbili ila Mtanzania MILELE ABAKI MTANZANIA.

  Wahindi wanayo hiyo. Wajapan nao wana hilo saaana. Wewe hata uowe Mjapan hawakupi URAIA na hutoa kwa nadra sana uraia wao. Ila Mjapan hata awe raia wa nchi gani au hata Rais (Fujimori wa Peru) akirudi kwao ni MJAPAN.

  Wakati mwingine inaweza kuwa kutoa HATI au KADI YA KUZALIWA. Hii inaweza kuwa inatumika mipakani kuingilia nchini Tanzania. Hivyo inaweza kuwa mtu ana PASS ya UK, ila ana HATI YA KUZALIWA YA TANZANIA. Akiwa nchi yeyote duniani na awe M-UK. Ila akirudi Tanzania, anakuwa MTANZANIA wa kuzaliwa.

  Kuna njia nyingi sana zinaweza kutumika kuwapa faida wazawa bila ya kuwaruhusu wakuja.

  Sasa wewe usiyeona faida, unajianika jinsi UPEO wako wa MWAMKO duniani ulivyo. Hao Wazungu kama wanataka kuja Tanzania na kuishi si wanafika na kuowa tu au kuolewa? Mzungu akija Tanzania leo anataka kuowa, si ataowa hata timu mbili za mpira kwa siku moja? Wewe kweli mtu wa kuja. Amka kijana, dunia hii sasa ni KIJIJI. AU unaungana na wenzio kufanya wanavyofanya au UNAKUFA. Yes, kama una wivu, go hang your self.

  Mtu huna ahata AIBU. Hapo ulipo umekaa kwenye kiti cha kizungu, meza (neno la Ki-Spanish) ya kizungu, computer ya kizungu, mtandao wa Wazungu, nguo na viatu vya kizungu na bado una bwabwaja kuwa tusiige wazungu. Shame on you. Litanzania linchi kubwa sana. Acha tuchanganye damu labda itasaidia kuongeza asilimia kutoka 30 nakuwa walau 49% ya WASIOFUATA UPEPO anaowasema Kikwete.

  Work up kijana. Mzungu kama anataka kuja kuiba basi wala hahitaji kupata URAIA. Atakuja na dola 5 na aondoke na dola milioni 5. Chonya wa Chilonwa wee.....
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Dec 25, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Na huyu naye ni "Great Thinker?"
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mpango ambao uko sasa hivi ni kuandaliwa kwa database ambayo itaandikisha watanzania wote walio nchi za nje ili kuweza kuwatumia indapo itahitajika kufanya hivyo mpango wa dual citizenship bado mchanga sana ingawa kuna watu wanaongea kwa juu juu ila wengi wanaopinga wanatoa sababu za kiusalama zaidi haswa kwa wale walio nje kurudishwa nyumbani kufanya kazi tena .

  Hata hivyo kutokana na kukua kwa technologia haswa za mawasiliano mtu anakuwa hana sababu za kuwa na uraia wa nchi mbili kama nia yake ni kufanya kazi sehemu zingine za dunia ni kwa nchi kuhakikisha ina watu wake na vituo vyake vya kisasa vya kuwasiliana kama tatizo ni wataalamu
   
 8. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna tishio la usalama wowote ule. Kenya, Uganda na Rwanda wameruhusu DC na mpaka sasa hivi hakuna tishio lolote la usalama lililotokea dhidi ya nchi hizo. Ni roho ya korosho tu miongoni mwa Watanzania walio wengi wakiwemo hao viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi. Wakati huo huo wanapiga debe Watanzania walio nje wawekeze nyumbani lakini hawataki kuruhusu DC kwa visingizio mbali mbali ambavyo ni vya kipumbavu tu.

  Akitokea mtoto wa Kitanzania (Baba Mbongo na Mama Mbongo) wamehamia nchi nyingine kupata nafasi ya juu ya uongozi katika moja ya nchi za magharibi basi wote tutataka kumkumbatia yule ni mbongo mwenzetu. UNAFIKI MTUPU!
   
 9. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana mkuu, umenikuna mpaka natoka unga. itabidi nikugongee thanks.

  mtu mzima hataki kurudi nyumbani anabangaiza apate uraia wa nchi nyoingine utadhani hana nchi yake. hawa ndio wanaotutia aibu huku ng'ambo. nikipata nafasi ya maamuzi siku moja msahau kabisa huyo punda anayeitwa uraia wa nchi mbili.

  mi niko ng'ambo kwa sasa naingia na kutoka karibu kila nchi ninayotaka bila matatizo ya kunyimwa au kucheleweshewa viza na nina uhakika wa kuendelea kukaa huku niliko (kama nitataka) ng'ambo kwa muda wote nitakaopenda. lakini uraia wa nchi tofauti na tanzania hata ukiniletea bure kwenye karai sichukui. upuuuzi mtupu.

  nimetembea sana dunia sijaona nchi nzuri kama tanzania! jamani watanzania turudi nyumbani tujenge nchi yetu, sio mkae huku mkiuliza tanzania imewafanyia nini mje kula.

  mimi narudi februari mwakani.

  jamani kila anyetaka kurudi aandike hapa anarudi lini sio huu upuuzi wa dual citizenship!.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hadi wakakupa VIZA za kuingia na kutoka EUROPE nzima si ulisota sana. Pia kila ikiisha inabidi uende kuomba. Unalipia shule, matibabu na takataka nyingine kwa wingi zaidi ya ungelikuwa raia wa pale. Na nafikiri utakuwa unaishi peke yako maana ungelikuwa na familia ndiyo ungelielewa umuhimu wa kuwa RAIA ya nchi unayoishi.

  Na wewe unaonekana utakuwa ni mtu MBINAFSI SANA. Kama wewe umeshiba basi wengine wote wanaweza kufa njaa. Sasa ulisubiri nini kurudi miaka yote hiyo hadi MKATABA wako unakwisha na ndiyo unajifanya UNAIPENDA sana Tanzania na unarudi february na siyo mwaka juzi?

  Kuna wengine wanakuja wakiwa watoto kwa sababu tu wazazi wao wamehamia huko. Ila wao milele wanataka kuwa Watz na kusadia kule. Nina mshikaji wangu yuko UK huwa akija Tanzania ananisimulia jinsi wanavyomtumia kuandikisha mikataba ya UJENZI. Nikiangalia MIKATABA mibovu inayoandikwa hapa kwetu Tz, huwa natamani nimuombe awafundishe watu wa madini, Tanroads, wizara ya ... nk kuwa ni vitu gani wawe macho wakati wanafanya mikataba.

  Na wewe unaonekana ni walewale ambao WAMESOMA ila HAWAJAELIMIKA.

  Hamna kingine zaidi ya ROHO KOROSHO. Na nikichunguza sana nafikiri au unaandika ukiwa TANZANIA na ukweli ni kuwa wewe pia ni roho korosho au unaandika wakati TAYARI ULISHAMLIPUA MSOMALI. Nyie ndiyo watu ambao mafanikio yenu yamekuja kwa shida sana na mnataka wote wasote kama nyie. Masikini wa roho YARABI.
   
 11. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana Sikonge umemaliza kila kitu na hawa WALIOSOMA lakini HAWAKUELIMIKA Tanzania tunao wengi sana.
   
 12. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  masikini, unaongea kitu usichojua!!!!!!!!!!!!!!!!
  1.
  kama wewe ulisotea viza, mzee nikujuze kuwa si wote wanasotea viza!!!!!!
  uliza wazoefu watakuthibitishia.
  2.
  unasema mi mbinafsi, labda hapo ni changamoto tu na nitaifanyia kazi kwenye kampeni zangu.
  3. huku niliko nina familia na nitakuwa nayo hadi nitakaporudi

  4.
  mi naingia na kutoka bongo mara nyingi tu kwa mwaka, kwa sasa wala siko ulaya, niko mashariki ya mbali kwa ajili ya sikukuu na baadaye nitamalizia kwa makongamano huko huko mashariki ya mbali na mwisho wa hayo makongamano ni februari ndo narejea nyumbani.

  5.
  sijashiba mzee, ningekuwa nimeshiba sasa hivi ningekuwa naishi arumeru kwani ndiyo sehemu ninayopenda zaidi kuishi hapa duniani! huku kote nahangaika tu na kutafuta maisha. namuona mkapa, aliposhiba alienda kule alipopaona pazuri zaidi licha ya kutembea dunia yote aliend lushoto!

  6.
  kupinga watu kuzamia ng'ambo si roho orosho bali uzalendo. mtu akienda sawa lakini arudi sio aishi hukohuko wakati kasomeshwa na hela zetu! taifa lake linamuhitaj, yeye anafanya vibatua huko kwa sababu ya vijisenti? nani kakwambia tanzania hakuna maisha mazuri? acheni ulimbukeni!

  7.
  kuna ushamba fulani umeonyesha kwenye aya yako ya mwisho. mimi nikudanganye wewe kuwa niko nje wakati niko tanzania? hahahaaaaaaaa......... mambo ya vijiweni bwana!!!!!! hahaaaaaaaaaaa labda wewe ndivyo unavyofanya! lakini nakupa pole kwa hilo.

  8.
  nakushauri mpendwa (tena leo ni xmass) tuipende nchi yetu, tukienda ng'ambo kutafuta maisha, tukumbuke kwetu kama anavyotuasa rais wetu, turudi, sio tupiganie uraia wa nchi mbili tubaki hukohuko.

  asante mkuu, ubarikiwe na wote waliokuunga mkono
   
 13. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Watanzania tunafungwa magoli ya kuotea siku zote, Viongozi wangapi wana uraia wa nchi mbili mbona hatuwasemi? Mandela kapewa uraia wa nchi hii ikowapi sheria hiyo?
  Tuseme ukweli tu hakuna sababu ya usalama wala kitu gani mbona mafisadi wako hapa hapa na wao hawakamatiki jee tuseme na wao wana uraia wa nchi mbili?
  Hakuna kitu walala hoi ndio wajinga wao nchi hii haitoendelea kamwe
  Ninaandika wakati nina hasira kweli

  Hivi Ndulu ana tumia mamilioni ya hela usama wetu uko wapi wa hela zetu, Yuko wapi Mchungaji hata jina lake limenitoka kweli makabachodi wanakula nchii na viongozi sisi walala hoi eti kilimo kwanza
   
 14. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mgombea ubunge tafazali nyamaza kwani,
  Nina hasira kweli na watu kama nyinyi, wewe umeifanyia nini nchi hii leo unasema eti kwenye KAMPENI YANGU hivi bado hilo tumbo ulilokuwa nalo unataka hata kule kwetu Kiwawa na Mbwemkuru tusile machungwa na watu wetu, huko kula kote na bado unataka ubunge kwa lipi utakalofanya zaidi ya kuiba,
  Unataka kusema kule Dodoma ma Phd wote wanafanya nini zaidi ya kuwaibia walala hoi, wamesomeshwa kulitumikia Taifa sio kwenda kulala Bungeni, bado tukupe kula hapa Tanzania kweli Tanzania shamba la bibi
  Huyu anatoka huko anakuja hapa eti aise nina hasira na wanasiasa kweli
   
 15. L

  Lampart Senior Member

  #15
  Dec 25, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivyo Kenya na Uganda wenzetu tayari wamesharuhusu?
  Labda kwetu hilo tishio lipo kwa upande wa ZNZ, kwani 40% ya Wana-znz wapo nje.
   
 16. M

  Mende dume Member

  #16
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani maoni ya wasomi wenu haya hapa:-
  UDSM "scholars" Say NO To Dual Citizenship Manji Supporter [​IMG] 12th April 2007, 02:23 AM
  Uraia nchi mbili NO - Wasomi UDSM
  Wakati Wabongo wengi walioko nje ya nchi wanafagilia muswada wa kuwa na uraia wa nchi mbili, wasomi wa UDSM wametolea nje suala hilo.

  Wasomi hao wamedai hiyo ni janja ya Watanzania wachache kwa maslahi yao binafsi na wala haina manufaa kwa wananchi wengi wa nchi hii.

  Wamesema kuwa endapo kwenda Wabongo hao wana mapendo na nchi yao, basi ni bora warejee nchini kuendeleza nchi yao.

  Hayo yalisemwa wakati wa mjadala ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Taaluma -IDS ya Chuo Kikuu cha Dar baada ya pande kutoka kwa Rais JK aliyetaka kuwepo kwa mchakato wa suala hilo.

  Washiriki wa mjadala huo waliongeza kuwa sheria hiyo itaibua hasara kuliko faida kwani hata baadhi ya wageni wataruhusiwa kumiliki ardhi kwa kuwa watakuwa na uraia wa Bongo.

  Maslahi ya wachache yasiingilie maslahi ya taifa kwa kuwa si rahisi kwa mtu mmoja kutumikia kwa dhati uraia wa nchi mbili, walisema washiriki hao.

  Walizidi kushindilia kuwa sheria hiyo mpya itawanufaisha Watanzania wachache wanaoishi nje ya nchi na si Wabongo wanaoishi nchini, kwa hiyo ni bora maslahi ya wengi yazingatiwe kwanza.


  http://www.darhotwire.com/dar/Habari.../11/31633.html

  Maoni yangu, ni suala la DC sio baya. Wenzetu katika hali ya uzalendo, hawafikirii uraia wanafikiria permanent residence kama ndo unataka kuingia na kutoka bila matatizo. The fact kwamba tunazungumzia DC, tunakubaliana kuwa utanzania is the best and sort of hatupo tayari kuupoteza! Why sufer, force tz to accept, je waki accept hizo nchi nazo zikageuza sheria zao, kuwa wao kwao hawaaccept entrants with DC?

  wazungu wanatuchezea akili na sisi n´tunageuka tu kama midori, kama wachunguzi anaglieni shule zao, kwanza course nyeti hawachangamani na watu wa developing world afu ada sisi tunalipa mara tano hadi 10 ya wao in a case of europe, angalia scandnavia wao hawakuwa na tuition fee for years that has attracted many immigrants lakini sasa wanaona wahamiaji wanatosha, tayari wana ingiza ada, ila cheap fo EU members and very limiting kwa wenzangu na mimi!

  sasa viongozi wetu, midori na sisi tunakuwa midori mwenye afadhari haonekani.

  hebu great thinkers tuambizane kinagaubaga DC kwa mwananchi wa kawaida ina msaaidiaje? i do not understand, patriotically unakuwa upo wapi? unauraia wa US, na Afdhastan, umerudi zako home kwa bibi, unakutana na vita na wewe unapaswa kusaidia ndugu zako, baada ya vita unarudi marekani, unachanga fungu kusaidia Vita Afghan, which is which.

  seems 70% ya upepo inaweza kupanda, maana we have no context! utalii na wildlife tunajifunza jamaica na Saudia, forgeting kuwa wao utalii is something different from ours! Mvua tunaenda thailand, ila DC ndo tunaangalia Uganda na Rwanda.
  kweli either way we are fucked
   
 17. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu punguza hasira. nchi hii ni yetu sote. na ndio kampeni yetu kuwa mafaniko yetu tufaidi sote. sasa tukianza kuumana badala ya kushirikiana tutafika kweli? lete hoja zako si kusema wengine hatutakiwi kushiriki uongozi wa taifa letu.

  ukiniuliza nimefanya mamnapi kwa taifa langu ni mengi mno. nimetumikia taifa langu kwa kipindi irefu sana nimeanzia ualimu, nikafanya maofisini. nimefanya wizara za kazi, miundombinu na elimu, pia nimewahi kuwa mtaalam mshauri kwenye NGO moja ya kimatafa ya dakar senegal nk

  kusema sijaisaidia nchi yangu ni kupotosha!
   
 18. L

  Lampart Senior Member

  #18
  Dec 25, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndugu TingaTinga,

  Hili suala naona limekufa. Labda tutakapomchagua Dr. Slaa kuwa Waziri Mkuu, Zitto kuwa Foreing Minister na Mbowe kuwa Mr President, labda hapo tutakuwa na tamaa ya dual citizenship, lakini with CCM at the helm, there is no hope at all!
  Hebu tujikumbusheni hapa chini kidogo:


  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=+3]National[/SIZE][/FONT]
  21.05.2009 1118 EAT
  Tanzanians opposed to dual citizenship, says JK

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]From Correspondent Los Angels

  TANZANIANS are opposed to dual citizenship and the Government has shelved the issue for now so that people are educated on the matter.

  This was stated by President Jakaya Kikwete when he addressed Tanzanians living in South California on Tuesday.

  He said the issue of dual citizenship was not popular with most people in the country and it was being resisted.

  “I think there is a point in having dual citizenship but the truth is that this issue is not accepted by your brothers and sisters at home. The issue of dual citizenship faces resistance,’’ Kikwete noted.

  However, he said the Government would continue educating the people on that although he emphasized that the issue was received negatively right from the beginning.

  Tanzanians living in Los Angels and San Francisco are for dual citizenship. They wanted the President to tell them why the Government was delaying to approve it.

  Meanwhile, Kikwete has reiterated his call to Tanzanians living abroad to invest at home.

  He said they shouldn’t bother striving to mull big development projects because that was being undertaken by the state.

  “If you get a good investor bring him/her home.

  My advice to you is build at home first to justify why you qualified to live abroad,” he emphasised.

  He warned them over the danger of finding nowhere to shelter when they returned if they forget to build at home.
  [/FONT]​
   
 19. L

  Lampart Senior Member

  #19
  Dec 25, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MODS ondoweni hilo neno kwa haraka kabla watoto wetu hawajaliona na wekeni ****
  Msalieni Mtume jamani (SAW), leo ni siku ya YESU!!!!
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unafikiri kuwa Tanzania ndiyo kuipenda Tanzania?

  I wish Lowassa na kundi lake la Mafisadi wangelikuwa wanaishi nje.

  Anyway, Utanzania uko moyoni mwa mtu na siyo kwenye JF au kurudi Tanzania. Hata Boss wa Marks and Spencer aitwaye Stuart Rose ambaye alishawahi kuishi zamani Dodoma, alirudi huko na kusaidia shule ambapo zamani walikuwa wanakaa. Huyu ingawa si Raia wa Tanzania (na wala hahitaji) anaweza kuwa Mtanzania zaidi ya akina Lowassa, Mkapa, Liyumba, Mgonja, Mramba na wengine wengi tu.

  Mwisho niseme kimoja. Nashindwa kufahamu unachokisema hapa wewe ni kuipenda Tanzania au Uraia wa nchi mbili? Je mtu mwenye uraia wa nchi mbili, ina maana haipendi Tanzania? Mwenye wa nchi moja na anaishi Tanzania ina maana anaipenda sana Tanzania?

  Kwangu mie kuipenda Tanzania ni kama ule mfano wa tembo na vipofu 7. Kila mtu anagusa kipande fulani na anaonyesha mapenzi yake. Ukianza kuwacheka wanzako kwa kuonyesha mapenzi kwa Tanzania kwa njia nyingine tofauti na unazotaka wewe ndiyo hiyo ninasema kuwa Mkuu wewe una UMIMI SANA. Kwa nini unapoteza muda kwenye nchi za watu? Kaa Tanzania hadi uje ufie hapa. Una Passport yenye kukuruhusu kutembea dunia nzima na mwisho unakuja kudai watu WARUDI Tanzania. Wewe hiyo Passport na hizo VISA zilizomo ndani za nini?
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=t3vJr8WcofQ&feature=PlayList&p=9BDECF4E50EFE27A&playnext=1&playnext_from=PL&index=6[/ame]
   
Loading...