DU! Goli la NNE.... CCM wanajifunga tena hapa.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DU! Goli la NNE.... CCM wanajifunga tena hapa....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Nov 11, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kuendeleza katika topic ya Jenerali ulimwengu kuwa CCM walishajifunga magoli matatu, yote yakifungwa na Makamba; (Hat trick), naona sasa Makamba anaongeza goli la nne kwa kusimamia kuondolewa kwa Sitta Katika uspika. What a goal......... Huyu jamaa naona sasa sio tu ataondoka na mpira uliotumika, bali apewe na vili vibendera vya waamuzi wasaidizi...
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hiyo ndiyo ccm husimamia maamuzi yake hata kama hayo maamuzi yatakuwa na madhara ndani ya chama wao huwa hawa jari ilimradi tu wanaotakiwa kulidhishwa wamelizika

  naimani hawatajutia maamuzi yao kama ilivyotokea ktk kula za maoni

  mapinduziiiiiiiii daimaaaaa
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inawezekana CCM hawajajifunga hilo goli la nne.
  Pengine wamerudisha goli moja sasa ni 3 - 1.
  Sidhani kama wanaweza wakafanya makosa mfululizo namna hiyo lazma kutakuwa kuna kitu tu.
   
 4. Shomoro

  Shomoro Senior Member

  #4
  Nov 11, 2010
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Halafu kwa nini maamuzi yote ya ovyo wanamwachia huyu mzee mwenye kiherehere ndio ayatangaze kwa mbwembwe? Nina mashaka sana na upeo wa Ma-kamba
   
 5. N

  Nyafi Member

  #5
  Nov 11, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio CCM chama ambacho kimesahau kuangalia na kusimamia maslahi ya wengi (wananchi) na kukumbatia maslahi ya watu wachache au kikundi cha watu. Kwa mtazamo wangu maamuzi kama haya ndio yaliuwa vyama vingine vya ukombozi Afrika kama KANU-Kenya na UNIP-Zambia na CCM wanaelekea huko huko. That's their final destiny people!
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Tuko

  CCM wamesawazisha - na sasa tupo kwenye muda wa nyongeza. Mchezo unavyoelekea wataondoka na ushindi maana Upinzani unaonekana kuweka UKUTA wakati bado dk 30!
   
 7. R

  Ramos JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakuhakikishia Baba Enock, hakuna walichosawazisha. Fikiria kwamba wabunge wapinzani watakuwa wanauliza maswali magumu na ya mtego kwa waziri mkuu, na mawaziri wengine. Huyu mama kwa kufanya kazi aliyotumwa atakuwa anajitahidi kupangua yale anayohisi yataidhalilisha serikali, kwa kufanya hivyo atawachonganisha wananchi na bunge.

  La pili, fikiria kuwa kundi la wabunge 'wapambana na ufisadi' wa CCM, bado litakuwepo (Mwakyembe, Kilango, Lembeli, Manyanya na wengi wataongezeka kutoka kwenye wabunge wapya); Kwanza kwa sasa wanajua kuwa wamehujumiwa kwa kuondolewa kwa kamanda wao Sitta, kwa hiyo watakuja kwa hasira. Wataichachafya serikali, huyu mama atakuwa anapangua, na atajenga makundi ndani ya bunge. Kiuhalisia ni kuwa wakati akina Mwakyembe walikuwa wanaheshimu kiti cha bunge kwa sababu spika alikuwa upande wao, kwa sasa watakuwa wanafyatuka kisawasawa, kwa hasira za kuhujumiwa kiti cha uspika.

  Mwashoni itakuwaje.. Kwa kuogopa maamuzi ya wananchi hapo 2015, wabunge wa kuchaguliwa watakaokuwa upande wa mafisadi watakuwa kimya na kufanya kazi zao za kuunga mkono kwa njia ya kura peke yake. Hii itasababisha hoja nyingi ziombwe kuchangiwa na wabunge wanaopambana na ufisadi na hapo watapata nafasi ya kung'ara bungeni. CCM itapanic, na inawezekana kwa mara ya kwanza ikaawavua uanachama wabunge wake, kwa ajili ya kujilinda 2015...
   
 8. W

  We can JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani, kuwavua ubunge ni kuongeza shimo la kaburi kwa chama! Kitakachotokea ni BORA LIENDE, na ndipo litakapoenda kweli.
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Haiwezekani makosa yawe mengi na mfululiza hivyo!! KInachotokea kwa sasa ni kupanga safu ya kulinda mafisadi!!!

  Hata kesi za kina mramba sasa zitamalizwa... maana kazi yake imekwisha!!!:doh:
   
 10. p

  pierre JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu sana kushindana na ukweli,unaweza kujitahidi kuficha ficha ila haiwezekani.CCM wamejaribu kwa kila njia kukwepa kwenda kaburini,ila kaburi la ccm liko palepale halikwepeki.CCM bye bye.
   
Loading...