Dr. Slaa njoo sasa utueleze Lowassa ni Mali au Lah!

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
→→→ Wakati katibu mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akitangaza kujiondoa chama hicho, aliacha maswali ya kutathmini ujio wa Edward Lowassa kama utakuwa mzigo au mali kwa vyama vya upinzani, na sasa wilaya za Ilala na Kinondoni zimekamilisha majibu.

→→→ Ushindi wa kwanza wa vyama vya upinzani katika nafasi ya umeya za manispaa hizo mbili umeonyesha nguvu ya Lowassa.

Na ni dhairi Dr Slaa kama alikuwa akihitaji mali baasii tunasema alitupa dhaabu chooni. Kwa matokeo haya. Natarajia Dr arudi hapa JF atuambie kwa mara ya pili. Lowassa ni mtaji au ni hasara?

Karibu sana Mhe. Dr Slaa utupatie majibu.
 
Usisahau juhudi zilizofanyika 2011 mpaka 2014, CHADEMA ilitabiriwa kufa lakini ikashamiri.

Usisahau pia uwepo wa UKAWA kabla ya uchaguzi.

Baada ya hapo ndio umuongelee Lowassa.
 
Ni mzigo kama hulijui hilo
Toka siasa za vyama vingi kuanza nchini.Hamna chama cha upinzani kilishawahi kupata kura nyingi za urais wa muungano kama 2015
Je,Bado kwako ni mzigo?Kama ndio,Jipime upya uwezo wako wa kufikiri
 
→→→ Wakati katibu mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akitangaza kujiondoa chama hicho, aliacha maswali ya kutathmini ujio wa Edward Lowassa kama utakuwa mzigo au mali kwa vyama vya upinzani, na sasa wilaya za Ilala na Kinondoni zimekamilisha majibu.

→→→ Ushindi wa kwanza wa vyama vya upinzani katika nafasi ya umeya za manispaa hizo mbili umeonyesha nguvu ya Lowassa.
Na ni dhairi Dr Slaa kama alikuwa akihitaji mali baasii tunasema alitupa dhaabu chooni.
Kwa matokeo haya,Natarajia Dr arudi hapa JF atuambie kwa mara ya pili.Lowassa ni mtaji au ni hasara?Karibu sana Mhe.Dr Slaa utupatie majibu.
Kumbe umeya ilala na Kinondoni ndiyo yalikuwa malengo yao tu sio Ikulu!!
 
Huo ushindi unatokana na kuunganisha nguvu kwa vyama vya ukawa, ikichangiwa na kampeni za M4C zilizofanyika wakati Lowasa anaitetea CCM. Lowasa Hana mchango kabisa kwenye kuongezeka Kura za upinzani au kupatikana kwa mameya wa upinzani.
 
Tuwe wakweli hata kidogo tu...Hivi kilichofanya UKAWA washinde nafasi za umeya Dar ni:

1) Kuunganisha nguvu kwa vyama vya upinzani na kuundwa kwa UKAWA....au

2) Lowassa kuvibeba vyama vya upinzani
 
Tunaongelea mafanikio ya Dr 2010 na Lowassa 2015
Je kwa slaa Chadema wameongeza au wamepoteza?Aje hapa atujibu
Chadema wanajipa moyo tu, iliyofaidika na ukawa ni Cuf na siyo chadema.

Chadema wamepoteza majimbo mengi sana na kurudi ccm
 
Huo ushindi unatokana na kuunganisha nguvu kwa vyama vya ukawa, ikichangiwa na kampeni za M4C zilizofanyika wakati Lowasa anaitetea CCM. Lowasa Hana mchango kabisa kwenye kuongezeka Kura za upinzani au kupatikana kwa mameya wa upinzani.

Kweli kabisa.
 
Mnaongelea wapi hayo mafanikio!! nyie mmeishapoteza muelekeo? Tumieni akili bana,...
Kura milion 6 kutoka million 2
Halimashauri 36
Ruzuku milion 300 kutoka milion 100
Bado unabisha tu?
Viti maalum,Madiwani Hahaha Ccm na Dr mmechanganyikiwa
 
Tuwe wakweli hata kidogo tu...Hivi kilichofanya UKAWA washinde nafasi za umeya Dar ni:

1) Kuunganisha nguvu kwa vyama vya upinzani na kuundwa kwa UKAWA....au

2) Lowassa kuvibeba vyama vya upinzani
Umeanza kujitambua, Mungu mkubwa. Naamini msemo kuwa kwenye ukweli uongo hujitenga.
 
Viatu vya Slaa vikubwa Lissu. ...Wewe endelelea kujifariji na hiyo Ruzuku. !
 
Kutoka kutamba kwamba wana chukua nchi asubuhi, na akishindwa Lowasa nchi haitatawalika hadi kushangilia umeya Wa ilala ?!?!

Are you serious Chadema??

Pia hao wabunge hawajaletwa na Lowassa , hata asingekuja hao wabunge wangepatikana tu.

Kumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa..
 
→→→ Wakati katibu mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akitangaza kujiondoa chama hicho, aliacha maswali ya kutathmini ujio wa Edward Lowassa kama utakuwa mzigo au mali kwa vyama vya upinzani, na sasa wilaya za Ilala na Kinondoni zimekamilisha majibu.

→→→ Ushindi wa kwanza wa vyama vya upinzani katika nafasi ya umeya za manispaa hizo mbili umeonyesha nguvu ya Lowassa.
Na ni dhairi Dr Slaa kama alikuwa akihitaji mali baasii tunasema alitupa dhaabu chooni.
Kwa matokeo haya,Natarajia Dr arudi hapa JF atuambie kwa mara ya pili.Lowassa ni mtaji au ni hasara?Karibu sana Mhe.Dr Slaa utupatie majibu.

Ni vema kufanya mambo kisayansi. Umeuliza swali zuri....ila jibu lako halikuwa la kisayansi....zaidi limegubikwa na hisia,mahaba ya ushabiki.

Ili ubaini kama Lowassa ni Mali au hasara kwa kigezo cha ukawa kuongoza halmashauri....unatakiwa kujiuliza nchi nzima zipo halmashauri ngapi...na kati ya hizo Chadema inaongoza ngapi....hapo ndio utakuwa na jibu sahihi.....badala ya kuwa na judgment ambayo msingi wake ni ushindi wa kuongoza halmashauri mbili tu kati ya halmashauri 157 (kama sikosei) zilizopo nchi nzima.
 
Back
Top Bottom