DStv yashusha bei za vifurushi, yajaza chaneli

kamikaze

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
422
610
Dstv Yashusha Bei za Vifurushi, Yajaza Chaneli

DSTV-4.jpg


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).



Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally akiwauliza swali viongozi wa Multchoice Tanzania (hawapo pichani).

dstv-1.jpg


Ronald Shelukindo akijibu swali la Saleh Ally.



Mwandishi wa habari kutoka New Habari, Hassan Bumbuli akiuliza swali kwa viongozi wa Multichoice Tanzania.



Meneja Mauzo wa Multichoice Tanzania, Salum Salum akijibu maswali ya wanahabari.



Wanahabari na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakibadilishana mawazo baada ya mkutano.

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania leo imetangaza huduma mpya kwa wateja wake baada ya kutangaza kufanya mapinduzi makubwa katika huduma yake ya DStv.

Kuanzia Novemba Mosi, mwaka huu wateja wa DStv wataanza kunufaika na punguzo la bei katika vifurushi vya Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kuwa DStv Premium imepokea punguzo la asilimia 16 kuanzia Novemba Mosi ambapo bei yake mpya itakuwa ni Sh 184,000. Pamoja na hayo pia kifurushi hicho kitakuwa na ongezeko la chaneli nane.

Kifurushi cha DStv Compact Plus kimepokea punguzo la asilimia 17 na bei yake itakuwa ni 122,500.

“Chaneli hizo mpya zitarushwa na Vuzu, AMP, Lifetime, Discovery, Crime & Investigation, History na Africa Magic Showcase. Compact Plus imeongeza pia chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa soka kupitia vipindi vya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi za Ulaya na Europa na zote zitapatikana kwenye chaneli ya Supersport 6 na 4,” alisema Shelukindo.

Aidha, kwa wapenzi wa filamu za kiafrika watafaidi kupitia Nollywood, wapenzi wa tamthilia za Kilatini, wataburidika na Telenovelas, filamu za Bollywood na sinema zitakazopatikana kwenye chaneli za ROK, Eva Plus na B4U.

Kuhusu kifurushi cha Compact, bei yake mpya itakuwa ni 82, 250 ikiwa ni punguzo la 5%, kitakuwa na Ligi Kuu ya England, Premier na ile ya Ligi Kuu Hispania, La Liga lakini wateja wameongezewa chaneli za ITV Choice, TCM na Super Sport 4.

“Kwenye kifurushi cha Dstv Family, bei mpya ni 42,900 na kimepokea ongezeko la chaneli tano za B4U Movies, Eva, Eva Plus, Supersport 4 na Fox. Na kuhusu kifurushi cha Dstv Bomba, kuna ongezeko la chaneli tatu na bei yake mpya ni 19,950 kutoka 23,500,” aliongeza mkurugenzi huyo.

Je wana jf kuna nafuu yoyote hapa kweli? kwangu mimi sijaona nafuu yoyote.

Chanzo : Global Publishers
 
nasubiria punguzo lifike nusu.. punguzo la 2250 hata bado hawajanisaidia.. :p:p:p:p:p
Hata mimi haijanisaidia kabisaa, ingekuwa vizuri kama wangepunguza angalau asilimia kumi na nane kwa kifurushi cha compact then waongeze na mechi za UEFA, inabidi waangalie hali halisi ya kipato cha mtanzania
 
DSTV punguzeni compact plus to 105,000 TZS or below ,na wengi tutahamia hicho kifurushi.
 
Hawa Dstv vipi?punguzo gani hilo?hivi tunawang'ang'ania nini hawa hapa tz?nahisi ndio walifanya mpk Gtv wakafilisika ili waendelee kutesa waafrika,.magufuli ingia uko uondoa ukiritimba HUU wa dstv watanzania tunapenda mpira lakin hatuoni ligi za mataifa ya ulaya kwasbb ya dstv mpk uefa ni shidaa,kombe la dunia ni shidaa yani wmechukua kila kitu,.WATTO wakitanzania cjui Mpira watauona kwny tv gani wakat wazazi hawana uwezo wa kulipia dstv, siwapendi kweli.
 
punguzo bado sana halijafikia watumiaji wa hali ya chini
DsTv haipo kwa ajili ya "watu wa chini", sijui ni lini tutaelewa kuwa duniani kuna classes. Kumbuka hatuko zama za kijamaa, its capitalist economy my brother.

Kama huna uwezo wa DsTv karibu sana Digitek, no monthly subscription au uje Startimes, tshs. 6,000 tu unaangalia tv mwezi mzima.
 
heko kwa dstv...Premium inanihusu kuanzia mwezi ujaooo...kwaheri compact Plus...[HASHTAG]#VizuriVinagharama[/HASHTAG]
 
Sisi wa extra view mbona bado tunaumia tu, hebu punguzeni zaidi ili watu wengi tuhamie premium lakini pia watu wengine wahamie dstv
 
Wamepunguza kweli lakini sidhani kama wameconsult na wadau au kama walifanya homework yao vizuri. Tunashukuru lakini kwa walichofanya.
 
DsTv haipo kwa ajili ya "watu wa chini", sijui ni lini tutaelewa kuwa duniani kuna classes. Kumbuka hatuko zama za kijamaa, its capitalist economy my brother.

Kama huna uwezo wa DsTv karibu sana Digitek, no monthly subscription au uje Startimes, tshs. 6,000 tu unaangalia tv mwezi mzima.
umenishushua kweli yaani!

Azam tu inantoa roho na elf15 yao!
 
Haya mambo ya kupunguza vitu bei ni hujuma kwa serikali kukosa mapato, mnapunguza bei kwani wananchi tumeomba kupunguziwa? Anko akiwasikia mtakoma, kodi mtalipa ileile ya kabla ya punguzo. Siko serious sana.
 
DsTv haipo kwa ajili ya "watu wa chini", sijui ni lini tutaelewa kuwa duniani kuna classes. Kumbuka hatuko zama za kijamaa, its capitalist economy my brother.

Kama huna uwezo wa DsTv karibu sana Digitek, no monthly subscription au uje Startimes, tshs. 6,000 tu unaangalia tv mwezi mzima.
Kweli hatuko katika ulimwengu wa kijamaa na kama kuna mtaalamu mwambie akuingizie channel moja inaitwa sport 24 unaangalia epl match zote
 
Back
Top Bottom