IKITOKEA MMOJA AKAFUNGWA
Mechi kati ya Dogo Sisco na Cr 7 kama itachezwa (ingawa ninamashaka) na ikatokea mmojawapo akapoteza basi inaweza kuwa na madhara yafuatayo.
1.
Tuanze na Sisco
Sisco akifungwa
- Ronaldo atapata sababu lukuki za kusema yeye ndio kiboko ya Watu wa Uhuru hata kama hatarudiana na Nduli wala kucheza na Mzee Noel.
- Mechi yoyote ya Cr 7 dhidi ya Wenye Uhuru itakuwa na thamani kubwa sana
- Mengi aliyoyafanya Dogo Sisco yatapungua uzito na umuhimu kwani italazimishwa ionekane alokuwa anapambana nao ni wachezaji dhaifu.
- Inaweza kuwa ndio mechi ya mwisho Sisco kukutana na Ronaldo. Namna pekee ya kujifariji itakuwa ni kwa Sisco kusema aliwahi shinda tano na itaonekana kama ni maneno ya mchapikaji tu
- Wadai Uhuru wataingia kucheza na Cr 7 wakihisi tayari wamefungwa endapo kama mmojawapo atajiloga kukubali mechi na Cr 7.
- Akatae akubali, wakatae wakubali; japo kipigo cha gol 1 alichopata Sisco kwa Cr 7 ni cha kawaida ukilinganisha na golu 5 alizoshinda yeye, ila ni ukweli kwamba Sisco anatamani sana kufuta lile golu. Akichapika tena basi atazeeka na kovu moyoni.
NIMESEMA WAKATAE WAKUBALI, huo ndio ukweli.
- Team watu huru watapambana sana kuaminisha watu kwamba Sisco kashinda mechi nyingi lakini wahuni watawaona kama Madomokaya tu kumbe sio

2.
Tuje kwa Ronaldo
Kama Ronaldo atafungwa
- Itaonekana ile sare ya michezo 24 na mkulima ilikuwa ya mchongo; hapa mtegemee Dulla Mabau kutamba kwelikweli kwamba alisema...

- Itakuwa ndio mechi ya mwisho kwa Cr 7 kucheza na Sisco.
- Inaweza kuwa ndio mechi ya mwisho yenye msisimko kwa Cr 7 kwani italazimika kuthibitisha zama zake ni Zama za Kale za Mawe kwa sasa


.
- Asilimia kubwa ya kitakachokumbukwa ni zile goli 5 na kichapo kipya na mengine yote yatasemekana yalikuwaga ni ujanja ujanja tu

- Sisco atatajwa pasi na shaka kwamba ni mchezaji bora aliyewahi kuwa kwenye kiwango Bora kuliko kiumbe yeyote aliyewahi kucheza mabau
- Sisco atatajwa kama binadam pekee aliyefanya makubwa kuliko yeyote aliyewahi kuzaliwa tena katika umri mdogo

- Noel Namaloe atapata tege la kutokuja kucheza na Cr 7 kabisaa


. Kila akipangiwa nae atasema kama ulimshindwa dogo utaniweza mie Bingwa wa dunia

Wachezaji wanapojiandaa kucheza mchezo huu basi wayategemee hayo


na mengine endapo kama mmojawapo atachezea kichapo.
Ikibidi, hii mechi iwekewe mazingira Bora kwenye kuiratibu.
1. Wachezaji na wasimamizi wasigusane na wachezaji
2. Mazungumzo au maneno ya mashabiki kwa wachezaji yadhibitiwe na atakayejaribu kutaka kuvuruga mchezo adhibitiwe mala tu atakapoonyesha dalili; wakiwepo wale wanaopenda kuonyesha mazingira ya ushirikina.
3. Tahadhari zote za muhimu zichukuliwe ili mchezo uanze kwa amani na umalizike salama.