DR SLAA: Vurugu za Arusha zimenifungua macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR SLAA: Vurugu za Arusha zimenifungua macho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PayGod, Jan 19, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dk Slaa: Vurugu za Arusha zimenifungua macho Send to a friend

  KATIBU Mkuu wa chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema tukio la vurugu walizofanyiwa na jeshi la polisi mjini Arusha, sasa zimemfungua macho na kuona nini ambacho kinasukuma nchi kuingia katika machafuko.

  "katika maisha yangu, sijawahi kuona mambo ya ajabu kama waliyofanya polisi Januari 5 mwaka huu, nilikuwa kwenye mkutano nahutubia walinirushia mabomu na sikuweza kuona kabisa," anasema Dk Slaa.

  Katibu huyo wa chadema ambaye, alikuwa mgombea wa Urais wa chadema mwaka 2010, anasema alibaki akiduwaa juu ya jukwaa huku umati wa watu uliokuwa umefurika uwanja wa NMC Arusha ukitawanyika.

  "Nilishangaa, nikasema mbona mkutano wetu una kibali...hakuna aliyenijibu, vijana waniambia shuka mzee utakufa ndipo nilishuka chini ya jukwaa na walinipa maji na kuanza kunawa machoni," anasema Dk Slaa.

  Katibu huyo, anasema baada ya muda, alipata taarifa viongozi wengine wa chadema, walikuwa tayari wamekamatwa katika vurugu za kuvunjwa maandamano.

  Dk Slaa anasema baadaye alipanda tena Jukwaani na akawaita wananchi na wakaendelea na mkutano ambapo mwisho ndipo vurugu nyingine zilianzishwa tena na polisi.

  "Nilikuwa sijuwi kinachotokea....pale pale uwanjani wakajitokeza vijana wawili mmoja ameripukiwa na bomu mguuni na kuungua na mwingine bomu lilimpasua hadi alama zake zikawa zinaonekana wote damu zilikuwa vinawavuja"anasema Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema alisema katika kampeni zilizopita za uchaguzi mkuu, alifanya mikutano ya hadhara zaidi ya 400 hakuona fujo za aina yoyote zikitokea.

  Slaa ambaye hivi sasa ni mmoja kati ya wafuasi 29 wa chadema, waliofunguliwa kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali, anasema tukio la Arusha limempa funzo kubwa la ukiukwaji wa sheria na taratibu nchini.

  Anasema kabla ya yeye kufika Arusha, alipata barua toka kwa msajili wa vyama vya siasa John Tendwa, ikiwaruhusu kufanya mkutano na maandamano.

  "Tangu desemba 22 ofisi za msajili wa vyama vya siasa na jeshi la polisi walikuwa na taarifa za mkutano wetu na maandamano na wakati wote nilikuwa nawasiliana na msajili," anasema Dk Slaa.

  Katibu huyo wa chadema anasema, walikubaliana na Tendwa kabla ya Januari 4 mwaka huu wawe na kikao cha pamoja baina ya chadema, ofisi za msajili, polisi na ofisi ya waziri mkuu.

  "Ilipofika jioni Januari 3, saa 10 nilimpigia simu Tendwa na kumkumbusha akasema bado hajarudi Dar es Salaam ila tayari alifanya mawasiliano na Waziri Mkuu, Mizengo PInda na IGP said Mwema," anasema Dk Slaa.

  Dk Slaa anasema baadaye Tendwa baada ya kuongea naye mara nne alimweleza kuwa, waendelee na mkutano na maandamano na kikao chao kitafanyika baada ya Januari 5 mwaka huu.

  "Tendwa akaniuliza sasa katika kikao tukiwa na waziri mkuu, ajenda zitakuwa zipi nikasema..ajenda tutazipanga kwenye kikao...tukakubalina," anasema Dk Slaa.

  Anasema Januari 4, saa sita wakati anaondoka Dar es Salaam kuja Arusha akampigia tena simu, Tendwa na kumweleza kuwa sasa anakwenda Arusha.

  "Nikiwa njiani Tendwa akanieleza amewasiliana na viongozi wengine je, kama wakitangaza uchaguzi wa Meya kurejewa, watasitisha maandamano,..nikwamwabia hatuwezi kwani tayari tumetangaza kwa gharama kubwa na watu wamejiandaa," anasema Dk Slaa.

  Anasema baadaye saa 10:30 alimpigia simu Tendwa kumuulizia kuhusu barua ya kuruhusu mkutano wao na maandamano akamuomba ampe Email Adress ili amutumia.

  "nikamtumia na ila baadaye barua ikawa imepelekwa ofisi za chadema Dar..nikampigia kumshukuru kwani walipoipata Dar nikawaomba wanisomee na nikaielewa," anasema Dk Slaa.

  Anasema baada ya hapo, safari iliendelea kuja Arusha lakini ikamlazimu alale njiani na Januari 5, ndipo alimalizia safari na majira ya asubuhi alifika Arusha.

  "baada ya kufika nikwenda hotelini na baadaye tulianza kujiandaa kwenda katika mkutano na hapo nilielezwa kuwa kulikuwa na taarifa za mkuu wa jeshi la polisi kusitisha maandamano....nilishangaa lakini pia nikaoneshwa barua ya kuruhusu maandamano na mkutano , barua ya mkuu wa polisi mkoa wa Arusha," anasema Dk Slaa.

  Dk Slaa anasema baada ya kuondoka Mount Meru Hoteli walianza kutembea kwa miguu kwenda uwanja wa NMC na walipofika njiani yeye na mzee Ndesamburo waliamua kupanda Magari ili kwenda kuwapokea viongozi wengine.

  "Sasa mpaka hatua hii sidhani kama tulikuwa na makosa na matembezi yale yalikuwa ya amani tumevaa vitambaa vyeupe na baadaye ndipo vurugu zikatokea," anasema Dk Slaa.

  Anasema kwa mazingira ya sasa, hawadhani kama serikali ina nia njema na chadema na hawatarajii kufanya mazungumzo tena.

  "Namshangaa Nahodha (Waziri wa Mambo ya Ndani) yaani baada ya kuuwa watu ndipo anataka mazungumzo, hatuwezi kukaa tena," anasema Dk Slaa.

  Katika vurugu hizo hadi sasa, watu watatu wamefariki dunia na watu wengine zaidi ya 31 walijeruhiwa
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  mimi bado nashangaa askari waliopiga wanawake kwenye maandamano
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Malipo ni dunia hapa hapa ,wanofikili watadumu kama mawe ndo wanapiga watu hovyo.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nieipenda signature yako well na mengine ya hapo juu nimekubaliana nayo!
   
 5. Don Alaba

  Don Alaba Senior Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukweli mtupu kila maamuzi yanayofanywa na serikali yametawaliwa na siasa
   
Loading...