Dr. Ulimboka hatukuelewi ! ! !

Dr. Ulimboka hatukuelewi ! ! !

Ulimboka alishasema kila kitu, tena akiwa bado na majeraha, mwanahalisi likapigia mstari, mmefanyia nini hizo taarifa? Aje akanushe au arudie yaleyale? Nini kipya mnataka kusikia kutoka kwake?


Umesema vyema mkuu. Dr Uli alishasema kila kitu. Kwann watu wanajifanya kusahau haraka hivi?
 
Suala hili la Ulimboka nalifananisha na lile la Mwakyembe! Alipiga kelele nyingi na mpaka kuandika waraka. Alivyokuja, yeye mwenyewe akasema AMEFUNGA MJADALA juu ya afya yake. Kilichomtuma hatukijui ila tunaona alipandishwa cheo kutoka Naibu Waziri sasa ni Waziri kamili.

Kuna baadhi walitabiri kwamba katika mabadiriko ya baraza la mawaziri hasingekuwemo kwa sababu ya kauli za kupingana viongozi wenzake, yako wapi?

Sitashangaa nikisikia Dr. Ulimboka akitoa kauli kama: 'namshukuru Mungu kwa kuninusuru mengine namwachia yeye', 'nimezuiwa kuliongelea suala hili kwa kuwa liko mahakamani', 'nimeendelea kupata vitisho toka nirudi hivyo nina wasiwasi na maisha yangu', 'mambo yaliyotokea nilishasema kabla sijaenda kutibiwa hivyo sioni lipi la kuongeza'...

Mungu ibariki Tanzania!
 
hivi kuna ulazima gani aseme? wale waliowekwa kizuizini akina maalim seif, mapalala na wengine mbona hamuwalazimishi kuongea? Bora ashukuru Mungu kwa uzima aliobaki nao na akipewa nafasi ya ushauri katika moja ya balozi zetu apokee kwa mikono miwili akapumzike hata miaka 20
 
Tatizo sio ulimboka tatizo ni nyinyi madaktari mliokubali kurudi kazini wakati mwenzenu akiwa maututi. Na sasa hivi mnaendelea na kazi lakini mnataka yeye andelee na libeneke.
Exactly...
 
Mi nilishamdharau sana ulimboka

Huwa sipendi sana kupinga. Lakini nadhani Tumemtelekeza Ulimboka na finaly amehisi atabaki peke yake katika mapambano. akiwa mahututi alisema mengi, mwanahalisi likasema mengi tena kwa kufanya utafiti, kuingia kwenye mitandao ya simu na kuanika ukweli wote. Wakatafuta majina ya waliomtesa Ulimboka mpaka kwenye vitabu vya wapiga kura, wakatueleza, TUMEKAA KIMYA TUKISUBIRI PRESS CONFERENCE ! Kwakweli hakuna atakaloweza kusema tofauti na hayo. Naomba tufanyie kazi yale tuliyoyapata. Kama mwanahalisi limetamka, hatufanyii kazi mpaka gazeti limefungiwa, hayo atakayotuambia Ulimboka tutayafanyia nini ? sioni tunaloweza kufanya zaidi ya kuandika story tu kama vile "ULIMBOKA UFUNGUKA", "... AWATAJA WALIOMTEKA", "ULIMBOKA AKATA MZIZI WA FITINA" nk. Lakini mwisho wa story hizo utakuwa ni simulizi tu, I am sure hatujajiandaa kuchukua action yoyote zaidi ya kusubiria kufurahia stories !
 
Si unajua watz tena, mtishie kidogo, kisha mlambishe kajiasali kadogo kwisha habari yake! Atacheza kila ngoma utakayompigia. Mimi naamini kuwa kaasali na kakitisho kadogo kameshaminya haki za mamia ya watz. Si nnaijua sirikali yetu!. Uli angejua hisia zetu angeacha mchezo anaofanya. Hapo ujue anatafutiwa cheo na kazi nzuri na kajumba kanajengwa chapchap ndipo atakuja na kudai...ooh mimi ndiyo najua mchezo wote, aliyenidhuru ni yule aliyekamatwa! Nk, subirini tu mtasema nilisema

Hili ndilo jibu sahihi la hoja hii!!! Mjadala closed!!!!
 
kwasasa hayo yote ni maisha yake yatakayomuhusu yeye mwenyewe Dr ulimboka.Ameona bora kama ni kuhongwa gari/ajirampya/Pesa/ bora apokee tuu. kuliko Akielezea kila kitu kwenye media ili awafurahishe nyinyi na wanasiasa, then baadae hapati chochote zaidi ya uhasama na uadui na wanausalama.
 
Tunategemea kuskia mengi kutoka kwake,ukimya wake unatushtua! Au wamemziba mdomo kwa noti za kijani!? Anyway,Time will tell. Lets wait to hear from the organs responsible,labda na yeye ata rise na kusema chochote!
 
RAMADHANI IGHONDU mfanyakazi wa Ikulu

Ushauri kwa RAMADHANI IGHONDU, peleka tuhuma hizi unazosingiziwa mahakamani ili ujisafishe uwe huru mbele ya jamii. Hivi unavyotajwa tajwa sidhani kama unaishi kwa amani. Najitolea kukuwekea wakili na ukishinda lazima tulipwe fidia.
 
Mi nilishamdharau sana ulimboka

Sasa ww unamdharau kwanini? Hata akisema ww utafanya nn? Umeshayafanyia kazi mangapi? Kwa mfano yamesemwa ya APPLE, RICHMONDE, KASTURI, CHENJI YA RADI, ILIMLADI KOMBI....... ulichokua hatua gani?. Utaendelea kudharau milele. Anza kuchukua hatua kwanza acha excuses. Fanyia kazi zile za kwenye youtube na mtotohalisi kwanza.
 
Tuachane na mambo ya Ulimboka, muda ukifika ataongea kila kitu

Mwambie Ulimboka achunge sana na kuharibu jina la Usalam wa taifa na kutia Dowa ikulu .kuna ripoti ya uchunguzi itatolewa ikikamilika na Jeshi la polisi ambayo itaweka bayana uongo wa huyu kiumbe Ulimboka ,kwa kifupi tu inasemekana ni watu waliokuwa wanamdai mamilioni ya fedha ndio waliokuwa nyuma ya tukio hilo.
 
Hii ndo njia watakayoitumia kummaliza safari hii hata kama ataenda nje ya nchi tena huko ndo rahisi. Dalili zote ukizisoma hapa chini na ukilinganisha na hali ya Dr. Mwakyembe ni perfect match

Symptoms of arsenic poisoning begin with
headaches, confusion, severe diarrhea, and
drowsiness. As the poisoning develops,
convulsions and changes in fingernail
pigmentation called leukonychia may occur. When
the poisoning becomes acute, symptoms may
include diarrhea, vomiting, blood in the urine,
cramping muscles, hair loss, stomach pain, and
more convulsions. The organs of the body that are
usually affected by arsenic poisoning are the
lungs, skin, kidneys, and liver. The final result of
arsenic poisoning is coma to
death

KOFIA na GLOVES mmepata jibu!

Watanzania kwa kupenda kudanganyana! hadithi kama hizi si uwasimulie wajukuu zako?
 
Huyu ndugu yetu alikumbwa na machungu yaliyomgusa kila mmoja wetu! Nchi nzima ilizizima, na kuamini (nakuweka msisitizo kwenye tunacho fahamu) kua vyombo vya dola ni wabaya. Tukajitolea kwa matibabu yake, hadi kufikishwa hosiptali SA ambapo hata huko tulihisi serikakali ya Tz bado ingaliweza kumfuatilia na kummalizia !. Mimi kama mimi iliniuma sana.

Tunashukuru Mungu, kwa uwezo wake kapona na karejea nchini. Watu walitoa maoni mengi mitandaoni ambayo naamini ilimfikia kua akija aibukie press conference na kuyasema yote. Hataivyo, kutokusema siku ileile hatukushangaa sana maana jamaa lazima apumzike japo kidogo! Na akusanye kumbukumbu vizuri hata kukumbuka simu yake ilipo! .

MY TAKE:
1. Huu muda uliotumia kukusanya kumbukumbu ni mrefu sana,
2. Unajaza wasiwasi.
3. Hicho unacho subiri kwanini usieleze uma?
4. Hukumbuki kua wewe ungalikwisha 'decompose' (inaniuma sana)
5. Unaumiza vichwa vya watanzania wengine wapenda haki.
6. Vikao na kamati za serikali ni vyanini tena wakati walipopanda gari kukuacha Msituni usiku walijua wamekuua?
7. Utakayo yasema hata sasahivi, bado kutakua na hojaji tofauti kisa kutokuaminika tena.
8. Kumbuka ulishasema watu waachane na familia yako , wewe ndio ufahamuye ukweli.
9. Kumbuka kuna mengi yaliyo wakumba wanao kutetea
10. Mods naombeni msichanganye hii thread na ile inayosema " polisi leo kufunguka. . . . "

Hongera Ulimboka sasa Umefunguka maana hapa TZ kelele nyingi vitendo hamna mambo yakiharibika kama yalivyoharibika kwa ma-dr, ni wewe peke yako uliumiza na kupata maumivu, familia yako ndiyo ilipata hasara na ukiwa. Ma-dr wenzio wakarudi kimya kimya kazini.

Umefunguka Ulimboka hongera huna muda wa kuanza malumbano na serikali wakati wanasema 'togather we stand alone you fall'. Jinyamazie endelea na shughuli zako upate maendeleo na familia yako mambo ya WaTZ kujifanya eti ongea ilikuwaje, itakuwa kwa manufaa ya nani???
achana nao
 
huyu ameisha tulizwa subiri wammalize taratibu, imekuwa unafiki sana. Wakiwa kwenye matatizo watanzania niombeeni mwenyezi Mungu akinijalia kurudi salama nitakuja kueleza yote, wakirudi baada ya kulambishwa asali wanakuwa kimya, je mmesahau na Mwakyembe?.

Unahakika na unacho ongea au ni opinion yako tu kaka. Wewe umeshafanya au kusaidia nini toka issue ya Dr. Uli. Au kujifungui ndani na laptop na moderm. Haya mambo ni rahisi ukiwa ndani na laptop, lakini believe me ni issue nyingine kama wewe ndio upo front. Naamini Dr. ameshafanya mengi ya ujasiri na iwapo kama tunaona yeye ameshapewa chochote ajitokeze mwingine aendeleze pale alipoishia
 
Dr. Ulimboka ametishiwa maisha lazima ajitahadhari sana. Hawezi kutoka hadharani akatamka kitu dhidi ya jeshi au wahusika wakuu.
 
Mimi nahisi huyu jamaa alikua amepiga pombe sana, hata hajui kilichotokea vizuri. Sina ufahamu vizuri kama anaweza kusimama na kusema chochote, maana yawezekana sana ikawa (ni /au ) siyo usalama umehusika.
 
Mi nilishamdharau sana ulimboka

Unamdharau Dr. Uli kwa kosa gani?...unataka arudie story gani ambayo hajaizungumzia? Hapa swala ni kuchukua hatua kwa yale tulioambiwa nayeye mwenyewe (Dr.Uli) na gazeti la Mwanahalisi. Otherwise tusimsukumie mzigo mwingine tena kha!!!
Tatizo si taarifa, tatizo is WHAT DID WE DO WITH WHT WAS ALREADY SAID? Hapa tukae kimya tu maana ineonesha hatuwezi kuchukua hatua, wote ni waoga kama mimi, so tusilazimishe mwenzetu awe tofauti.
 
Back
Top Bottom