Mzee Kijana
JF-Expert Member
- Nov 25, 2011
- 1,405
- 1,086
Ktk dunia hii wamepita watu wenye madhambi makubwa na Mwenyezi Mungu atawaadhibu vibaya sana kama hawakutubia madhambi yao. Hebu fikiria hili: watu wametoka huko walikotoka wakahamia sehemu ambayo ni pori (Isimani) lisilo na huduma zozote. Wakavumilia mateso yote huku wakifanya kazi kwa bidii hadi Mwenyezi Mungu akawajaalia kupata riziki zao na kuwa wakulima matajiri wakubwa. Ghafla anatokea mtu mwingine kwa falsafa yake ambayo Muumba haikubali anataifisha mali zao na kuwahamisha ktk majumba yao na kuwapeleka anakotaka yeye kwa sababu ya huo uitwao Ujamaa! Hivi kosa hili halifai kuwa miongoni mwa madhambi makubwa? RIP Mwamwindi ulisimama imara kutetea haki dhidi ya batili na Mwenyezi Mungu siku hiyo ya hukumu ataonyesha ni nani kati yako na wao alikuwa sahihi. Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.