DStv yashusha bei za vifurushi, yajaza chaneli

niko Compaq nimepunguziwa elfu 3,Mtu Yuko serious na Suti kali ananitangazia,Dstv yashusha bei...ungese huu
 
Asante sana DSTV kwa punguzo la bei na ongezeko la channels
 
Dstv Yashusha Bei za Vifurushi, Yajaza Chaneli

DSTV-4.jpg

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally akiwauliza swali viongozi wa Multchoice Tanzania (hawapo pichani).

dstv-1.jpg

Ronald Shelukindo akijibu swali la Saleh Ally.

Mwandishi wa habari kutoka New Habari, Hassan Bumbuli akiuliza swali kwa viongozi wa Multichoice Tanzania.

Meneja Mauzo wa Multichoice Tanzania, Salum Salum akijibu maswali ya wanahabari.

Wanahabari na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakibadilishana mawazo baada ya mkutano.

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania leo imetangaza huduma mpya kwa wateja wake baada ya kutangaza kufanya mapinduzi makubwa katika huduma yake ya DStv.

Kuanzia Novemba Mosi, mwaka huu wateja wa DStv wataanza kunufaika na punguzo la bei katika vifurushi vya Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kuwa DStv Premium imepokea punguzo la asilimia 16 kuanzia Novemba Mosi ambapo bei yake mpya itakuwa ni Sh 184,000. Pamoja na hayo pia kifurushi hicho kitakuwa na ongezeko la chaneli nane.

Kifurushi cha DStv Compact Plus kimepokea punguzo la asilimia 17 na bei yake itakuwa ni 122,500.

“Chaneli hizo mpya zitarushwa na Vuzu, AMP, Lifetime, Discovery, Crime & Investigation, History na Africa Magic Showcase. Compact Plus imeongeza pia chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa soka kupitia vipindi vya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi za Ulaya na Europa na zote zitapatikana kwenye chaneli ya Supersport 6 na 4,” alisema Shelukindo.

Aidha, kwa wapenzi wa filamu za kiafrika watafaidi kupitia Nollywood, wapenzi wa tamthilia za Kilatini, wataburidika na Telenovelas, filamu za Bollywood na sinema zitakazopatikana kwenye chaneli za ROK, Eva Plus na B4U.

Kuhusu kifurushi cha Compact, bei yake mpya itakuwa ni 82, 250 ikiwa ni punguzo la 5%, kitakuwa na Ligi Kuu ya England, Premier na ile ya Ligi Kuu Hispania, La Liga lakini wateja wameongezewa chaneli za ITV Choice, TCM na Super Sport 4.

“Kwenye kifurushi cha Dstv Family, bei mpya ni 42,900 na kimepokea ongezeko la chaneli tano za B4U Movies, Eva, Eva Plus, Supersport 4 na Fox. Na kuhusu kifurushi cha Dstv Bomba, kuna ongezeko la chaneli tatu na bei yake mpya ni 19,950 kutoka 23,500,” aliongeza mkurugenzi huyo.

Je wana jf kuna nafuu yoyote hapa kweli? kwangu mimi sijaona nafuu yoyote.

Chanzo : Global Publishers
Mimi naona bei za mishahara ya watu hapo na marupurupu mweee kweli hela sabuni ya roho.
 
kama huwezi mkuu nenda Ting
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] umenishushua kweli yaani!

Azam tu inantoa roho na elf15 yao!
Umeona eeh gen!
Inabidi wengine tubanane azam na startimes tu. Manake dstv ni gharama sana, hasa sisi ambao mpira ndio kipaumbele, 80k kila mwezi ni kubwa mnooo..
 
Mh,pamoja na hayo,bado wapo juu. Nianzaga na Compact plus,sasa nipo Compact,hawajanicomvince kurudi pkus but naona dalili zote bado kushuka Family. Sipendagi ujinga mm pia na mapato yangu
 
Ila hawa jamaa hata wasingeshusha wako mbali sana kiubora dhidi ya ving'amuzi vingine!
 
Lakini bado kuna cha kujiuliza je ni kitu gani leo kimefanya washushe bei hata kwa kiwango hicho kidogo wakati miaka miwili nyuma wamepandisha bei zao karibu mara dufu?
 
Tunachofata Dstv ni EPL tu hakuna zaidi, Ila mimi nilishaweka kambi hapa Dstv hawanipati ng'o.www.eplsite.com na www.mama.com nakula live game zangu zote EPL na champions league na international match zote hapa
 
azam kawa mpizani wa kweli tusubiri akipata haki ya EPL na UEFA mambo yatakua mazuri zaidi
 
Hawajapunguza chochote kwa wateja wengi ni "movies" na "sports" ambazo kwa "bundle" za simu unaweza kuangalia "movie" na "sports live" kwenye simu au "PC/Laptop" na ukipenda unaunganisha kwenye TV.

Mwenyevu uwezo wa kulipia Dstv lazima awe na uwezo wa kununua "bundle" na kutumia kila anapohitaji kuangalia. Dstv ukilipia uangalie usiangalie muda uliolipia ukiisha basi tena.

Wenye simu kuna apps nyingi tu na wa PC software kibao pia
 
DSTV-4.jpg

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania leo imetangaza huduma mpya kwa wateja wake baada ya kutangaza kufanya mapinduzi makubwa katika huduma yake ya DStv.

Kuanzia Novemba Mosi, mwaka huu wateja wa DStv wataanza kunufaika na punguzo la bei katika vifurushi vya Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kuwa DStv Premium imepokea punguzo la asilimia 16 kuanzia Novemba Mosi ambapo bei yake mpya itakuwa ni Sh 184,000. Pamoja na hayo pia kifurushi hicho kitakuwa na ongezeko la chaneli nane.

Kifurushi cha DStv Compact Plus kimepokea punguzo la asilimia 17 na bei yake itakuwa ni 122,500.

“Chaneli hizo mpya zitarushwa na Vuzu, AMP, Lifetime, Discovery, Crime & Investigation, History na Africa Magic Showcase. Compact Plus imeongeza pia chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa soka kupitia vipindi vya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi za Ulaya na Europa na zote zitapatikana kwenye chaneli ya Supersport 6 na 4,” alisema Shelukindo.

Aidha, kwa wapenzi wa filamu za kiafrika watafaidi kupitia Nollywood, wapenzi wa tamthilia za Kilatini, wataburidika na Telenovelas, filamu za Bollywood na sinema zitakazopatikana kwenye chaneli za ROK, Eva Plus na B4U.

Kuhusu kifurushi cha Compact, bei yake mpya itakuwa ni 82, 250 ikiwa ni punguzo la 5%, kitakuwa na Ligi Kuu ya England, Premier na ile ya Ligi Kuu Hispania, La Liga lakini wateja wameongezewa chaneli za ITV Choice, TCM na Super Sport 4.

“Kwenye kifurushi cha Dstv Family, bei mpya ni 42,900 na kimepokea ongezeko la chaneli tano za B4U Movies, Eva, Eva Plus, Supersport 4 na Fox. Na kuhusu kifurushi cha Dstv Bomba, kuna ongezeko la chaneli tatu na bei yake mpya ni 19,950 kutoka 23,500,” aliongeza mkurugenzi huyo.
 
Huenda wametabiri kuzaliwa kwa competitor siku za usoni
 
Kweli hatuko katika ulimwengu wa kijamaa na kama kuna mtaalamu mwambie akuingizie channel moja inaitwa sport 24 unaangalia epl match zote
mkuu hiyo sport 24 unaipata kwenye kingamuzi gani??...dstv au
 
Back
Top Bottom