Dr. Wilbrod Slaa kesho kuanza rasmi vikao vya chama

Dr. Wilbrod Slaa kesho kuanza rasmi vikao vya chama

Status
Not open for further replies.
Ile "kesho" ya "jana" ndo leo. Vipi Dr. Slaa alikuwepo kwenye kikao cha kamati kuu? Swali kwa G sam.
 
Hivi mbona jamii forum tunaifanya kama kirasa ya magazeti ya udaku? hii forum ilinishawishi sana kijiunga nayo sababu ya ubora na uhakika wa habari zenye uhakika.na kama mtu hana uhakika na taarifa basi anasema kama ni tetesi. sasa katika mambo mhimu kama haya mtu anaandika taarifa bila hata ya source ya habari. inasikitisha sana.kuna kila linalosemwa mpaka inatokea mkanganyiko na mpaka wengine kushushuliwa na wahusika
ushauri wangu tuheshimu jamvi letu kwa kutoa taarifa sahii na zenye.uhakika kwa wasomaji.
 
Mkuu G Sam kesho ya tarehe 02/08 ni tarehe 03/08 ambayo ndiyo leo na imepita. Vipi tena??
 
Last edited by a moderator:
Wadau watanzania wengi walikuwa tayari kuondokana na CCM Alkn vyama vya upinzania naona vimekosa muelekeo na busara kwa hali hii ccm itutawatesa sanaa !
 
Mkuu, G Sam mkutano ndo huuuooo...vipi DR wapi.

Ila nashauri JF Members muwe na uhakika wa hbari kabla ya kukimbilia kupost.
 
wewe Garasa njoo ujibu huku novadu sijui ndio nini ishaisha au umeamua kusali wewe tena siku tisa ..kenge wa ufipa wee
 
Naam kiongozi wangu niliyependezwa nawe pale Jangwani 2010, nikapendezwa nawe tena mara kwa mara ulipokuja kutuhutubia wana CHASO-UDSM mwaka 2011 tukiwa na kina Juliana Shonza. Hakika ulinivutia sana kuipenda siasa yako na uliyoyasimamia!

Nimekuja kwenye 'kijibaraza' eneo la makazi yako nikiamini kabisa leo lazima utoke! Ni lazima kwasababu muda uliojitengea kwa maombi maalum umeisha baba! Sasa ni zamu yetu kusikia kutoka kwako. Naamini kabisa leo utatutendea haki tulio na kiu ya kuungana na wewe kwenye ile safari waliyokwishaanza wenzetu kuelezea kuitoa CCM madarakani.

Kiongozi wangu, kwa hakika umebaki wewe tu! Maalim Seif aliyekuwa kikwazo kikubwa jana kapanda Jahazi hadi mlimani city kuja kukamilisha. Mwingine kajivua mpaka uwaziri ili mambo ya kamilike! Baba Slaa, UKAWA tulipokuwa tukiiona kama kukumbwa na giza nene mbeleni jana imeng'ara peupee!

Naambiwa kuwa Kinana aliishia kukatiza hotuba yake pale Lumumba aliyokuwa akiisoma kwa neno 'UKIWA' badala ya 'UKAWA' pale alipotumiwa 'meseji' kuwa maadui wameshinda kwa kishindo pale mlimani city!

Kinana akatweta kwa jasho akaishia kumkaribisha mwenyekiti! Masikini ya Mungu kumbe naye muda uleule ndo aliupata huo ujumbe alopata Kinana! Mwenyekiti akaishia kutoa vitisho kwa jazba na jeuri ya dola kuwa lazima washinde kwa kutumia kila namna!

Kiongozi wangu, hebu amua ku-sacrifice kama alivyosema kamanda Mbowe tuimalize shughuli nyepesi mapema na asubuhi! Mimi nimesha amua ila nakusubiri tuongozane maana najua kuwa Mungu wetu aliyetuongoza ni mmoja! Mimi kaniambia nenda haraka G Sam.

Kwa hakika tukiendelea kusubiri nachelea watu wataanza kukusahau kiongozi wangu mpendwa! Si unawajua Watanganyika? Baba twende tukauchukue ushindi mapema! Kwa hakika yule mtu anakubalika! akiingia sehemu panatikisika! Ila wewe kwake ni kiungo muhimu sana! Naomba twende maana kazi imeisha!
 
Kama ni kukubalika mbona hata shetani anakubalika na ana wafuasi wengi hapa duniani zaidi ya Mwenyezi Mungu! Dr ana kura yake moja tu, kwanini anawasumbua hivi!
 
Tunamwomba Mungu amjalie DK SLAA nguvu na wepesi wa kuungana tena na Chadema katika safari hii ya mabadiliko.
 
Mkuu it is really touching! Ninaona hata hivyo juhudi za kumleta Dr katika campaign zinaendelea. Hapa anatakiwa Mhs Mbowe asacrifice naye aende akapige magoti ili Dr arudi. Kupiga magoti hakutapunguza madaraka yake. Ila kutusaidia ktk kuleta ushindi.
 
...Kwa hakika tukiendelea kusubiri nachelea watu wataanza kukusahau kiongozi wangu mpendwa! Si unawajua Watanganyika? .......
Hapo umenena kweli. Nadhani katika hili Dr Slaa hajashauriwa vizuri. Siasa ni dynamic na kama huwezi kwenda na mawimbi lazima utazama.
 
Vipi Mkuu, maji shingoni? Kwa utu wake, na hadhi yake hawezi kamwe kutangamana na MAKAPI
 
Maneno Mazito sana haya.Dr Slaa tafadhali Mungu akutie nguvu uje uungane na Jeshi lako kumkomboa Mtanzania kutoka katika kifungo cha miaka zaid ya 53.
 
Kamanda G Sam kuna jambo hukuliweka wazi siku uliyotuhakikishia kwamba Dr.Slaa angeonekana kesho yake kwenye mkutano mkuu.

Pamoja sana mkuu, waache wenzetu watangulie sisi tutachukua fastjet rubani akifika tu tutashambulia kwa kutumia anga!!!!!! adui wakati huu lazima anyanue mikoni.

Matokeo ya mwanzo kabla ya vita venyewe kuanza, wameanza kwa kutishia nyau eti watashinda kwa namna yoyote ile.
 
"Kwa hakika tukiendelea kusubiri nachelea watu wataanza kukusahau kiongozi wangu mpendwa! Si unawajua WaDanganyika?";

Hilo nalo neno! chukua 5!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom