Dr. Slaa: Uongo ni dhambi na siko tayari kuishiriki!

Dr. !

Mwachie huyo fisadi achague katibu mkuu wa chama anaye mtaka yeye ...... Eeheee si ameuziwa chama!

Ni kweli, kwa kuwa chama kimeuzwa ni heri wawaache wanunuzi wenyewe wachague Katibu wao wa kuandaa namna watakavyoiba wakiingia ikulu.

How come Dr Slaa awe mpambe wa fisadi Lowassa wakati akijua kuwa kundi hili linalotumia pesa za kifisadi kuingia ikulu linakwenda kwa ajili ya kutafuta kurudisha pesa walizotumia?yaan leo mwanachadema anyejiita mzalendo eti anawapigia kampeni akina Rostam Aziz, Karamagi, Change na wezi wengine warudishe pesa walizopoteza kuhonga ili Lowassa awe Rais?alafu unajiita una uchungu na nchi?shame
 
Wale bendera fuata upepo tayari wameshapotezwa,wamebaki macho juu kama abiria kapoteza nauli.

Mtu kama Slaa aliyemnaga Lowassa juzi tu mchana kweupe,yahitaji moyo kuanza kumnadi.

Nilishasema humu nadhani last year kwamba hao ma-pro walioko hapo ni njaa tupu hata hawajielewi,hawawezi kumshauri lolote la maana wala kuhoji maamuzi ya Mbowe yaani wapowapo tu.

Na nilihitimisha kwa kusema ATAKAYEIUA CHADEMA NI MBOWE MWENYEWE. wala siyo hao mnaoaminishwa ni wasaliti.

Lowassa (mliyetuaminisha ni fisadi) anakuja huko na karibia nusu ya ile orodha yenu ya Mwembayanga na kwa kuwa ndo ma-Don tayari chama ni chao so itakuwa ni branch ya mafisadi tu kama CCM.

Ngoja tuone.
 
Hujashangaa yule mwizi na fisadi eti ndio shujaa wa Chadema?zamani ukivaa ngwanda ulikuwa unaonekana kamanda lakin sikuhizi ukivaa ngwanda maana yake kibaraka wa mafisadi maana chama kimeishauzwa sasa, akina Rostam Aziz, Change, Karamagi na wezi wenzao wanasubiri kumuingiza Ikulu fisadi mwenzao Lowassa ili waile nchi.

Ni heshima kubwa Dr Slaa kukataa kuwa kuwadi wa mafisadi hawa

haya maneno yana ukweli ndani yake na ni mazito kwelikweli.
 
Hawa ndio Makamanda.. Raisi wa mioyo yao wanapomkana kisa Fedha za Fisadi.
 
Nadhani ingekuwa bora watanzania wote tungeungana kupiga vita ujinga wa kutuletea viongozi mafisadi wa kuwapigia kura.CCM wametuletea muuza nyumba za serikali,barabara zetu zinajengwa chini ya kiwango pesa zote zinaingia mifukoni kwao inshort wote wawili Magufuli aka Makomeo na mwenzake Lowassa aka Edo hawatifai kabisa.

Tuchague viongozi wanaoonekana kuwa na uwezo wa kusema hapana kwenye rushwa na ufisadi na wanaonekana hivyo.Lakini kwa hawa wawili hakuna anayetufaa.
Unafikiri tufanye nini ikiwa sisi hatuna uwezo wa kupendekeza na wala hatumo kwenye kamati zao
 
Sasa hapo amezira?hivi wewe unatumia akili ya kawaida au tui la nazi?subiri tarehe 8.8.2015 tuimalizie kazi nanyi ccm mgawane mbichi

Shift yako imeshaisha..team ya propaganda mmeshindwa kufunika moshi...kibaruachako kiko mashakani
 
teh teh chadema walichofanya ni sawa na FC Barcelona imsajili Ronaldo halafu Messi aombe kuondoka

Hujui kitu, Lowassa kanunua hiyo nafasi kwa pesa Billion 12, Lowassa nyuma yake yupo Rostam Aziz, Karamagi,Chenge na kundi kubwa la wezi na mafisadi, wanataka kwenda ikulu.Ndicho Dr Slaa ambacho hakubali, kushiriki dhambi hiyo ya kulihujumu taifa.
 
Yericko,

Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.

Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.

==========
Moderator:
Baada ya wadau kutaka maoni ya Dr. Slaa yajitegemee na hoja ya Yericko ifungwe, tumeona ni vema kuiweka hoja hii ikijitegemea kama ilivyopendekezwa. Majibu ya msingi yapo hapa

mzee wangu ondoka kwa hawa waganga njaa,,, wale ni worse than traitors kwasababu hawana course... usikae nao vikao kwa maana wao ni wenye mizaha
 
Lengo kuu ni nini kwa wapinzani?
Dr.W.Slaa agombee uraisi au CCM kuondolewa madarakani?

Takwimu za kitaalam zinasemaje tuachane na haya mambo ya mitaani?
Dr.W.Slaa alishapata hii nafasi na alikuwa na ushawishi mkubwa lakini haikuwa kama ilivyotarajiwa.

Na bado anayo nafasi kama mwanachama wa CHADEMA kuchukua fomu ndani ya chama chake akapambane na watia nia wenzake ndani ya chama chake na atayetoka kidedea apelekwe kwenye jopo la mchujo mwingine wa UKAWA.

LAKINI HII YA KUKAA KIMYA INATIA MASHAKA SANA NA MTAZAMO WAKE MZIMA WA KISIASA. NA KWA HILI LA KUKAA KIMYA AU KUTAFAKARI INAONYESHA UFAHAMU WA Dr.W.Slaa KATIKA DEMOKRASIA AMBAYO NI NGUZO KUU YA CHAMA CHAO IMEMPITIA PEMBENI.

Ngoja nimkumbushe Dr.W.Slaa nia na dhamira yake kubwa iliyomfanya ajiunge na CHADEMA AU Upinzani ni kuitoa CCM madarakani na siyo yeye kuwa raisi kama inavyoashiria sasa.

Then kipawa cha Dr.W.Slaa in leadership will be questionable if he decides to step down from Chadema?

Once Mzee JK Nyerere aliwahi kusema " kila alipotaka kustaafu viongozi wengine kwenye serikali walikuwa wanamwambia Mzee usiondoke, nchi yetu bado ni change sana.Kumbe baadae alikuja kugundua uchanga waliokuwa wanauzungumzia ulikuwa ni familia na mali zao na siyo inchi kama walivyokuwa wanavyoashiria."

Pia aliulizwa swali kwanini ulishindwa kuiunganisha Afrika ikawa moja kama ulivyokuwa unadhamiria? Mzee Nyerere akajibu " ni nafsi za watu ndizo zimekwamisha, wale maraisi alipokuwa anahimiza katika kuungana wao walikuwa wanafikiria nafsi zao kwani mimi nitakuwa nani kwenye huo UMOJA. Na ukishaanza kujiuliza maswali hayo malengo mazima ya UMOJA yanasahaulika."

Chaguzi za siku hizi zinakwenda kwa takwimu na Slaa analitambua hilo vyema, ikiwa kama takwimu zinatoa ishara tofauti kwa Dr.W.Slaa basi aseme kuliko kukaa kimya.



Hivyo Dr.W.Slaa kama kweli wewe ni kiongozi shupavu na unajiamini kwenye kipawa chako cha uongozi nategemea utatangaza nia na unenda CHADEMA ukachukue fomu upambane na Lowasa kwenye kamati kuu. Na atayeshinda huko ndiyo atakuwa mwakilishi na atayeshindwa atasimama kidete na mshindi ili mtimize nia na madhumuni yenu ya kuitoa CCM madarakani na si vinginevyo.

LA SIVYO UTAKUWA UMEUTANGAZIA UMMA KWAMBA WEWE NI MPENDA MTEREMKO NA USIYEPENDA USHINDANI, HIVYO HUFAI KUWA KIONGOZI WA UPINZANI SABABU HUNA NIA NIA NA MADHUMUNI YA KWELI YA UPINZANI.

We are waiting Dr.W.Slaa

Dr.akachukue fomu wapi na tayari uongozi umeshaamua mgombea ni Lowassa peke yake?
 
Last edited by a moderator:
Yaani mi nimebaki speechless kwa hizi siasa za TZ

Tulitaka Dr Slaa ajitokeze kueleza ukweli kinachoendelea, leo ameshindwa kukaa kimya tokana na propaganda chafu zinazoendeshwa na Yeriko.

Mada niliyoleta kuhusu Udikteta wa Mbowe ndani ya Chadema, msuguano wake na Dr Slaa na kisha kununuliwa na mafisadi Dr ali like kwamba mada iliakisi ukweli wa yanayojilia.

MboweKanisa.jpg

Mbowe kaharibu chadema kwa kukaqa kusikilizana na baba mkwe weke Edwin Mtei.
 
Hii mada kama kweli kaweka Slaa mwenyewe! Basi Slaa ni mtu wa ovyo kweli, lietawaliwa na uchu wa madaraka.

Hujui unachokisema, Lowasa kanunua nafasi hiyo kwa pesa, Mbowe kahongwa.

Lowassa nyuma yake kuna kundi la mafisadi wa CCM, ndio wanaotoa pesa hizo kununua ikulu.

Dr Slaa kushiriki uchafu huo ili mafisadi anaowapinga sikuzote waende ikulu wakawaibie watanzania litakuwa ni kosa kubwa sana.Kwa hapa Dr Slaa kafanya uamuzi makin
 
Yericko mtoto mwenye laana ya mzaz wako

Hatimae leo unakataliwa mchana kweupeeee

Na mtu uliekawa unapenda kujipendekeza kwake

Kilichobaki mwana izaya wewe ni kuolewa tuh
 
Dr slaa..watu wanaokushabikia leo ni akina Lizaboni ni Ritz kutoka Lumumba..kwa mara ya kwanza wanakuita mzalendo mwenye msimamo..tafakari
 
Yericko,

Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.

Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.

==========
Moderator:
Baada ya wadau kutaka maoni ya Dr. Slaa yajitegemee na hoja ya Yericko ifungwe, tumeona ni vema kuiweka hoja hii ikijitegemea kama ilivyopendekezwa. Majibu ya msingi yapo hapa

Dr Slaa please don't go wengine tuna presha za kushuka bora ujinyamazie tu shujaa wetu Mungu atakubariki sana.
 
Back
Top Bottom