Nimesoma Maoni wengi wameandika vizuri tu, mimi maoni yangu ni haya;
Chadema wanayo nafasi ya kushinda ikiwa watamchagua mtu miongoni mwa wanaigunga na awe ni mtu anayekubalika na kufahamika.
Swala la Dini halina msingi sana hapo igunga na hata watanzania walio wengi kote nchini hawalipi nafasi.
Swala la Wapinzania kuungana halina maana na halifai kusikilizwa kabisa, utamwachia CUF then akiingia bungeni anafundwa kuwa mpinzani wa Chadema badala ya CCM.
Kuhusu watu waliomlilia RA ni kwamba kwanza njaa mbaya na pili ndugu zangu wa Tabora yaani wanyamwezi wengi wao wavivu wa kujishugulisha na huwa wanaridhika kwa kitu kidogo sana, na hiyo siri RA aliifahamu na ndio maana akawa anawadaganya kwa vitu vidogo sana kama kuwapa vijisenti, kofia, fulana , khanga n.k
ila Watu hawa wakieleweshwa vizuri wakaelewa huwa wanabadilika na kufanya maamuzi magumu na huwa hawarudi nyuma tena.
Chadema wanapaswa kuwapeleka watu makini Igunga watakao ongea kwa lugha rahisi itakayowaingia wanaIgunga na hatimaye kuamua kufanya mabadiliko ya kweli, Waelezwe jinsi mkoa wao ulivyo na dhuluma amabayo ccm imeufanyia, kwa mfano waelezwe kwamba TBR ni kitovu cha elimu lakini hausaminiwi, ni kati kati ya nchi lakini ulitengwa kwa kutokuwa na miundombinu ya kunganisha na mikoa mingine, waelezwe jinsi walivyokuwa wakikopwa Tumbaku yao ilihali watoto wao wakifukuzwa shule kwa kukosa ada, waelezwe jinsi amabvyo Afya, maji , umeme vinayowasumbua katika maisha yao.
Naamini wakielezwa kwa Lugha sahihi wataigeuka ccm ambayo naamini walishaigeuka tangu mwanzo ila walitishwa na wengine kuhongwa na hata kuibiwa kura.