Nakuhakikishia Baba Enock, hakuna walichosawazisha. Fikiria kwamba wabunge wapinzani watakuwa wanauliza maswali magumu na ya mtego kwa waziri mkuu, na mawaziri wengine. Huyu mama kwa kufanya kazi aliyotumwa atakuwa anajitahidi kupangua yale anayohisi yataidhalilisha serikali, kwa kufanya hivyo atawachonganisha wananchi na bunge.
La pili, fikiria kuwa kundi la wabunge 'wapambana na ufisadi' wa CCM, bado litakuwepo (Mwakyembe, Kilango, Lembeli, Manyanya na wengi wataongezeka kutoka kwenye wabunge wapya); Kwanza kwa sasa wanajua kuwa wamehujumiwa kwa kuondolewa kwa kamanda wao Sitta, kwa hiyo watakuja kwa hasira. Wataichachafya serikali, huyu mama atakuwa anapangua, na atajenga makundi ndani ya bunge. Kiuhalisia ni kuwa wakati akina Mwakyembe walikuwa wanaheshimu kiti cha bunge kwa sababu spika alikuwa upande wao, kwa sasa watakuwa wanafyatuka kisawasawa, kwa hasira za kuhujumiwa kiti cha uspika.
Mwashoni itakuwaje.. Kwa kuogopa maamuzi ya wananchi hapo 2015, wabunge wa kuchaguliwa watakaokuwa upande wa mafisadi watakuwa kimya na kufanya kazi zao za kuunga mkono kwa njia ya kura peke yake. Hii itasababisha hoja nyingi ziombwe kuchangiwa na wabunge wanaopambana na ufisadi na hapo watapata nafasi ya kung'ara bungeni. CCM itapanic, na inawezekana kwa mara ya kwanza ikaawavua uanachama wabunge wake, kwa ajili ya kujilinda 2015...