DRC Updates: Kalemie, risasi zaanza kulindima

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,481
Reaction score
1,450
Baada ya kukamatwa kwa Uviru, M23 inaendelea na safari.

Siku ya jana, eneo lijulikanalo kama Mboko, lililopo umbali wa km 56bkutoka Uvira, liliangukia mikononi mwa kundi hilo la M23.
Inasemekana, kabla ya kuwaza kwenda Katanga, ambayo ndo kitovu cha uchumi w nchi, na ndo ilipo migodi ya raisi na familia yake, na watu wake wa karibu, wanataka kuhakikisha mipaka yote ya DRC wanayo wao.

Pichani, ni gereza la Kalemie, lililowashwa moto na wafungwa baada ya milio ya risasi kuanza, huku walinzi wakivua sale zao na kuanza kukimbia.
1765535362699.png

Taarifa zaidi zitawafikia kila hatua itakayokuwa ikipigwa.

Wakati huo, inasemekana ndege za kivita, asubuhi ya leo, zimetoka Burundi na kurusha makombola katika kambi ya Banyamulenge huko Minembwe.
 
Baada ya kukamatwa kwa Uviru, M23 inaendelea na safari.

Siku ya jana, eneo lijulikanalo kama Mboko, lililopo umbali wa km 56bkutoka Uvira, liliangukia mikononi mwa kundi hilo la M23.
Inasemekana, kabla ya kuwaza kwenda Katanga, ambayo ndo kitovu cha uchumi w nchi, na ndo ilipo migodi ya raisi na familia yake, na watu wake wa karibu, wanataka kuhakikisha mipaka yote ya DRC wanayo wao.

Taarifa zaidi zitawafikia kila hatua itakayokuwa ikipigwa.
Ule mkataba wa amani ulioasisiwa na Trump ni kanyaboya tu..
 
Kwaio destination yao ni Katanga?
Katanga ikishakamatwa, nchi haina ubavu tena. Kitovu cha uchumi wa nchi ile, ni Kivu zote mbili na Katanga. Mikoa mingine mchango ni mdogo sana. Na ukizingatia, target kubwa yao ni kuondoa utawala wa Tshisekedi.

Katanga,aliekuwa mgombea mwenza, na inasemekana alikuwa ndo mshindi wa urais, boss wa TP Mazembe, bwana Moise Katumbi, ni mzaliwa wa hapo. Hivyo, M23 ina nguvu kubwa ikifika hapo.
 
Yaani miaka zaidi ya mitano hajaunda jeshi la kuilinda DRC?
Kuna kosa kubwa walilofanya ndo matokeo yake na haiwezi kukaa ikaisha.
Alipokuwa anagombea, aliomba hawa M23, ambao kipindi hicho walikuwa CNDP, kuwa ndo wataunda Republican Guard. Watu wakachaguliwa, na batallion 3 zikawekwa standby.

Katika uchaguzi huo, Moise Katumbi, ndo alikuwa mshindi, ila kimpango akapokonywa. Rais alivoapishwa, akawageuka. Ndo hapo mambo oyote yalipoanzia.
 
Miaka mitano,!?..zogo la DRC ni la miaka mitano?..unakijua kisa cha lieutenant colonel mamadou!?.. DRC ipo kwenye deep shit,juzi amir wa Qatar alikua Rwanda
Nahisi mtoa comments amemaanisha baada ya M23 kufurushwa na Jeshi la DRC pamoja na vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2013, kundi la M23 lilirudi tena rasmi mnamo mwaka 2022.

Hapo ni miaka kama 9 hivi Sasa Kwa serikali ambayo ipo makini na suala la ulinzi na usalama hiyo miaka ilitosha kabisa kuunda Jeshi IMARA la kulinda mipaka yake.

Kama utakumbuka Hawa M23 baada yakupigwa walikimbilia Rwanda na Uganda walienda kujiorganize na kurudi Tena mwaka 2022 Hadi Sasa wamezidi kuwa tishio.
 
Hivi, jeshi likiwa na mwanajeshi wa miaka 90, na bado yupo kazini, kuna jeshi hapo au mgambo?
 
Nahisi mtoa comments amemaanisha baada ya M23 kufurushwa na Jeshi la DRC pamoja na vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2013, kundi la M23 lilirudi tena rasmi mnamo mwaka 2022.

Hapo ni miaka kama 9 hivi Sasa Kwa serikali ambayo ipo makini na suala la ulinzi na usalama hiyo miaka ilitosha kabisa kuunda Jeshi IMARA la kulinda mipaka yake.

Kama utakumbuka Hawa M23 baada yakupigwa walikimbilia Rwanda na Uganda walienda kujiorganize na kurudi Tena mwaka 2022 Hadi Sasa wamezidi kuwa tishio.
Mnaichukulia DRC kama tz, DRC ndani ya vyombo vya ulinzj na usalama kuna watu wa 'watu',nimetolea mfano colonel mamadou,baada ya kuongoza jeshi kuwashunda m23,aliuawa na wakubwa wake wa jeshi
 
Pamoja na madhaifu ya Jeshi la Congo ila Kigali haiwezi kukwepa lawama kwamba wako nyumba ya M23.

Mara kadhaa iliwahi kuripotiwa kwamba Jeshi la Rwanda limekuwa likipambana bega Kwa bega na M23 dhidi ya Jeshi la Congo.
 
Hao nao hata wakichukua nchi, wataanza ufisadi na waasi wengine wataibuka kuwapiga. Futile cycle. Hiyo nchi zinatakiwa kutoka nchi nyingi, tano, kumi au 20 hadi 26 kulingana na idadi ya majimbo yao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom