Usiwadharau mkuu, hii mbona ni kawaida sana kwa upande wa saikolojia? Ukimnyanyasa mtu kwa muda mrefu anaona ni sawa tu/inakua mazoea. Kwa Wana-Igunga waliolia inawezekana wanaona ni sawa kutawaliwa na kunyang'anywa rasilimali zao na Rostam) na wamepoteza identity yao kabisa wanaogopa change. Chukulia mwanamke au mwanaume aliyekuwa abused muda mrefu; unaweza ukampeleka mpaka kituo cha polisi lakini akakataa kufungua kesi, leave alone kuwa witness. Hawa watu for more than 15yrs wameshaharibiwa "psychologically" wanaona bila CCM hawawezi kuishi. Tunahitaji watu wakuwaambia na kuwaonyesha change is necessary and is possible; it is desperately needed now in places like Igunga. Igunga deserve a better leader/MP.Wakiona kwa vitendo mind zao zitafunguka taratibu.
mimi nitagombea mwaka 2015 sasa hivi nahangaika na mambo yangu ya phd mzee..asante kwa kunitabiria ..saint ivuga
Mimi ni mnyamwezi na nafahamu mazingira na khulka za wanyamwezi, juu ya alichofanya Rostam...CCM ISAHAU JUU YA USHINDI WA HAKI KATIKA MKOA WA TBR ktk chaguzi yoyote ijayo. Ni doa na pigo kubwa sana kwao CCM TBR, waila kwa wasioufahamu vema mkoa ule...wanaweza kudai kwamba CCM inaweza kuwa hai kwa miaka 10 ijayo.Dr Slaa mnapaswa mmuweke mtu ambaye ni kweli anatoka TBR, asipandikizwe mtu kinadharia kuwa ni mzawa wa TBR...wale hawachelewi kumsusa. Pelekeni mtu asilia ya mkoa ule na walau anajua lugha ya kinyamwezi na shupavu, MTASHINDA.
Mkuu unaelewa unachokisema? Kuna Wanyamwezi wa Dakama (Tabora) na Wanyamwezi wa Sukuma (Shinyanga na Mwanza). Sasa sijui kama ulielewa ulichokua unaandika.
Mbuzi kala mkeka,wapambe mtakalia nini?Taraatiiibu jua limeanza kuchomoza.
tena wanamlilia mtu aliyetufilisi! Wametia aibu kwa kweli.[/QUOTE
kwetu igunga katujali, kama fisadi sawa tu mana ufisadi wake umeleta maendeleo, tuna zahanati kila kijiji, umeme, n.k
tutakukumbuka rostam
Jina lako sawa linaonesha na wewe ni Msukuma (sitaki kukuita Mnyamwezi wa Sukuma kama unavyotaka kunilazimisha niamini). Kwa taarifa yako haya ni makabila mawili tofauti ingawa wanasikilizana, labda kama umesoma yale masomo yetu ya kuimba mashairi utusaidie historia fupi ya haya makabila mawili (unayotaka kutuambia kuwa ni kabila moja). Tunachokifahamu watu tunaotoka Mwanza ni kwamba Sukuma ni Kaskazini na Dakama ni Kusini, hivyo ningekuelewa kama ungesema kuna Msukuma wa Sukuma na Msukuma wa Dakama (Kwa maana ya Mnyamwezi).
Hivyo niliposema kuna Wasukuma na Wanyamwezi nilitaka kuweka msisitizo kwamba hayo ni makabila mawili tofauti. Nenda hata sasa hivi huko Tabora, Mwanza na Shinyanga utasikia hivyo hivyo wala hakuna kitu kinaitwa Mnyamwezi wa Dakama au Mnyamwezi wa Sukuma (Shinyanga na Mwanza kama ulivyosema). Pole sana kama umekaririshwa!!
Mbona muiran aliweza kuwa mbunge kwa miaka kibao? Sema waweke mislamu kwa vile TBR inawaislamu kibao!