km ulifuatilia uzinduz wa ukawa utakubaliana na mm kuwa hakutoa ahad ya kupambana na ufisad, amezidiwa na magufuli... unategemea nn km anapata kigugumiz kupambana na ufisad
Siku ile ya ufunguzi hakukuwa na muda Wa kutosha kuongea mambo mengi.... Hilo swala limo ndani ya ilani ya ukawa!
Alafu niambie Magufuli hilo swala La ufisadi kaliongeleaje huyo Magufuli?
FULL TEXT; HOTUBA ya
Mgombea Urais wa CHADEMA,
Edward Lowassa, live ITV.
HOTUBA YA MGOMBEA URAIS
KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA
NA UKAWA MH. EDWARD
NGOYAI LOWASSA
YA KUZINDUA ILANI NA
KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29
AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na
Watanzania wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria.
Baada ya miaka ishirini na tano
tangu mfumo wa vyama vingi
urejeshwe, vyama vya upinzani
wa CHADEMA, CUF, NCCR na
NLD umeungana chini ya Umoja
wa Katiba ya Wananchi
kupigania uchaguzi mkuu wa
mwaka huu na kuwa na
mgombea mmoja katika ngazi
zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya
utawala wa serikali za CCM na
waasisi wake, umekuwa utawala
wa wachache walio hodhi
madaraka na mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya
uhakika ya kuleta mabadiliko
ya kweli nchini.
a. Mabadiliko yaletayo neema
na kujenga upya mfumo wa
uchumi, haki na sheria nchini.
b. Mabadiliko ya kuimarisha
huduma za jamii kama elimu,
afya, maji na makazi.
c. Mabadiliko ya kuondoa
umaskini.
d. Mabadiliko tunayatoahidi ni
mabadiliko ya kurejesha
matumaini kwa Watanzania kwa
kubadili hali zao za maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa
maisha ya Watanzania imeshuka
wakati tunaambiwa kuwa pato
laTaifa linakuwa.
5. Lakini Watanzania
wanachotaka siyo takwimu bali
kuona kipato chao kinakua,
shule, hospitali na barabara
bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi
na salama ya kunywa.
Wanataka makazi bora.
7. CHADEMA na UKAWA, tuna
dhamira ya kuleta mabadiliko
ya kweli ili kuona azma ya
Watanzania tangu uhuru ya
kuondoa umaskini, maradhi,na
ujinga inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji
tufanye mabadiliko ya fikra,
uongozi, sera na utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na
changamoto nyingi za ki-
uchumi, kisiasa na kijamii.
Changamoto hizi ni matokeo ya
sera za utawala wa Chama
kimoja wa miaka hamsini. Sote
ni wahanga wa siasa na sera
hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM
imetosha. Tunataka mabadiliko
na siyo ahadi zile zile kila
mwaka
11. Tusidanganyike, CCM
hawana jipya
12. Chagueni UKAWA wenye
dira ya kubadili maisha ya
wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini
na mimesimamia maendeleo
kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri
Mkuu nilijaribu kubadili hali hii.
Nilisimamia ujenzi wa shule za
kata, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Nilihakikisha mikataba mibovu
ya maji inavunjwa na sasa
wananchi wa kanda ya ziwa
wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna
mpango gani wa kumaliza
umaskini. Sisi hatuahidi tu.
Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya
kuondoa umaskini kwa mikakati
sahihi na siyo nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa
umaskini si wa sekta kwa sekta
bali wa sekta zote kwa pamoja.
Ni ujumla wa utendaji na
utekelezaji wa sera za kila sekta
utakao leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA
wa kuondoa umaskini utakuwa
na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya
serikali na mashirika yake na
kuimarisha utendaji na
uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa
kudhibiti ukwepaji na misamaha
ya kodi holela na kuhakikisha
nchi inawekeza katika sekta
muhimu na inapata gawio
halisia kutoka wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na
sheria endelevu ikiwa ni pamoja
na kukuza biashara na
uwekezaji hasa katika sekta za
madini, kilimo, viwanda, ufugaji
na uvuvi na kuondoa kodi kwa
wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za
umma kama elimu, afya, maji
na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na
mfumo wa haki na sheria chini
ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili
kufanikisha mkakati wa
kuondoa umaskini, serikali
yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA
MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma.
Nalisema tena leo. Elimu
kwanza, Elimu kwanza, Elimu
kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa
msingi utakuwa kutoa Elimu
itatayogharamiwa na serikali
kwa kila Mtanzania kutoka
elimu ya msingi hadi Chuo
Kikuu na pia:-
1. Kuimarisha elimu ya
teknolojia, ustadi na ufundi
inayojenga uwezo wa kujiajiri na
ushindani katika soko la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa
miundombinu ya elimu ikiwa ni
pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango
vya elimu kote nchini.
4. Kuimarisha taaluma na
mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na
kuboresha afya za wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na
vitendea kazi kwa walimu ikiwa
ni pamoja na nyumba, posho
ya kufundishia, usafiri na zana
za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara
ya shule za kata
AFYA
1. Afya na tiba ya kila
Mtanzania itagharamiwa kupitia
bima za gharama nafuu na
mifuko ya hifadhi ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi
pamoja na kinga kupunguza
gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna
uwiano na upatikanaji wa
watumishi wa afya katika kada
mbalimbali ili kuleta tija na
huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya
afya pamoja na kujenga
hospitali za kisasa ili kusogeza
huduma za afya karibu na jamii
na pia kuepukana na tiba za
nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la
kuboresha maslahi na vitendea
kazi katika sekta ya Afya ikiwa
ni pamoja na nyumba na
usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la
gharama za huduma za afya
bila kuathiri uendeshaji wa
watoaji huduma za afya kama
vile serikali na hospitali za
sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
1. Tutaimarisha mfumo wa
umiliki wa ardhi kwa
Watanzania na kudhibiti
migogoro ya ardhi hasa kati ya
wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya
Tanzania na kumilikisha vijiji na
wakulima kwa hati za serikali ili
kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo
kwa kuimarisha elimu, ufundi
na teknolojia ya kisasa na
kumkomboa mkulima kutoka
jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji
na uvuvi wa kisasa na
kuunganisha sekta hizo na ya
viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi
wanatunza na kulinda vyanzo
vya maji.
6. Tutakuza kilimo cha
umwagiliaji kwa kuwapa
wakulima elimu na mikopo ya
riba nafuu ya kuvuna maji na
kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki
yatakayomhakikishia kwa kila
Mtanzania kupata maji safi na
salama. Kumaliza kero za maji
nchini kutamkomboa
mwanamke kutokana na adha
ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao
na mifugo kwa wakulima na
wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha
biashara kinachozingatia
maslahi ya nchi na ya
Watanzania.
10. Tutaanzisha programu
maalum ya kufufua mazao asilia
ya Tanzania hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya
Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo
na kujenga mpya kama vitega
uchumi vya Taifa ili kurejesha
biashara tulizopoteza kwa
bandari za nchi jirani.
2. Tutajenga barabara nchini
kwa kuzingatia ubora hasa zile
za vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa
viwango vya kisasa
4. Tutajenga shirika la Ndege la
Taifa linalojiendesha kwa
misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya
kisasa na kuondosha
misongamano ya magari hasa
katika majiji ya Dar es salaam,
Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na
usambazaji wa umeme vijijini ili
kufikia zaidi ya asili mia sabini
na tano ya Watanzania
VIWANDA
1. Tutaimarisha sekta ya
viwanda kuwa mhimili wa
uchumi kwa uzalishaji wa
bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya
kusindika mazao ya kilimo,
uvuvi na ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya
miaka mitano mali ghafi zote za
Tanzania zinasindikwa kabla ya
kusafirishwa nje ili kuongeza
mapato na ajira ya mamilioni
ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji
wa Viwanda
UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi
wa nchi ili kuhakikisha kuwa
mfumo wa uchumi wa Tanzania
unakuwa ni wa soko-kijamii
ambapo nguvu za soko
zitatumikia jamii kwa serikali
kuweka uwiano wa mapato
unaohakikisha huduma za
kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na
bidhaa za ndani kwa kuwapa
Watanzania upendeleo wa
maksudi kwa kipindi cha mpito
ili waimarike na waweze
kuhimili ushindani. Tutawapa
wafanyabiashara wetu
upendeleo katika manunuzi ya
serikali na kuwajengea
mazingira mazuri ya biashara
na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania
kupata mitaji ya biashara kwa
masharti nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na
wawekezaji wenye tija. Kuweka
udhibiti wa wahamiaji wasioleta
tija wala maslahi kwa Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia
baina ya Serikali na Sekta
binafsi kwenye maeneo muhimu
ya kiuchumi na kibiashara. Pia,
kuwawezesha Watanzania
kuwekeza kwa njia ya ubia na
wawekezaji wenye mitaji
mikubwa bila kujali
wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa
kubadilisha mfumo wa Vyama
vya Ushirika nchini ili utokane
na uendeshwe na wakulima
wenyewe ikiwa na pamoja na
kuwawezesha kuboresha makazi
kwa mpango wa kushirikiana
kujenga nyumba bora
7. Tutaanzisha na kuwezesha
uanzishaji wa viwanda
vidogovidogo vinavyotoa ajira
kwa wingi kwa kuvihusisha na
vyuo vya ufundi na benki
maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
1. Tutasimamia swala la ajira
hasa kwa vijana kwa kukuza
elimu ya ufundi ili waweze
kujiajiri
2. Tutazipa kipaumbele sekta
zinazozalisha ajira kwa wingi
hasa za viwanda, kilimo,
ufugaji, uvuvi na utalii na
kuzipa unafuu wa kodi ili zikue
kwa haraka.
3. Tutawapa wawekezaji
wakubwa katika sekta hizi
upendeleo maalum na viwango
vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
1. Serikali itashiriki kikamilifu
katika uzalishaji wa nishati
2. Itatengeneza mazingara
mazuri ya kisera yatakayovutia
na kuwezesha ushiriki wa
Watanzania na ubia kati yao na
wageni.
3. Serikali yangu itaupa
uzalishaji mkubwa wa umeme
wa maji kipaumbele namba
moja, umeme wa makaa ya
mawe kipaumbele namba mbili,
umeme wa gesi asilia
kipaumbele namba tatu na
umeme wa urana kipaumbele
namba nne.
4. Serikali itatoa vipaumbele
muhimu kwenye usambazaji wa
huduma kubwa ya umeme
sehemu za uzalishaji uliyolenga
masoko ya ndani, ya nchi jirani
na ya nchi za kigeni.
5. Itapitia upya mikataba yote
mikubwa ya nishati na madini
ili kubaini iliyo mibovu na
kuifanyia maboresho.
6. Serikali yangu itatumia
sehemu ya hisa zake kwenye
raslimali kubwa ya gesi asilia
iliyopatikana hapa nchini kama
rehani kwenye kujichukulia
mikopo kwa ajili ya ujenzi wa
miundo mbinu ya mabomba ya
gesi.
7. Serikali itatoza kodi na ada
ndogo zaidi kwa wazawa wenye
ubia kati yao na wageni kuliko
zitakazotozwa kwa wageni
wasiowekeza kwa kushirikisha
wazawa.
8. Serikali itasitisha utoaji wa
misamaha ya kodi isiyo lazima
kwenye sekta ya madini, na
badala yake itawekeza kwenye
kuongeza thamani ya raslimali
zake za madini.
9. Tutakuza nishati mbadala
kutamkomboa mwanamke
kutokana na adha ya kukata
kuni
MALIASILI NA UTALII
1. Tutasimamia uvunaji na
matumizi ya rasilimali za Taifa
kwa manufaa ya kila Mtanzania
wa kizazi hiki na kijacho
2. Tutapiga vita ujangiri na
kuimarisha utunzanji wa hifadhi
za taifa na mazingira
3. Tutachochea ujenzi wa
miundombinu ya utalii nchini
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
mahoteli na kuimarisha
mafunzo
4. Tutaongeza idadi ya watalii
kufikia milion mbili ifikapo
2020.
UTAWALA BORA, ULINZI WA
NCHI NA USALAMA WA RAIA
1. Tutasimamia Katiba mpya
inayolinda haki za msingi za
wananchi na kuweka bayana
mipaka ya madaraka ya serikali
na viongozi, Bunge na
Mahakama.
2. Tutaboresha miundobinu ya
sheria na kuimarisha utendaji
wa Mahakama na maslahi ya
wafanyakazi
3. Tutasimamia haki za raia na
kuangalia upya sheria
kandamizi ili wananchi kama
Masheik wa Zanzibar hawasoti
jela kwa sababu za kisiasa.
4. Tutaimarisha mafunzo ya
vyombo ya Polisi hasa
wapelelezi na waongoza
mashtaka ili wapate uwezo wa
kusimamia utoaji wa haki.
5. Tutavipa vyombo vyote vya
ulinzi na usalama nyenzo na
kuboresha mazingira yao ya kazi
na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA
UWAJIBIKAJI
1. Tutajenga uzalendo ili kila
Mtanzania aweze kutathmini
mchango wake kwa taifa kila
siku
2. Tutaimarisha nidhamu,
utendaji na uwajibikaji katika
Sekta ya Umma
3. Tutaimarisha mchango wa
Wataalam wetu, wanawake na
vijana katika kusimamia uchumi
na kuwajengea mazingira
stahiki ya kazi pamoja na
mafao.
4. Tutapiga vita rushwa na
ubadhirifu katika sekta ya
Umma na binafsi
5. Tutadhibiti na kupunguza
matumizi ya serikali ikiwa ni
pamoja na kufuta safari za
watumishi serikalini zisizokuwa
muhimu pamoja na zile za Rais
na kupiga marufuku matumizi
ya mashangingi serikalini.
6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa
kuanza na ukaguzi wa madeni
ya serikali ili kuhakiki jinsi
yalivyotumika
7. Tutaimarisha uwazi na
kuondoa usiri katika shughuli
za serikali na kuweka bayana
mikataba yote ya nchi ikiwa ni
pamoja na ile ya mafuta,
madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
1. Tutadhibiti mapato kutokana
na raslimali kwa kupitia upya
viwango vya mirabaha kutokana
na madini na gesi asilia ili
kuhakikisha kuwa Tanzania
inapata gawio stahiki.
2. Serikali itaanzisha Wizara
maalum itakayosimamia nishati
ya gesi na mafuta.
3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili
wa Hazina ili kusimamia vema
uwekezaji wa Serikali katika
mashirika na mapato yake.
4. Tutahakikisha kuwa
mashirika ya umma
yanaendeshwa kwa misingi ya
faida na uadilifu.
5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za
ushuru wa forodha na kupiga
marufuku misamaha ya kodi
holela ili kuokoa mabilioni ya
fedha yanayopotea kila wiki.
6. Sambamba na hilo
tutarahisisha utaratibu wa
kulipa kodi ili kuondoa kero na
mazingira ya rushwa. Kwa
kudhibiti makusanyo ya kodi
tutakusanya fedha za
kugharimia huduma za msingi
kama afya na elimu kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
1. Tutaimarisha umoja, usalama
na udugu wa Watanzania na
Muungano kwa misingi ya haki
na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA
WAZEE
1. Wanawake watapewa fursa
na haki sawa katika elimu na
uchumi ili waweze bila
kuwezeshwa.
2. Tutahakikisha wazazi
wanapata fursa ya kuwa walezi
na wafanyakazi kwa kuongeza
urefu wa likizo ya uzazi
3. Tutaimarisha elimu ya
watoto hasa wasichana na
kukuza fursa zao na kukomesha
ndoa za watoto wadogo.
4. Tutaongeza uwakilishi wa
akina mama katika ngazi zote
serikalini na mashirika yake
kufikia asili mia hamsini ifikapo
2020.
5. Wazee na wasiojiweza
watapewa posho ya kujikimu
inayokidhi mahitaji ya msingi
itakayowawezesha kuishi kwa
heshima na kulinda utu wao
ndani ya familia na jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA
MICHEZO
1. Tutaendeleza na kuwezesha
vipaji vya sanaa na michezo
2. Tutarudisha viwanja vya
michezo vilivyovamiwa
3. Tutafuta kodi zote za vifaa
vya michezo.
4. Tutadhibiti viwango na
maadili ya bidhaa za nje
zinazoingizwa nchini na kuzitoza
kodi halisia
5. Tutajenga taasisi na vyuo
vya kukuza michezo ili
kuhakikisha kuwa ndani ya
miaka mitano Tanzania
inashiriki kwa ushindi katika
mashindano ya kimataifa ya
soka na riadha
6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa
nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa
wasanii chipukizi ili kuwapa
muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE
TIJA KWA TAIFA
1. Tutakuza ushirikiano wa
Kimataifa wenye tija na Ujirani
mwema.
2. Tutatetea haki za binadamu,
usawa wa nchi na kuimarisha
ushiriki wa Tanzania katika
diplomasia ya kimataifa.
3. Tutakuza umoja na
ushirikiano wa Umoja wa Afrika,
Jumuia ya Afrika Mashariki,
SADC na Umoja wa Mataifa.
4. Tutaimarisha Umoja wa
Mataifa ikiwa ni pamoja na
kudai mabadiliko ya mfumo ili
kuleta usawa wa nchi shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema
yafuatayo
1. Natambua kuwa uongozi ni
dhamana. Mkinichagua nitaienzi
dhamana hiyo kwa utendaji
uliotukuka.
2. Nawaahidi Watanzania kuwa
kwa uwezo, akili, uzoefu na
nguvu zangu zote
nitawatumikia. Nawaomba
nanyi mniahidi jasho lenu na
uwezo wenu wote ili kwa
pamoja tuvuke. Tutajikomboa
toka utawala wa CCM
unaodumaza uchumi na
maendeleo. Tutaanza safari ya
uhakika kuondoa umaskini.
3. Mabadiliko pia ni kuthamini
utu na kukataa hadaa ya hongo
ili kuuza haki yako ya
kuchagua. Msikubali rubuni za
uchaguzi kwa kupewa pesa au
vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo
sera ya CCM. Ukikubali basi
umeuza pia haki na sauti yako
ya kuwalalamikia walio
madarakani. Imetosha.
Tukatae. Tulinde utu na haki
zetu. Tuchague mabadiliko.
4. Mabadiliko ni fikra. Ni
kufikiri na kutenda tofauti.
Hatuwezi kuendelea kufikiri na
kutenda kama kwamba hatuna
dharura ya maendeleo. Kwanza
tuanze kwa kufanya mabadiliko
na tujiamini kuwa sisi kama
Taifa tunaweza. Tunaweza
kujitegemea na kuleta
maendeleo yetu wenyewe bila
kutegemea wafadhili. Hii si
ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa
kuondoa umaskini katika kizazi
kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
5. Tuwe taifa linalotumia
raslimali zake kujiendeleza na
siyo kuwanufaisha wageni na
kuwafanya Watanzania watwana
katika nchi yao. Inabidi tuache
kuwa taifa ombaomba. Tuache
kuukubali na kuvaa umaskini
kama joho la fahari.
6. Mabadiliko ya kweli hayawezi
kuletwa na CCM. Tusitegemee
kuwa leo wana jipya. Ndiyo
maana ahadi walizotoa miaka
thelathini iliyopita ndizo
wametoa juzi. Tukatae hadaa.
Miaka hamsini ya CCM
imetosha.
7. Tunaamani kwamba
tutashinda kwa sababu
Watanzania mpo nyuma yetu.
Watanzania mmeamua kuleta
mabadiliko. Kura yako ndiyo
itakayokuwa mkombozi wako.
Hakikisha unapiga na kuilinda
kura yako. Wakati wa
mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania.
Asanteni sana