DRC watoto 15 waliuawa Ituri, UNICEF walaani

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limelaani vikali mauaji ya watoto 15 katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Taarifa ya UNICEF iliyotolewa jijini New York, Marekani hii leo inasema watoto hao waliouawa katika shambulio ni miongoni mwa watu 50 waliouawa huku pia watoto wengine zaidi ya 30 wakiwa wamejeruhiwa.

Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC Edouard Beigbeder amesema, "ukatili huu ni ushahidi tosha wa kiwango cha ghasia jimboni Ituri ambao unalenga watoto walio hatarini zaidi."

Shambulio hilo laelezwa ni tukio la hivi karibuni zaidi lililolenga kambi ya wakimbizi wa dani jimboni Ituri mashariki mwa DRC.

UNICEF inasisitiza kuwa watoto walioko kwenye mizozo wanapaswa kulindwa na si kulengwa
 
Hao weyewe ndio wanaoanzisha hiyo mizozo halafu wanataka watu waizuie,
Kwanza wao wangeacha kusababisha hiuo mizozo tungewaelewa
 
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limelaani vikali mauaji ya watoto 15 katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Taarifa ya UNICEF iliyotolewa jijini New York, Marekani hii leo inasema watoto hao waliouawa katika shambulio ni miongoni mwa watu 50 waliouawa huku pia watoto wengine zaidi ya 30 wakiwa wamejeruhiwa.

Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC Edouard Beigbeder amesema, "ukatili huu ni ushahidi tosha wa kiwango cha ghasia jimboni Ituri ambao unalenga watoto walio hatarini zaidi."

Shambulio hilo laelezwa ni tukio la hivi karibuni zaidi lililolenga kambi ya wakimbizi wa dani jimboni Ituri mashariki mwa DRC.

UNICEF inasisitiza kuwa watoto walioko kwenye mizozo wanapaswa kulindwa na si kulengwa
taarifa haijitoshelezi waliuwawa na nani na majambazi na codeco na ADF au na M23
 
Back
Top Bottom