Dr. Slaa silaha ya maangamizi kwa Lowassa

Dr. Slaa silaha ya maangamizi kwa Lowassa

Ally Kanah

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Posts
1,479
Reaction score
388
Wanajukwaa niaje??

Wacha tusemezane kidogo...na leo tusemezane juu ya hii silaha ya maangamizi ya ndugu Lowassa.

Ikiwa Lowassa na Mbowe wataweza kuhakikisha Slaa anaendelea kunyamaza, nini itakuwa athari kwa mbio zao kuelekea Magogoni? Hii itaendelea kuwaaminisha wale walioamua kufa kishujaa na Slaa na wale ambao bado hawajaamua nani wampigie kura waendelee kuamini kuwa Lowassa ni Fisadi na hafai kuwa Amiri Jeshi wa Majeshi yetu.

Ila Mbowe na Lowassa endapo watazichanga karata zao vizuri na kumuangukia Slaa na Slaa hata akaamua kushiriki katika Campaign japo kishingo upande, basi CCM wategemee upinzani mkali ambao hawajawahi kuupata tangu kuzaliwa kwa chama hicho.

Ila endapo Mbowe na Lowassa wakampuuza Slaa kwa kuamini kwamba hana impact yeyote eti kisa tu watu wanataka Mabadiliko, basi endapo Slaa ataamua kuufungua mdomo wake kuongea na Watanzania, Mbowe na Lowassa wategemee anguko kuu ambalo halijawahi kuonekana katika nchi hii.

Tujaribuni kusemezana kistaarabu tu, kama Mbowe na Lowassa wanavyohubiri namna Campaign zitakavyoendeshwa bila ya matusi, basi na hapa tusemezane tu bila Matusi.
 
Swala La Slaa Ndani ya wiki hii au wiki ijayo litatolewa taarifa rasmi na viongozi Wa Cdm
 
Swala La Slaa Ndani ya wiki hii au wiki ijayo litatolewa taarifa rasmi na viongozi Wa Cdm

Isiwe tu sanaa maana kuna kama maswali mawili matatu labda tujiulize...

1) Slaa kuendelea kukaa kimya je inaisiadia UKAWA na Mgombea wao??

2) Je Slaa kujiunga kwenye uwanja wa mapambano nini itakuwa impact yake??

3) Tumewasikia ACT-Wazalendo leo wakiibeba agenda ya UFISADI Je Slaa akiamua kuvunja ukimya na kujiunga na hao wazelendo kusimamia kile anachokiamini yaani VITA DHIDI YA UFISADI nini itakuwa athari kwa LOWASA na UKAWA??
 
Dr. Slaa popote ulipo wewe nakuomba mzee wangu endelea kujichimbia... umejizolea sifa kedekede kwa watanzania na uimara wa chama chako.... Kujitoa akili kama Mbowe ili kumpigia kampeni Lowassa mzee wangu utakuwa umepoteza maksi nyingi kwa Watanzania....

Mimi bado natembea kwenye itikadi zako. Heri kujiunga ACT au kuanzisha chama kipya mpaka 2020 utakuwa upo juuu... Achana na Mbowe, Mtei hawa ni wachumia tumbo hawana uchungu na taifa letu.
 
Ana umuhim wake lkn hata km asipokuwepo cdhan km anaweza kuwafanya watanzania wasiiamini ukaw
 
Isiwe tu sanaa maana kuna kama maswali mawili matatu labda tujiulize...

1) Slaa kuendelea kukaa kimya je inaisiadia UKAWA na Mgombea wao??

2) Je Slaa kujiunga kwenye uwanja wa mapambano nini itakuwa impact yake??

3) Tumewasikia ACT-Wazalendo leo wakiibeba agenda ya UFISADI Je Slaa akiamua kuvunja ukimya na kujiunga na hao wazelendo kusimamia kile anachokiamini yaani VITA DHIDI YA UFISADI nini itakuwa athari kwa LOWASA na UKAWA??

Slaa kuendelea kukaa kimya inasaidia ukawa ndio ingawa inaleta maswali mengi kwa makamanda wa CDM.....

Slaa akijiunga Leo ktk kampeni italeta nguvu sn na itakua km tsunami vile!

Slaa hawezi kutoka Cdm na kujiunga na ACT ata iweje.....

Swala La ufisadi sijui unalitizama vipi kwa upande Wa ukawa? Unataka kusema ukawa ni mafisadi kwa kumkaribisha Lowassa?
 
Shabaha ya chama cha siasa ni kushika dola. Sasa iwapo Dr. Slaa atakuja na yake ili UKAWA wasishike nchi, huo utakuwa ni usaliti.
Pia akithubutu kufanya usaliti atakuwa amepotea kama Prof. Lipumba..
 
Shabaha ya chama cha siasa ni kushika dola. Sasa iwapo Dr. Slaa atakuja na yake ili UKAWA wasishike nchi, huo utakuwa ni usaliti. Pia akithubutu kufanya usaliti atakuwa amepotea kama Prof. Lipumba..

Kwani mkuu Slaa kukaa kwake kimya unafikiri kunatokana na nini?? Kama angekuwa anataka UKAWA kuchukua nchi si tungemuona kwenye majukwaa ya siasa?? Embu dadavua mkuu
 
Kwa hiyo DR. Slaa baada ya kukimbia UKAWA na kuachana na siasa za kuiondoa CCM madarakani udini mliotuambia kwamba aliutumia mwaka 2010 umeisha?
Au CCM walitudanganya kama kawaida yao ya kupata kura kwa njia ya udanganyifu?
Au CCM wanataka kumtumia huyo huyo tulioami ishwa kuwa ni mdini ili tu wapate kura za malofa?
CCM mnaligawa taifa kwa manufaa ya wachache. Hatutaki kugawanywa na wauza unga.
 
Matunda ya Ngurdoto yanaonekana, lakini mmebuugi maana Watanzania hawadanganyiki teena
 
Back
Top Bottom