Twilumba
Platinum Member
- Dec 5, 2010
- 13,577
- 16,440
WanaJF Habari za asubuhi hii, Katika Pitia pitia katika vipindi vya TV nimekutana na maneno ambayo ni mara yangu ya kwanza kuyasikia, kimsingi nimeona niwashirikishe ili wanajamvi wenzangu mkikutana nayo yasiwe mageni kwenu
Maneno hayo ni;
Fola- lenye maana sawa na hongera lakini tofauti na hongera za kawaida hili hutolewa kwa mama aliyepata Kujifungua Mtoto, kwa hiyo watu wanapokutana/ kwenda kwa ajili ya kumpongeza hutimia neno Fola.
Kivukomilia-ni neno lenye maana ya sehemu ya barabra iliyochorwa mistari mweupe kwa ajili ya kuvuka kwa miguu, maarufu kama Pundamilia
Jibodoa- Ni sifa anazojimwagia/Jinadi mtu/kitu kutokana na umahiri wake, jinaki ni neno linalofanana na jibodoa.