Hahaahahahhah unajua running cost zao? unajua ni ligi ngapi wanazionesha?
ligi zote wanazozionesha ukijumlisha gharama zake hazifikii ligi ya uingereza, na ligi kama ya la liga, bundes liga etc sio exclusive kwa dstv unaweza ziona azam, startimes na kampuni nyengine hivyo wao dstv hawalipi hela nyingi, ni kwenye epl ndio wanapolipa hizo hela nyingi.
uingereza na marekani japo chanell zao zinachukua haki za nchi moja ila hawatozi hela nyingi sababu wanunuzi ni wengi hivyo wanaweza kulipa hio hela bila tabu
mfano NBC Ya marekani inayoonyesha ligi ya uingereza huko marekani imenunua haki hadi mwaka 2021, kuanzia mwaka jana (2015) na wamelipa dola bilioni 1 ambayo ni kama 2.2 trilioni ya huku kwetu.
wao NBC wana subscriber 480,000 hivyo ukifanya mahesabu rahisi utaona watu wengi wanavyosaidia
-2.2 trilion gawanya kwa miaka 6 hapa utapata kama bilioni 366, hii ndio hela wanayolipa kwa mwaka
-wana watumiaji milioni 480,000 kwa data za mwaka jana ukichukua 2.2 trilion gawanya 480,000 gawanya 12 unapata cost kama 63,500 hivo kwa mwezi
n Hata ukiangalia package zao zinakuwa hivyo hivyo add on ya kama dola 20 hadi 30 kwenye basic package.
huku dstv anatoza hela nyingi sababu ana wateja wachache na pia akitoka nje ya nchi yake anatozwa kodi.