Dr. Slaa: Sina Mpango wa kugombea Urais 2015

Dr. Slaa: Sina Mpango wa kugombea Urais 2015

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,233

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa

DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kitu kitafanywa kwa wakati muafaka, kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.

Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, niaheshimu uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.

UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala la rais, serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.

Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba."

Chanzo: Mtanzania Juni 11, 2014

My take:
Dr. Slaa ni kiongozi mtiifu

Hata akigombea atapoteza muda wake bure watanzania wameisha wajua Chadema ni matapeli wa kisiasa.
Uungwana ni vitendo, hata mwanzo hakutaka allitikia mwito wa chama chake. Ritz hebu kua kidogo.
 
Yeye na Mbowe wameharibu chama kiasi kwamba hata yeye mwenyewe anaona uwezekano wakupata urais hakuna. Mbona hakusema hivyo baada ya uchaguzi mkuu wakati Chadema ilikuwa na nguvu?
 
Hata hivyo siyo yeye anayeamua kugombea,bali ni watu
wanampendekeza,huyu Dk ana akili za kuzaliwa,wengine
hawaoni hizi akili kubwa,wamebaki kwenye akili ndogo.
Tanzania hatutaendelea kama tutaendelea na siasa za aina
hii nyepesi nyepesi watu wanachukua mali sisi tunabaki
kuwatetea.hii ajabu kabisa ya Dunia.
 
Tukumbuke hata 2010 dr. Slaa hakupenda kugombea urais bali alipendekezwa na chama chake!kiongozi yeyote makini na anayefaa hupendekezwa na watu wenyewe..na si kukimbilia madaraka.hongera dr..maoni yangu ni kuwa bado ungetufaa sana 2015 kama uzima utakuwepo.Mungu akulinde wakati wote!
 
kikwete hawezi kutamka haya maneno,anajua 2010 aliiba kura,akisikia jina slaa kifafa kinampanda anaanguka jukwaani....

Kikwete aliiba kura za urais na ubunge? Mbona mliambulia wabunge 23 tu? hata Slaa angeshinda urais angewezaje ku-survive na wabunge 23? Uongo mwingine hata haufanani na ukweli.
 
ameona kazikosa pesa nyingi za posho za bunge mpaka la katiba anajuuuuuuta
 
Sizitaki mbichi hizi ...Ndivyo anavyoonekana kuwaza Dr.Slaa.

Slaa halazimishi uongozi. Slaa analazimishwa na wananchi kugombea. Hata 2010 Slaa alikuwa Karatuuuu anakula kitimoto umati wa watanzania ukaenda kumwomba agombee. Hana presha Slaa. Na ndio tabia ya wenye akili nyingi,tabia za watu wenye upeo mkali sana. Tabia za mwerevu hizo. Slaa hataki madaraka, sisi tunaompenda tunataka atake madaraka
 
Mshaurini atafute jiko kwanza.
 
Hawezi shinda akagombee ubunge Kama mrema maana biashara ya jumla ni ya ccm tuu ukawa waende kwenye reja reja
 
Kikwete aliiba kura za urais na ubunge? Mbona mliambulia wabunge 23 tu? hata Slaa angeshinda urais angewezaje ku-survive na wabunge 23? Uongo mwingine hata haufanani na ukweli.
nani kakwambia za ubunge hazikuibiwa,mlikimbia na masanduku ya kura na sehemu nyingine mmeua watu na kutangaza washindi kwa nguvu,sehemu mlizokubali kushindwa ni zile ambazo nguvu ya umma ilishinikiza mkaona hamna jinsi mkakubali yaishe....
 
Hata hivyo siyo yeye anayeamua kugombea,bali ni watu
wanampendekeza,huyu Dk ana akili za kuzaliwa,wengine
hawaoni hizi akili kubwa,wamebaki kwenye akili ndogo.
Tanzania hatutaendelea kama tutaendelea na siasa za aina
hii nyepesi nyepesi watu wanachukua mali sisi tunabaki
kuwatetea.hii ajabu kabisa ya Dunia.

Umenena vzr
 
Back
Top Bottom