Dr Slaa; Tafadhali Pokea ushauri huu

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Dr pole kwa mapambano ya kulikomboa taifa hili. naomba nishauri kupitia jf nadhani ujumbe utakufikia. si jambo jipya lilishasemwa sana ila nataka kujua hatua iliyopigwa. tunashauri kuhusu kufungua matawi ya cdm nchi nzima. kuna watz wengi wanapenda kujiunga na chama tatizo hawajui wapate wapi kadi. mtu ambaye ni mwanachama anakuwa responsible zaidi na kwa vile wanakuwa na vikao anapata nafasi ya kutoa mawazo yake. hawa ndio wanawahimiza watu kujiandikisha, hata kuwapitia majumbani wakapige kura na kusimami
https://www.jamiiforums.com/
 
Hakukua na haja ya kuanzisha thread ya kuomba kadi, unge m-pm tu dakta Slaa. Ni muungwana sana atakujibu tu
 
tena nimekwenda huko Kijiji cha Mtega one of remote and high mountain areas ilikuwa wilaya ya kilosa sasa ni Gairo .... wananchi wanataka kusikia CHD tuu
 
Hakukua na haja ya kuanzisha thread ya kuomba kadi, unge m-pm tu dakta Slaa. Ni muungwana sana atakujibu tu
Hapana palikua nahaja kubwa sana ya kuanzisha thread kwa faida ya wote, huwezi jua ni wangapi katusaidia kwa post hii.
Na kwani kuanzisha thread ni kumshutumu mtu.
I really hope hauko ngazi yeyote ya ushauri au utekelezaji katika organisation yeyote!

Asante ibange for this very useful post!
 
bahati mbaya msg ilikatika. cdm lazima iweke malengo ya kuwa na wanachama hai milioni kumi. kila kijiji na mtaa uwe na tawi hai na linalofanya vikao. kila mkoa uwekewe malengo ya idadi ya wanachama. haya yafanyike kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa. pasaka njema
 
nakubaliana na wewe mkuu
 
Mambo ya tawi kila mtaa yamepitwa na wakati hii sasa ni dunia nyingine si ya TANU, CCM mbali kuwa na Tawi kila uchochoro lakini bado inakimbiwa na wanachama. Kinachotakiwa kwa chama ni kuangalia maeneo muhimu ambayo yanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kama vyuoni, mashuleni na kadhalika, kuna wakati mwingine matawi ni kuongeza mzigo na migogoro tu kwa chama, hata unapotaka ku invest lazima kuwe na feasibility study si kuanzisha kila unapoambiwa kuna wateja angalia kama kuna raw materials na zita last kwa kipindi gani.
 
Nadhani ili ni jukwaa la siasa,mleta mada uko sahihi kabisa! Cdm kwa kweli ikifanikia kutwaa wasomi wa kutosha,nchi itakombolewa! Huwezi amini cdm kwa kumbukumbu zangu ilikuwa na wanachama kama laki3 lakini ilipata kura zaidi ya mil2 baada ya Nec Structural vote adjustment! Hapa inaoneka kuwa 85%ya wapenda cdm si wanachama hai. Upande wa ccm wanachama walikuwa mil.3,520,000 lakini ilipata kura mil.4 baada ya Nec upward bonus! Je, kama hawa wangekuwa wana wa chama wa cdm hali ingekuwa vipi? Tafakari,chukua hatua!
 
Mambo ya tawi kila mtaa yamepitwa na wakati hii sasa ni dunia nyingine si ya TANU, CCM mbali kuwa na Tawi kila uchochoro lakini bado inakimbiwa na wanachama. Kinachotakiwa kwa chama ni kuangalia maeneo muhimu ambayo yanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kama vyuoni, mashuleni na kadhalika, kuna wakati mwingine matawi ni kuongeza mzigo na migogoro tu kwa chama, hata unapotaka ku invest lazima kuwe na feasibility study si kuanzisha kila unapoambiwa kuna wateja angalia kama kuna raw materi
 
bahati mbaya msg ilikatika. cdm lazima iweke malengo ya kuwa na wanachama hai milioni kumi. kila kijiji na mtaa uwe na tawi hai na linalofanya vikao. kila mkoa uwekewe malengo ya idadi ya wanachama. haya yafanyike kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa. pasaka njema

Naunga mkono hoja. Unajuwa CDM yapaswa kufikiri na kwenda mbali zaidi. Iko haja kubwa ya CDM kuhakikisha kuwa huko vijijini wapiga kura wanaielewa na kujiunga na CDM kwa wingi zaidi. Kwa mfano, ziara aliyoo fanya hivi karibuni huko Tabora ilikuwa ni yamafanikio makubwa kwaani iliweza vuna wanachama wengi sana japo wengi walikuwa wa mijini. Nadhani ingefaa zaidi kama nguvu kazi ingeelekezwa pia vijijini.
 
lakini kama unaitakia mema CDM na unaamini ktk mageuzi kupitia CDM basi kila mmoja wetu kwa nafasi yake kokote alipo anawezA kuanzisha tawi then akatoa taarifa makao makuu kwa uthibitisho tu,kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumemsaidia sana Dr Slaa na CDM kiutendaji kuliko kumsubiri yeye apite boda kwa boda,kitaa kwa kitaa,
 
natofautiana na aliyesema si lazima kuwa na matawi. ukweli ni kwamba hakuna taasisi yeyote imara duniani ambayo haina organisation kuanzia grassroots. hiyo ndio kete pekee waliyonayo ccm. ukitaka kujua thamani ya grassroots angalia kanisa katoliki. akitoa agizo leo pope litafika hadi jumuiya zote duniani kwa muda mfupi. ila kwa madhehebu mengine kwa kukosa hilo hawana ushawishi mkubwa duniani.
 
Naungana nawe,hapa dr. slaa lazima wajipange kuhakikisha CDM vijijini inaimarishwa kwa sana; maana huko ndo mtaji wa ccm. wanakijiji wakielimishwa na wakaelimika, basi kazi itakuwa imekwisha. Hilo lifanywe haraka kuanzia sasa. Nashauri mikutano ya Dr. slaa ianze kushuka hadi katani na vijijini kufungua matawi. wakuu wa chama wilaya / mikoa wasilale usingizi ndo wakati mwafaka kwao kuimarisha chama ngazi za vijiji katika maeneo yao.
 
Kweli mimi naona Tabora bado kunahitajika Operation Sangara. Itakwenda lini Tabora ili kuweka mizizi ya CDM pale?
 
Mambo ya tawi kila mtaa yamepitwa na wakati hii sasa ni dunia nyingine si ya TANU, CCM mbali kuwa na Tawi kila uchochoro lakini bado inakimbiwa na wanachama. Kinachotakiwa kwa chama ni kuangalia maeneo muhimu ambayo yanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kama vyuoni, mashuleni na kadhalika, kuna wakati mwingine matawi ni kuongeza mzigo na migogoro tu kwa chama, hata unapotaka ku invest lazima kuwe na feasibility study si kuanzisha kila unapoambiwa kuna wateja angalia kama kuna raw materials na zita last kwa kipindi gani.

Nakuunga mkono mkuu thanks
 
Wanatakiwa kujifunza DEMOCRATIC wanavyofanya MAREKANI, Kwani OBAMA analist na CONTACT za wanachama, washabiki na wapenzi wake wote kiasi akitaka kuwasiliana nao ni swala la dakika tu.

Nashahuri CHADEMA wafanye hivyo na ni rahisi sana kwa wakati huu kwani CHADEMA ingeweza kuwa na DATABASE ya CONTACTS za watu wake na inakuwa rahisi kuwasiliana nao wote with few minutes.
 
Mabadiliko ya uongozi katika Africa hayategemei wingi wa wanachama ulionao, inategemeana na sera mlizonazo, waafrica wengi sio wanachama wa chama chochote angalia katika watanzania million 40 sasa wanachama wa vyama vyote hawafiki hata mil. 8 Kitu muhimu ni CDm kuhakikisha kinakuwa chama cha wanyonye wanaotesswa katika nchi yao wenyewe
 
Huo ndio ukweli. CCM wanategemea sana watu wa vijijini zaidi kwa kuwapigia kura.
Wengi uchaguzi uliopita kilichosaidia ni vile vitambilisho amabavyo wengi waliona ni vya uraia. WATU WENGI WA MJINI HAWAJALI KUPIGA KURA. Vijijini mzee nyumba kumi anahakikisha watu wake wameenda kupiga kura. CDM HUKU JUU SAFI SASA WAKUBALI GHARAMA WAJENGE CHAMA KUANZIA CHINI. Pia kuna watu wengi hata tulio mjini hatujakata kadi hasa walio serikalini.
UNIQUE
 
Haya Dr Slaa umesikia ushauri wetu sasa changanya na zako!!
Wapo wanaotoa ushauri kwa kukitakia mema chama na tupo tunaokitakia kifo. Kumbuka Chadema ni taasisi na taasisi hii inaundwa na wanachama hivyo mawazo yote uyachambue kisha uone pumba na mchele. Nakushauri muongeze bidii kupata wanachama hasa vijijini na muwe na matawi yanayoeleweka vyema kuliko wazo mbadala. Jamaa amewapa mtihadi wa wanachama milioni kumi ..... mie nakupunguzia hadi milioni tano. Muwe na data base yao kabisa siyo suala la kugawa kadi na kukimbia.

Kazi kwako katibu wetu!
 
Back
Top Bottom