Bei hujulikana baada ya kufahamu unataka kujenga nini? Na gharama ya hilo jengo ni kiasi gani? Kumbuka, Ujenzi ni gharama na huwezi weka fixed price ya ramani kwa sababu kila mdau anakuja na hitaji lake la techinical style ambayo huhitaji gharama za ziada kufikia hitaji lako.
Tsh 40,000/= uliyonayo hata gharama za uchapishaji hiyo michoro kumi na mbili ya ramani utayotaka hazitoshi kabisa, sasa sijui unafikiria kuwa kila mtu ni draftmen hapa au ni kwa vigezo vya professional katika design, hivo wachoraji ndo cheap lakini ukija kwa designer ujiandae pesa inayoeleweka kwa sababu hapo kuna skills, time, energy vyote vitahitajika kukamilisha ramani yako.
Nimalize kwa kusema hivi njoo nikupe ramani tu ukajenge ili hiyo 40,000/= utumie kuchapisha kazi, maana hata bei ya frem tu la mnazi haitoshi. Na mpingo frem, mninga frem itakuwaje???, hello ujenzi gharama kubwa sana.