Kwani mkuu unafikiri watumishi wa umma hawana vyama? Akikosa nafasi ya kisiasa anarudi kwenye utendaji ambacho hakiruhusiwi ni kuonesha maslahi ya Chama kwenye utendaji basi.
jembe shambani kwako labda.Wewe haujuı maana ya kada.Katiba inasema chama kitampendekeza mtu kinayetaka awe spika.Spika sıyo lazima mwanachama hata km ataungwa mkono au kupendekezwa na chama fulani.Huyo Atson hataweza kubabaishwa na bush lawyers wa UKAWA.Nı jembe balaah!
Ag ni mwanasiasa kwa nature ya nafasi yake.Spika sio mwanasiasa,hvyo hakuna kosa wa kasoro.Ameomba nafasi hyo kupitia CCM km ambavyo angeweza kuomba kupitia ACT,NLD n.k.
Mkuu VUTA-NKUVUTE ,Naweza kuamini kuwa sasa umeshaanza kunogewa na vyeo. Ulianza kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Ukafuata kuwa kiongozi wa Kamati ya Bunge Maalum la Katiba. Kama hiyo haitoshi, ukateuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Sasa unataka Uspika wa Bunge.
Ukiwa ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hukupaswa kujitokeza kisiasa na kugombea Uspika wa Bunge. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali si mtu mdogo. Ndiye Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale ambapo Bunge hufanyika kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali huwa Bungeni Dodoma. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mtu wa kitaifa zaidi.
Kujianikaanika kama kada wa CCM si jambo jema wala vutizi. Kutakuwa na kitu na watu wanaosababisha. Nani kakutuma? Unataka nini hasa? Kwanini? Dr. Tulia, umejianika kama kada. Watumishi wa Ofisi yako na wananchi kwa ujumla watakuonaje ikiwa utaendelea kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
Ili kulinda heshima yako, jiuzulu Unaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na urejee Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ukahadhiri pale ambapo Uspika utagoma kupatikana. Ujiuzulu haraka!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Kifungu gani cha sheria au kanuni kinamkataza kuwania hiyo nafasi?
Huyu pale wizarani anafanya kazi kama katibu mkuu,ndio maana WIZARA hiyo haina katibu mkuu,pia huyu ni Deputy Attorney General ambaye wakati mwingine huwa anaenda mahakamani kuitetea serikali au maslahi ya umma,pale ambapo serikali inawashtaki kijinai chadema,NA yeye akawa mmoja wa prosecutor,inaleta picha gani? Ni wazi picha ni kwamba kada wa Ccm kaanda hati za mashitaka, kada wa Ccm kwa kujificha kwenye cheo cha unaibu mwanasheria mkuu anawashitaki,hatakuwa fair,lazima ukada utamuongoza kuwakomoa wapi zani wake kisiasa,hata kama katika hali ya kawaida angetakiwa asipeleke mashtaka mahakamani
haya mambo yapo kila mahali mfano chadema kuteua viti maalum ilhali bado ni ccm ajabu kabisa.