Mbinu iliyobakia sasa ni kulipa watu kutoa matamko, kila kukicha ni matamko. Na hii mbinu nyingine ya kutumia mahakama, bundi bado hajakubali imeshindikana. Najua kikundi cha wasaliti kimeishiwa mbinu sasa kinanunua wajumbe na kuwatumia watawala kuishinikiza mahakama. Huwezi kuzuia mabadiliko kwa hulka zako za kupenda uongozi.
CCM lazima wajue wale watoto elfu 11 na wengine wengi wanaotafuta ajira bila mafanikio ndio watawatoa madarakani. Wazee waliostaafu bila malipo ndio watawatoa madarakani, matumizi mabaya ya ofisi za umma na uhujumu uchumi ndio utawatoa madarakani, Wizi, upendeleo, rushwa na maisha duni ndio adui yao namba moja.
Kuindamana CDM kwa kutumia mamluki na wenye tamaa haitasaidia, watanzania wamechoka na ahadi hewa.
Tumechoka na wachache kuhodhi nchi na uchumi wa nchi.
Hizi Rushwa za kisiasa mnazotumia kuteka watu, ni sababu tu ya ukosefu wa ajira na wachache kuchumia matumbo. Watanzania wanataka mabadiliko na hakuna anayeweza kuyazuia, hata mkiindamana vipi CDM mabadiliko ni lazima.
Binadamu akichoka kitu huwezi tena kumlazimisha. Ni wajibiu wa CCM na mamluki wake wote inaowatumia kujikita zaidi kurusdisha imani kwa wananchi kwa kugawa keki ya Taifa sawa na kutimiza wajibu badala ya kutumia hongo, hila, matamko ya kulipia, kesi za kutengeneza, na kulinda wasaliti mahakamani.
Wasaliti:
Dhambi ya kuwakaanga watanzania kwa tamaa zenu za fedha na madaraka zitawatokea puani, mtahangaika sana. Rudini kwa wananchi kwa ukweli acheni kutunga maneno kwa fedha za CCM. Adui wa Mtanzania ni umasikini na maisha duni, afya mbovu na elimu mfu, wizi wa mali za umma na wachache kuhodhi nchi. Mkishindwa kusoma ishara za nyakati nyakati zitawasoma ninyi.