DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?

DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo wanatarajia kukubali Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama wake wa saba katika mojawapo ya matukio yenye maana kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii katika eneo la Maziwa Makuu.

DRC - ikiwa na watu takribani milioni 92, litakuwa ndiyo taifa lenye watu wengi zaidi miongoni mwa nchi wanachama na kutaifanya EAC sasa kuwa jumuiya yenye soko la takribani watu milioni 260. DRC ni kubwa kieneo na inapakana na takribani nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo - kwa maana ya nchi zote kuondoa Kenya. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini.

Hatua hiyo ya wakuu wa EAC kupitia mkutano wao utakaofanyika kwa njia ya mtandao leo, ni hitimisho la safari ya takribani miaka 10 - iliyoanza wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila na kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki lililoongozwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Peter Mathuki, kati ya Juni na Julai mwaka huu.

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameonyesha hamu kubwa ya taifa lake kujiunga na jumuiya hiyo na alitumia sehemu kubwa ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa taifa lake mwaka huu kueleza namna taifa lake lilivyokuwa tayari kuwa mwanachama mpya wa EAC.

Kwanini Tshisekedi na Wakongomani wana hamu ya kujiunga muungano huu?

Jiografia
Kijiografia, hakuna nchi nyingine yenye sifa ya kuwa mwanachama wa EAC kuizidi DRC. Mojawapo ya masharti ya mwanzo ya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo yalikuwa kwamba nchi ni lazima iwe inapakana na mojawapo ya nchi wanachama lakini taifa hili mashuhuri duniani linapakana na nchi zote wanachama.

Kuondoa ujirani mwema huo, Wakongomani ni kama vile walikuwa wanachama wa EAC hata kabla ya nchi yao kuwa mwanachama rasmi wa jumuiya. Kwa mfano, kwa muda mrefu, DRC ilikuwa inaongoza kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake kuliko nchi wanachama, muziki wenye asili ya taifa hilo ukiwa mashuhuri katika nchi zote za Afrika Mashariki na watu wake mbalimbali wakiweka makazi yao ya kudumu katika nchi tofauti inazopakana nazo.

Je, DRC inaweza kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika MMashariki

Miongoni mwa nchi wanachama wa EAC, pengine hakuna taifa ambalo watu wake wametapakaa katika nchi zote za jumuiya hiyo - Wakongomani wakijulikana kwa tabia yao ya kutoogopa kutafuta riziki popote nje ya taifa lao - tofauti na wananchi wa baadhi ya nchi wanachama wengine ambao si watu wa kuhangaika duniani kutafuta maisha.

Kwa sababu hiyo, kijiografia na kiutamaduni, DRC ilikuwa mwanachama wa EAC miaka mingi kabla hata haijapata fursa hii ya kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa sita.

Wakati jumuiya ikionekana kuzidi kutanuka, ni vigumu kuona taifa lingine litakalokuwa na "wenyeji wengi walio wageni "kuzidi ujio huu wa taifa lililokuwa likijulikana kama Zaire wakati wa utawala wa Mobutu Sesesseko.

Uchumi
Kwa sasa, Pato la Nchi Wanachama wa EAC linafikia kiasi cha dola bilioni 193 na ujio wa DRC utaongeza pato hilo kwa dola bilioni 50 zaidi kufikia dola 240. Hiki ni kiwango kikubwa kuongezwa na nchi moja katika eneo la dunia linalofahamika kwa umasikini mkubwa.

Lakini siri kubwa iko katika soko. Kwa sababu ya matatizo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, DRC inaonekana kama nchi ambayo bado fursa zake hazijatumiwa ipasavyo na wananchi wake lakini pia na nchi Jirani.

Hata kabla ya kuiruhusu DRC kuingia EAC, viongozi wa juu wa nchi wanachama kama vile Uhuru Kenyatta, Paul Kagame na Yoweri Museveni wameonekana kujisogeza karibu na Tshisekedi.

Kuna mpango wa Afrika wa kuunganisha upande wa Mashariki na Magharibi - kutoka Bahari ya Hindi hadi Atlantic na DRC ni mojawapo ya nguzo muhimu kwenye jambo hilo kubwa.

Kuna mpango wa kujenga barabara kupitia mradi wa TAH8 unaounganisha bandari ya Mombasa, Kenya kwenda katika jiji la Younde, Cameroon na kisha Atlantic. Hizi ni mojawapo ya miradi mikubwa ya miundombinu barani Afrika inayotazamwa kwa jicho la kipekee na Umoja wa Afrika.

Rais Museveni amewahi kuzungumza huko nyuma kwamba tatizo kubwa la Afrika ni ukosefu wa masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na ujio wa taifa lenye watu milioni 92 unamaanisha soko kubwa kwa bidhaa za nchi wanachama wa EAC.

Usalama
Mara zote ukubwa wa DRC umekuwa na changamoto za kiusalama kwa nchi wanachama. Rwanda na Uganda zimekuwa zikisumbuliwa na makundi ya waasi yanayojificha katika misitu minene ya DRC. Lakini pia nchi hizo mbili zimewahi kupigana zenyewe ndani ya taifa hilo kwa sababu ya kuwania kuwa na ushawishi kwa viongozi wa DRC.

Ni matarajio ya viongozi wa EAC kwamba kuwa na DRC ndani yao kutasaidia kujenga mipango itakayowezesha urahisi wa kudhibiti vikundi vya waasi na ugaidi lakini pia kufanya biashara kwa Pamoja badala ya kudhulumiana.

Kuna dhana kutoka katika baadhi ya jamii ya Wakongomani kwamba Rwanda na Uganda wamekuwa wakitumia utajiri wa taifa lao kwa faida yao kwa kutumia visingizio vya kiusalama.

Amani ya kudumu katika eneo la maziwa makuu itasababisha viongozi wa nchi husika sasa kutumia nguvu zaidi katika kujenga uchumi na ushirikiano badala ya kupanga namna ya kufanya uvamizi au kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi au uasi kupora mali za DRC.

Ndoto ya Waasisi
Hatua ya DRC kuingia EAC inachukuliwa pia kama kutimia kwa ndoto za waasisi wa siasa za Umajumui wa Afrika walioamini kwamba namna pekee kwa Afrika kusonga mbele ni kwa kuwa na umoja wa kisiasa na kiuchumi miongoni mwao.

Wakati Tshisekedi akitaka DRC iingie EAC, alikuwa anatimiza ndoto za Patrice Lumumba, Julius Nyerere, Milton Obote na Jomo Kenyatta. Ni matarajio ya wachambuzi wa masuala ya ushirikiano kwamba muda si mrefu nchi kama Somalia, Congo Brazaville na Ethiopia nazo zinaweza kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.

Kwa kufanya hivyo, nchi wanachama wa EAC wanaweza kuwa na uwezekano wa kuwa na kura moja kwenye masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa eneo la Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla - bila kuzingatia tofauti za lugha wanazozungumza.

Ni jambo zuri kwamba Museveni ambaye ndiye kiongozi mwenye ari zaidi ya mtangamano wa Afrika yuko madarakani bado na jambo hili linaendana na ndoto zake za muda mrefu za kuunganisha Afrika kwa mafungu.

Changamoto
Takribani miaka 10 iliyopita, Sudan Kusini iliingia EAC kwa mbwembwe na furaha kubwa. Wengi walitaraji makubwa kutoka katika taifa hilo. Hata hivyo, kuwepo kwake kwenye jumuiya hakuonekani kupunguza chochote kwenye migogoro na sintofahamu miongoni mwa vinara wakuu wa taifa hilo.

Kimsingi, hakuna mijadala inayofanyika au jitihada za makusudi zinazofanywa na EAC kuhakikisha nchi hiyo mwanachama inakuwa na amani ya kudumu.

Kwa maneno mengine, kuwa kwake mwanachama wa jumuiya hakujaondoa tofauti zake za ndani na hakujaongeza uwezekano wa nchi wanachama kusaidia kuondoa matatizo yake.

Hili ndilo swali ambalo wachambuzi wanajiuliza sasa kwamba kama DRC itakuwa tofauti na italeta kinachotarajiwa na wengi baada ya kujiunga kwake na EAC. Kama ilivyokuwa kwa akina Salva Kiir na Riek Machar huko nyuma, Tshisekedi anaonekana kuwa na nia na ari kubwa - tatizo ni kwamba haijulikana EAC iko tayari kiasi kuisaidia DRC kusimama vizuri.

Changamoto nyingine kubwa kuhusu DRC inahusu dhamiri za ndani za baadhi ya viongozi wa EAC kuhusu kuwa na taifa hilo jipya kama mwanachama. Kuna nchi zinaitazama Kongo kama taifa la kuibiwa - shamba la bibi, na haijulikani kama tabia hiyo itaondoka au itamea zaidi kupitia muungano huu.

Tayari baadhi ya viongozi wa nchi za EAC wamefanya ziara kwa Tshisekedi kufanya dili kwa ajili ya nchi zao hata kama ya tukio la leo. Ipo hatari ya uhakika kwamba huenda maslahi ya baadhi ya nchi yakagongana huko mbele ya safari na hatimaye nchi zikajikuta zinarudi palepale zilipokuwa awali.

Lakini, leo ni siku ya kusherehekea kuikaribisha DRC ndani ya EAC.

DRC, Tanzania, Uganda, Kenya, South Sudan, ni nchi muhimu sana duniani. DRC Ina kila kitu, mafuta, mbao, eneo, watu.

Unajua bandari tu ikifanya kazi kwa ufanisi itaikomboa Tanzania kusaidia sana DRC. Vitu vingi kwenye simu, mobile phone, mawasiliano vinatoka hapoo DRC. Mafuta, Gesi, madini ya lia namna yanapatikana hapa.
 
Inapaswa kuwa tunafuata au tunatekeleza?

Anyway Tanzania tuna uchumi huria, uchumi wa Tanzania upo huria lakini wenye ushawishi wa ujamaa ndani yake.

Kwa lugha ya kiingereza Tanzania inajulikana kama moja ya Countries with constitutional references to socialism
Haya mambo ya raisi hakosei sio bahati mbaya ni akili za ujamaa wa mwalimu huu,
Ukimuona Polepole anasema ujamaa ni iman ndio hiyo.
Jaribu kupitia ujamaa utaona Tanzania namna gani tunavyouishi kila siku.
 
Uchumi huria kwenye raia na viongozi wenye mawazo na akili za kijamaa.
Unaamini tunapaswa kuendelea na huu mfumo(kwa maana ya kuwa mfumo huu umefaulu).
Maana ya ujamaa wa Nyerere ulikua na lengo la kumuokoa mwananchi wa chini kabisa aliekua hana nguvu ya partnership na multi billion companies kutoka ulaya inayotaka kuwekeza Tanzania

Unafikiri kingetokea nini kama makampuni makubwa kutoka nje yangehodhi mashamba makubwa, migodi, mashirika makubwa ya Bima, Banks, Cooperates na Institutions kwa binafsi yao bila serikali kuwa na chochote cha kufanya dhidi ya wananchi wake?

Kama ulishafika South Africa ungekua na uwanda mpana wa jinsi ubepari unavyofanya kazi, hapa East Africa hakuna taifa lolote lenye ubepari angalau kwa 20%
 
Haya mambo ya raisi hakosei sio bahati mbaya ni akili za ujamaa wa mwalimu huu,
Ukimuona Polepole anasema ujamaa ni iman ndio hiyo.
Jaribu kupitia ujamaa utaona Tanzania namna gani tunavyouishi kila siku.
Tanzania sio Taifa pekee lilokua na ujamaa duniani, tena mataifa yaliokua na sera za kijamaa yapo vizuri kiuchumi kuliko mataifa ya Africa yaliyoanza na sera za kibepari toka mwanzo

80% Yana uchumi mkubwa kuliko mataifa yalioanza na ubepari

Screenshot_20211223-170208_1.jpg
 
Maana ya ujamaa wa Nyerere ulikua na lengo la kumuokoa mwananchi wa chini kabisa aliekua hana nguvu ya partnership na multi billion companies kutoka ulaya inayotaka kuwekeza Tanzania

Unafikiri kingetokea nini kama makampuni makubwa kutoka nje yangehodhi mashamba makubwa, migodi, mashirika makubwa ya Bima, Banks, Cooperates na Institutions kwa binafsi yao bila serikali kuwa na chochote cha kufanya dhidi ya wananchi wake?

Kama ulishafika South Africa ungekua na uwanda mpana wa jinsi ubepari unavyofanya kazi, hapa East Africa hakuna taifa lolote lenye ubepari angalau kwa 20%
Sina tatizo na ujamaa wa Mwalimu miaka hiyo na hakuna
nchi yenye ubepari 100% shida ni kwa watu waliofuata kushindwa ku-twist na karne ya leo
Naamini isingekuwa vita ya kagera na kuanguka USSR ujamaa ungetupeleka mbali japo sio kwa karne hii.
Binafsi ni mwanafunzi mzuri wa Karl Max lakini karne ya leo inahitaji akili kubwa kujua wapi uapply ujamaa
na wapi uapply ubepari kitu ambacho viongoozi wamefeli.
 
DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo wanatarajia kukubali Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama wake wa saba katika mojawapo ya matukio yenye maana kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii katika eneo la Maziwa Makuu.

DRC - ikiwa na watu takribani milioni 92, litakuwa ndiyo taifa lenye watu wengi zaidi miongoni mwa nchi wanachama na kutaifanya EAC sasa kuwa jumuiya yenye soko la takribani watu milioni 260. DRC ni kubwa kieneo na inapakana na takribani nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo - kwa maana ya nchi zote kuondoa Kenya. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini.

Hatua hiyo ya wakuu wa EAC kupitia mkutano wao utakaofanyika kwa njia ya mtandao leo, ni hitimisho la safari ya takribani miaka 10 - iliyoanza wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila na kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki lililoongozwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Peter Mathuki, kati ya Juni na Julai mwaka huu.

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameonyesha hamu kubwa ya taifa lake kujiunga na jumuiya hiyo na alitumia sehemu kubwa ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa taifa lake mwaka huu kueleza namna taifa lake lilivyokuwa tayari kuwa mwanachama mpya wa EAC.

Kwanini Tshisekedi na Wakongomani wana hamu ya kujiunga muungano huu?

Jiografia
Kijiografia, hakuna nchi nyingine yenye sifa ya kuwa mwanachama wa EAC kuizidi DRC. Mojawapo ya masharti ya mwanzo ya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo yalikuwa kwamba nchi ni lazima iwe inapakana na mojawapo ya nchi wanachama lakini taifa hili mashuhuri duniani linapakana na nchi zote wanachama.

Kuondoa ujirani mwema huo, Wakongomani ni kama vile walikuwa wanachama wa EAC hata kabla ya nchi yao kuwa mwanachama rasmi wa jumuiya. Kwa mfano, kwa muda mrefu, DRC ilikuwa inaongoza kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake kuliko nchi wanachama, muziki wenye asili ya taifa hilo ukiwa mashuhuri katika nchi zote za Afrika Mashariki na watu wake mbalimbali wakiweka makazi yao ya kudumu katika nchi tofauti inazopakana nazo.

Je, DRC inaweza kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika MMashariki

Miongoni mwa nchi wanachama wa EAC, pengine hakuna taifa ambalo watu wake wametapakaa katika nchi zote za jumuiya hiyo - Wakongomani wakijulikana kwa tabia yao ya kutoogopa kutafuta riziki popote nje ya taifa lao - tofauti na wananchi wa baadhi ya nchi wanachama wengine ambao si watu wa kuhangaika duniani kutafuta maisha.

Kwa sababu hiyo, kijiografia na kiutamaduni, DRC ilikuwa mwanachama wa EAC miaka mingi kabla hata haijapata fursa hii ya kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa sita.

Wakati jumuiya ikionekana kuzidi kutanuka, ni vigumu kuona taifa lingine litakalokuwa na "wenyeji wengi walio wageni "kuzidi ujio huu wa taifa lililokuwa likijulikana kama Zaire wakati wa utawala wa Mobutu Sesesseko.

Uchumi
Kwa sasa, Pato la Nchi Wanachama wa EAC linafikia kiasi cha dola bilioni 193 na ujio wa DRC utaongeza pato hilo kwa dola bilioni 50 zaidi kufikia dola 240. Hiki ni kiwango kikubwa kuongezwa na nchi moja katika eneo la dunia linalofahamika kwa umasikini mkubwa.

Lakini siri kubwa iko katika soko. Kwa sababu ya matatizo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, DRC inaonekana kama nchi ambayo bado fursa zake hazijatumiwa ipasavyo na wananchi wake lakini pia na nchi Jirani.

Hata kabla ya kuiruhusu DRC kuingia EAC, viongozi wa juu wa nchi wanachama kama vile Uhuru Kenyatta, Paul Kagame na Yoweri Museveni wameonekana kujisogeza karibu na Tshisekedi.

Kuna mpango wa Afrika wa kuunganisha upande wa Mashariki na Magharibi - kutoka Bahari ya Hindi hadi Atlantic na DRC ni mojawapo ya nguzo muhimu kwenye jambo hilo kubwa.

Kuna mpango wa kujenga barabara kupitia mradi wa TAH8 unaounganisha bandari ya Mombasa, Kenya kwenda katika jiji la Younde, Cameroon na kisha Atlantic. Hizi ni mojawapo ya miradi mikubwa ya miundombinu barani Afrika inayotazamwa kwa jicho la kipekee na Umoja wa Afrika.

Rais Museveni amewahi kuzungumza huko nyuma kwamba tatizo kubwa la Afrika ni ukosefu wa masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na ujio wa taifa lenye watu milioni 92 unamaanisha soko kubwa kwa bidhaa za nchi wanachama wa EAC.

Usalama
Mara zote ukubwa wa DRC umekuwa na changamoto za kiusalama kwa nchi wanachama. Rwanda na Uganda zimekuwa zikisumbuliwa na makundi ya waasi yanayojificha katika misitu minene ya DRC. Lakini pia nchi hizo mbili zimewahi kupigana zenyewe ndani ya taifa hilo kwa sababu ya kuwania kuwa na ushawishi kwa viongozi wa DRC.

Ni matarajio ya viongozi wa EAC kwamba kuwa na DRC ndani yao kutasaidia kujenga mipango itakayowezesha urahisi wa kudhibiti vikundi vya waasi na ugaidi lakini pia kufanya biashara kwa Pamoja badala ya kudhulumiana.

Kuna dhana kutoka katika baadhi ya jamii ya Wakongomani kwamba Rwanda na Uganda wamekuwa wakitumia utajiri wa taifa lao kwa faida yao kwa kutumia visingizio vya kiusalama.

Amani ya kudumu katika eneo la maziwa makuu itasababisha viongozi wa nchi husika sasa kutumia nguvu zaidi katika kujenga uchumi na ushirikiano badala ya kupanga namna ya kufanya uvamizi au kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi au uasi kupora mali za DRC.

Ndoto ya Waasisi
Hatua ya DRC kuingia EAC inachukuliwa pia kama kutimia kwa ndoto za waasisi wa siasa za Umajumui wa Afrika walioamini kwamba namna pekee kwa Afrika kusonga mbele ni kwa kuwa na umoja wa kisiasa na kiuchumi miongoni mwao.

Wakati Tshisekedi akitaka DRC iingie EAC, alikuwa anatimiza ndoto za Patrice Lumumba, Julius Nyerere, Milton Obote na Jomo Kenyatta. Ni matarajio ya wachambuzi wa masuala ya ushirikiano kwamba muda si mrefu nchi kama Somalia, Congo Brazaville na Ethiopia nazo zinaweza kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.

Kwa kufanya hivyo, nchi wanachama wa EAC wanaweza kuwa na uwezekano wa kuwa na kura moja kwenye masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa eneo la Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla - bila kuzingatia tofauti za lugha wanazozungumza.

Ni jambo zuri kwamba Museveni ambaye ndiye kiongozi mwenye ari zaidi ya mtangamano wa Afrika yuko madarakani bado na jambo hili linaendana na ndoto zake za muda mrefu za kuunganisha Afrika kwa mafungu.

Changamoto
Takribani miaka 10 iliyopita, Sudan Kusini iliingia EAC kwa mbwembwe na furaha kubwa. Wengi walitaraji makubwa kutoka katika taifa hilo. Hata hivyo, kuwepo kwake kwenye jumuiya hakuonekani kupunguza chochote kwenye migogoro na sintofahamu miongoni mwa vinara wakuu wa taifa hilo.

Kimsingi, hakuna mijadala inayofanyika au jitihada za makusudi zinazofanywa na EAC kuhakikisha nchi hiyo mwanachama inakuwa na amani ya kudumu.

Kwa maneno mengine, kuwa kwake mwanachama wa jumuiya hakujaondoa tofauti zake za ndani na hakujaongeza uwezekano wa nchi wanachama kusaidia kuondoa matatizo yake.

Hili ndilo swali ambalo wachambuzi wanajiuliza sasa kwamba kama DRC itakuwa tofauti na italeta kinachotarajiwa na wengi baada ya kujiunga kwake na EAC. Kama ilivyokuwa kwa akina Salva Kiir na Riek Machar huko nyuma, Tshisekedi anaonekana kuwa na nia na ari kubwa - tatizo ni kwamba haijulikana EAC iko tayari kiasi kuisaidia DRC kusimama vizuri.

Changamoto nyingine kubwa kuhusu DRC inahusu dhamiri za ndani za baadhi ya viongozi wa EAC kuhusu kuwa na taifa hilo jipya kama mwanachama. Kuna nchi zinaitazama Kongo kama taifa la kuibiwa - shamba la bibi, na haijulikani kama tabia hiyo itaondoka au itamea zaidi kupitia muungano huu.

Tayari baadhi ya viongozi wa nchi za EAC wamefanya ziara kwa Tshisekedi kufanya dili kwa ajili ya nchi zao hata kama ya tukio la leo. Ipo hatari ya uhakika kwamba huenda maslahi ya baadhi ya nchi yakagongana huko mbele ya safari na hatimaye nchi zikajikuta zinarudi palepale zilipokuwa awali.

Lakini, leo ni siku ya kusherehekea kuikaribisha DRC ndani ya EAC.
Umesahau kuzungumzia lugha kwasababu eastern Congo wanaongea Kiswahili
 
Sina tatizo na ujamaa wa Mwalimu miaka hiyo na hakuna
nchi yenye ubepari 100% shida ni kwa watu waliofuata kushindwa ku-twist na karne ya leo
Naamini isingekuwa vita ya kagera na kuangua USSR ujamaa ungetupeleka mbali japo sio kwa karne hii.
Binafsi ni mwanafunzi mzuri wa Karli Max lakini karne ya leo inahitaji akili kubwa kujua wapi uapply ujamaa
na wapi uapply ubepari kitu ambacho viongoozi wamefeli.
Ni kweli kabisa, waliomtangulia Nyerere walikuja na sera zao nyingi mbovu, lakini nimeguswa kujua kiundani ile kauli yako kwamba ujamaa ndio uchawi wa Tanzania na Nyerere angekua Hai angetuomba msamaha juu ya Ujamaa, hoja ambazo Kwangu zina ulakini kidogo na huenda wengi wanawaza hivi bila utafiti.
 
Tanzania sio Taifa pekee lilokua na ujamaa duniani, tena mataifa yaliokua na sera za kijamaa yapo vizuri kiuchumi kuliko mataifa ya Africa yaliyoanza na sera za kibepari toka mwanzo

80% Yana uchumi mkubwa kuliko mataifa yalioanza na ubepari

View attachment 2054789
Sina tatizo na ujamaa kabisa mkuu ila kwa karne hii inahitaji watu wenye akili kujua wapi
wa apply ujamaa na wapi wa apply ubepari.
Nnaupenda ujamaa lakini kwa sasa ubepari is the inevitable.
Tunahitaji watu wenye akili watakao weza ku-twist ndani ya ubepari inapotakiwa.
Sisemi watu wote wanaofuata mlengo wa ubepari wamefanikiwa ubepari bado umefeli latin america
baadhi ya maeneo ya asia pamoja na Africa.
Tatizo la Tanzania tunataka tu-interact na mabepari lakini hatuujui ubepari lazima
tupigwe.
Ndio maana nasema tujifunze ku-twisti kulingana na mahitaji.
 
Kielelezo bora cha ubepari Africa ni South Africa na Nigeria, hizi ni nchi ambazo kwa kiasi chake zipo kwenye middle line of capitalism kwa Nigeria na South Africa almost upper middle line lakini je maisha ya wengi wa wakazi wa kawaida wa hayo mataifa wanaendana na status ya uchumi wao?
 
Point yangu ni kwamba tunapoamua kufungamana na mabepari tusiende na mawazo ya kijamaa
twende kama mabepari vinginevyo tutatoa rasillimali zetu zote na bado tutakuwa maskini.
Tujue ubepari tunautummia wapi na ujamaa tunautumia wapi.
 
Sina tatizo na ujamaa kabisa mkuu ila kwa karne hii inahitaji watu wenye akili kujua wapi
wa apply ujamaa na wapi wa apply ubepari.
Nnaupenda ujamaa lakini kwa sasa ubepari is the inevitable.
Tunahitaji watu wenye akili watakao weza ku-twist ndani ya ubepari inapotakiwa.
Sisemi watu wote wanaofuata mlengo wa ubepari wamefanikiwa ubepari bado umefeli latin america
baadhi ya maeneo ya asia pamoja na Africa.
Tatizo la Tanzania tunataka tu-interact na mabepari lakini hatuujui ubepari lazima
tupigwe.
Ndio maana nasema tujifunze ku-twisti kulingana na mahitaji.
Ni kweli, study case ni makampuni mkubwa ya madini Tanzania yalioletwa na Mkapa na Kikwete (Nyerere aliyagomea mpaka Watanzania wajiweze iwe ni kwa partnership au wao wenyewe)

Je unafikiri bila mentality ya Nyerere kuhusu hizi multi-billion companies zinazochota rasilimali zetu muhimu sana ipo namna mtanzania wa kawaida anaweza kuhusishwa moja kwa moja na hii cake ya taifa tukiondoa kodi zitokanazo na uwekezaji na mirahaba, levies, ajira, social responsibility?

Ni haramu kwa serikali yenyewe kupata share kwenye haya Makampuni (ujamaa) since hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuingia ubia nao?
 
Ndio maana nikasema hawa waliingia kwenye ubepari bila kuujua ndio maana tukapigwa
bepari hana ndugu.
Hata sasa viongozi wana practice ubepari lakini hawaujui lazima tupigwe nadhani
Nyerere alikuwa anaujua vizuri ubepari hawa waliomfuata hawakujua ujamaa wala ubepari.
 
Point yangu ni kwamba tunapoamua kufungamana na mabepari tusiende na mawazo ya kijamaa
twende kama mabepari vinginevyo tutatoa rasillimali zetu zote na bado tutakuwa maskini.
Tujue ubepari tunautummia wapi na ujamaa tunautumia wapi.
Ila ujue ubepari ni watu binafsi wa nchi husika wanashiriki kuhodhi njia kuu za kiuchumi za Taifa (sio serikali 100% / serikali partially)

Kwa Tanzania yupo mtanzania yupi mwenye uwezo wa kuchimba gas au kuingia partnership na mgeni angalau ya 40% umiliki wa first class mining company?

Huoni ni muhimu serikali kuingia partnership (ujamaa) badala ya kuiachia company ya kigeni ichote rasilimali yote kwa kigezo kwamba sisi sio wajamaa?
 
Ila ujue ubepari ni watu binafsi wa nchi husika wanashiriki kuhodhi njia kuu za kiuchumi za Taifa

Kwa Tanzania yupo mtanzania yupi mwenye uwezo wa kuchimba gas au kuingia partnership na mgeni angalau ya 40% umiliki wa first class mining company?

Huoni ni muhimu serikali kuingia partnership (ujamaa) badala ya kuiachia company ya kigeni ichote rasilimali yote kwa kigezo kwamba sisi sio wajamaa?
Uko sahihi...
Ndio maana nasema viongozi waujue ubepari wajue namna ya kuishi nao.
Botswana imefanikiwa sana kwenye almasi sijui waliwezaje?
 
Botswana ni nchi ya watu million 2.3 tu ni kama Zanzibar lakini ina utajiri mkubwa wa diamond japo kwa asilimia kubwa utajiri huo unamilikiwa na wazungu, kutokana na uchache wao na tayari lilikua ni settlers colony ilikua tayari imeshaendelezwa toka siku nyingi

Katika Africa ni Nyerere/Tanzania pekee ilijitahidi kuja na African modern mode of production/economy, kwa kuzingatia kwamba modes zote za economy whether capitalism or socialism are all imported kutoka kwa mataifa ya kigeni, huwa nawashangaa sana wale wanaompinga Nyerere.
 
Pipe dreams.

You will link msa to Atlantic kupitia wapi? Hadi mfikie Congo mnajua mtapita wapi?

FYI, tunafika Atlantic soon via congo-zambia-Namibia. Railway line already in place from lobito port to Congo. We are finalizing to link railway to karema port then we will reach Congo.

While you are dreaming about it, we (TZ) are already at it. Kunyaland still have more issues to catch up... TZ ndio inatemgeneza mazingira ya ukanda huu.. Very calculated moves.. Congo tumemleta sisi, same to Burundi and Rwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
good for you 👍🏾
 
Welcome kongo ... kilichobaki ni kumake sure kongo inakua salama
Actually Congo is a massive addition to the east Africa community...what we need to show them from now moving forward is that this is the best decision they've ever made by.
1.Helping the stabilize as a country.
2.Build an SGR railway and a road from Kenya,Tanzania to Congo...
3.Help them stabilize their mining sector so that their deep wealth benefits Congo and East Africa.
I think east Africa formation is now done now we built and super powerful country that will take on the world.
 
Back
Top Bottom