Tafadhali Mzee, mimi nimekuwa mpenzi wako mkubwa sana. Nimekupenda sana, kwasababu daima umekuwa mwanamageuzi wa kweli. Inawezekana ni kweli mlitofautiana ujiyo wa Lowassa, lakini tafadhali tunakuomba tuweke mbele maslahi ya watanzania wengi ambao wamekuwa wahanga wa mfumo mbovu wa serikali ya CCM
Nachokuomba tafadhali kwa Jina la YESU Kristo, tusonge mbele kuleta mageuzi, na tusimpe adui nafasi yoyote. Kumbuka kila binadamu anamapungufu yake, na kama Mungu akihesabu mabaya, hakuna atakaweza kusimama, siyo wewe wala Lowassa. Kumbuka maamuzi utakayofanya kesho, yanaweza kukufanya ukumbukwe na vizazi kwa ushujaa wako wakukubali kuweka maslahi mbele, au kukumbukwa kwa kuwa adui mkubwa wa mageuzi.
Mungu akutangulie kesho ufanye maamuzi kwa maslahi na manufaa ya watanzania wote. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki ukawa, Mungu mbariki Slaa, Mungu mbariki mbowe, Mungu mbariki Lowassa