Drop irrigation ya bei rahisi sana

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,333
5,285
Kwa mkazi wa Dar kwenye jua kali na uhaba mkubwa wa maji jaribu kutumia njia hii kuotesha miti kwenye eneo lako.

Chupa za maji ya AZAM LT 12 wanauza kati ya 2800 hadi 4000. Ukishayanywa maji, jaza maji ya kawaida, toboa tundu kwa chini pembeni kwa kutumia pini au sindano kisha weka karibu na mche na hakikisha maji yanadondokea usawa wa mche.

Kwenye shamba langu nimeotesha miche kama 30 na inakuwa vyema kwani dumu ninakaa hadi siku tatu ..

Happy new year..
 
Attachments

  • 1451734980981.jpg
    1451734980981.jpg
    134.8 KB · Views: 114
  • 1451735000598.jpg
    1451735000598.jpg
    136.2 KB · Views: 130
  • 1451735023813.jpg
    1451735023813.jpg
    143.8 KB · Views: 149
haya bana, hongera kwa ubunifu, nilijua masihara nilipoiangalia harakaharaka
 
kwa mkazi wa dar kwenye jua kali na uhaba mkubwa wa maji jaribu kutumia njia hii kuotesha miti kwenye eneo lako.
chupa za maji ya AZAM LT 12 wanauza kati ya 2800 hadi 4000 ukishayanywa maji .jaza maji ya kawaida toboa tundu kwa chini pembeni kwa kutumia pini au sindano kisha weka karibu na mche na hakikisha maji yanadondokea usawa wa mche.
kwenye shamba langu nimeotesha miche kama 30 na inakuwa vyema kwani dumu ninakaa hadi siku tatu ..

happynew year
Upo vzr kwa ubunifu, hongera na big up
 
hapo kwenye kila mche nimeotesha maharage punje 2
 
hapo kwenye kila mche nimeotesha maharage punje 2
Umefanya vizuri mkuu, hii ni njia mbadala ya drip irrigation (low cost drip irrigation) na hasa inatumia local material na wewe naona umetumia chupa za maji!! nna maswali kidogo, ukitaka kujua mmea wako umepata maji ya kutosha unajuaje? na je mmea unapata kwa kiwango kinachotakiwa?

USHAURI.
  1. Rekebisha heading isomeke drip irrigation na sio drop irrigation
  2. Usiwe unafunga/unakaza mfuniko kiasi kwamba maji yakashindwa kutoka kwenye matundu, legeza mfuniko wa chupa kiasi flani ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi.
 
Last edited:
upepo wa pesa asante ..ushauri wako nimeshaufanyia utafiti kabla sijaweka bandiko .
kuhusu kiwango cha maji nia yangu kuwepo unyevunyevu kwenye mti na kujiridhisha kama hata kama sina maji mengi uwepo uwezekano wa kuotesha miti
 
Kitaalamu inaitwa Field capacity. nimependa kipimo chako, kuwepo na unyevu nyevu (mind you, sio maji yaliyotuwama) kwenye shina la mmea ni dalili nzuri kwamba mmea una maji. Hii njia yako ntaifwatilia zaidi!! kila lakheri mkuu..
 
naweza kupateje mbegu za mapapai high brid nahitaji kuoteshe miche 150
 
Kwa mkazi wa Dar kwenye jua kali na uhaba mkubwa wa maji jaribu kutumia njia hii kuotesha miti kwenye eneo lako.

Chupa za maji ya AZAM LT 12 wanauza kati ya 2800 hadi 4000. Ukishayanywa maji, jaza maji ya kawaida, toboa tundu kwa chini pembeni kwa kutumia pini au sindano kisha weka karibu na mche na hakikisha maji yanadondokea usawa wa mche.

Kwenye shamba langu nimeotesha miche kama 30 na inakuwa vyema kwani dumu ninakaa hadi siku tatu ..

Happy new year..
Hongera sana kwa ubunifu wako. Nimeupenda sana. Hongera sana
 
Inategemea na tundu ulilotoboa ..ila mimi natobolea pin na inaweza chukua siku mbili na mche saa zote unakuwa na unyevyu ..

Usiulize sana maswali fanya kazi kama na wewe una cha ziada leta jukwaani
 
Back
Top Bottom