Ukiwasikiliza vizuri wazee hawa Lowassa, Sumaye na Membe utagundua kuwa vyama vyote vya Upinzani ni mali ya CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,607
141,429
Kuna wakati Nape Nnauye akiwa Katibu wa uenezi wa CCM aliwahi kutoa siri kwa kusema Katibu mkuu wa Chadema wakati ule Dr Slaa alikuwa bado anamiliki kadi ya CCM na yeye Nape akamlipia Ada ya uanachama hadi 2020.

Mzee Lowassa aliwahi kusema hajawahi kuihama CCM.

Mzee Sumaye akasema alienda Chadema ili kuifanya CCM isilale usingizi.

Membe anasema hajawahi kuhama CCM.

Ukiwasoma vizuri hawa wastaafu utagundua kuwa Upinzani wa Tanzania ni wa bandia na ndio maana hayati Magufuli alividharau sana vyama vya upinzani vyenye kimbelembele.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Wote wasanii tu. Kila mtu akiamua aokoteokote tu sentensi kama ulivyookota dunia itakuwa nzito na kuangukia kuzimu.Tafuta ugali ule bwashee kutoka Mlanda Iringa.😝😝😝😝😝
 
Kuna wakati Nape Nnauye akiwa Katibu wa uenezi wa CCM aliwahi kutoa siri kwa kusema Katibu mkuu wa Chadema wakati ule Dr Slaa alikuwa bado anamiliki kadi ya CCM na yeye Nape akamlipia Ada ya uanachama hadi 2020

Mzee Lowassa aliwahi kusema hajawahi kuihama CCM.

Mzee Sumaye akasema alienda Chadema ili kuifanya CCM isilale usingizi.

Membe anasema hajawahi kuhama CCM.

Ukiwasoma vizuri hawa wastaafu utagundua kuwa Upinzani wa Tanzania ni wa bandia na ndio maana hayati Magufuli alividharau sana vyama vya upinzani vyenye kimbelembele.

Mungu ni mwema wakati wote!
Nimekosa la kufanya mbali ya kukupa hiyo 'wow'! kwa mada yako hii, ambayo inanilazimu niseme kwa mara ya kwanza umenishawishi nikupe 'like'!

Lakini upungufu pekee wa mada yako unapoonekana ni kutoandika chochote kuhusu 'ungangari' waliokutana nao hao watu walipojaribu kuifuta CHADEMA.

WOTE WAMESHINDWA!

Na sasa chama hicho kinaelekea kuwa tisio kwa uhai wa CCM.

Kwa hiyo nakupa nafasi ya kutafakari ili siku nyingine uje na mada ambayo sitakuwa na shida kabisa ya kukupa 'like', hata "Love" kabisa, kama utaweza kuiwasilisha mada inayochambua kushindwa kwa hao wote uliowataja na wengineo kwa kushindwa kwao katika harakati hiyo.

Isingekuwa unazi wako ulioteka akili yote, nadhani chembechembe za u-GT unazo kichwani mwako. Itazame TANZANIA, achana na hizo takataka nyingine.
 
Ulitarajia Aseme Amehama ili Afilisiwe
 
Kwa CCM kuendelea kung'ang'ania kutawala kwa nguvu ni kuendekeza njaa tu.

Hawataki ushindani wanataka kula mpaka wavimbiwe.

Dead Party.
 
Kuna wakati Nape Nnauye akiwa Katibu wa uenezi wa CCM aliwahi kutoa siri kwa kusema Katibu mkuu wa Chadema wakati ule Dr Slaa alikuwa bado anamiliki kadi ya CCM na yeye Nape akamlipia Ada ya uanachama hadi 2020

Mzee Lowassa aliwahi kusema hajawahi kuihama CCM.

Mzee Sumaye akasema alienda Chadema ili kuifanya CCM isilale usingizi.

Membe anasema hajawahi kuhama CCM.

Ukiwasoma vizuri hawa wastaafu utagundua kuwa Upinzani wa Tanzania ni wa bandia na ndio maana hayati Magufuli alividharau sana vyama vya upinzani vyenye kimbelembele.

Mungu ni mwema wakati wote!

No need beating about the bush. Achana na kauli ya ubabaishaji ya “vyama vya upinzani”. Taja CHADEMA. Hiyo ndiyo homa ya siasa za Tanzania. Ndiyo movement iliyotibua mpango wa dola kuunda vyama “rafiki” vya upinzani modeli ya UDP, TLP na NCCR.

Magufuli hakuwahi kuidharau CHADEMA. Alikuwa anaishi katika kivuli cha hofu ya nguvu ya kisiasa ya CHADEMA. Siku zote alitawala nchi akitumia propaganda, muda na nguvu nyingi kuzima viashiria vya uwepo wa “CHADEMA” katika jamii ya Watanzania. Tatizo, CHADEMA ndio sauti mbadala wa serikali hata ndani ya CCM. Haizimiki kirahisi kwa porojo za wazee wa fursa wa CCM.

Kuhusu kadi ya CCM, wahenga karibu wote wanayo tangu enzi za chama kimoja, lakini mfu. CCM ingekuwa inafuata maadili yake kadi nyingi zingeshafutwa.

Habari ya Membe na ACT ilikuwa comedy tu. Alitokeza muda mfupi na kupotea mapema sana zilipoanza kampeni za 2020.
 
Kuna wakati Nape Nnauye akiwa Katibu wa uenezi wa CCM aliwahi kutoa siri kwa kusema Katibu mkuu wa Chadema wakati ule Dr Slaa alikuwa bado anamiliki kadi ya CCM na yeye Nape akamlipia Ada ya uanachama hadi 2020

Mzee Lowassa aliwahi kusema hajawahi kuihama CCM.

Mzee Sumaye akasema alienda Chadema ili kuifanya CCM isilale usingizi.

Membe anasema hajawahi kuhama CCM.

Ukiwasoma vizuri hawa wastaafu utagundua kuwa Upinzani wa Tanzania ni wa bandia na ndio maana hayati Magufuli alividharau sana vyama vya upinzani vyenye kimbelembele.

Mungu ni mwema wakati wote!
Lakini Wanatumia matril. kuua upinzani

magufuli alitumia tril 2.4 kuua upinzani ambao ni hewa
 
Nimekosa la kufanya mbali ya kukupa hiyo 'wow'! kwa mada yako hii, ambayo inanilazimu niseme kwa mara ya kwanza umenishawishi nikupe 'like'!

Lakini upungufu pekee wa mada yako unapoonekana ni kutoandika chochote kuhusu 'ungangari' waliokutana nao hao watu walipojaribu kuifuta CHADEMA.

WOTE WAMESHINDWA!

Na sasa chama hicho kinaelekea kuwa tisio kwa uhai wa CCM.

Kwa hiyo nakupa nafasi ya kutafakari ili siku nyingine uje na mada ambayo sitakuwa na shida kabisa ya kukupa 'like', hata "Love" kabisa, kama utaweza kuiwasilisha mada inayochambua kushindwa kwa hao wote uliowataja na wengineo kwa kushindwa kwao katika harakati hiyo.

Isingekuwa unazi wako ulioteka akili yote, nadhani chembechembe za u-GT unazo kichwani mwako. Itazame TANZANIA, achana na hizo takataka nyingine.
Kama ilivyo jina lako, unaandika chochote kile, kwa kuwa kalamu haina maamuzi, means tuachane na siasa, Tz kwanza, kivipi yaan? Dola yeyote ile lazima iwe na mfumo wa Utawala, hata Dini zina viongozinwanaofuata taratibu zilizowekwa!
 
Mkuu umejua leo?
Mimi huwa nafikia kuwaza hata kule kwenye vyama vya upinzani wanakopokelewa ni Mamluki wa Chama pendwa.
Tunaochezewa akili ni sisi raia!
 
Back
Top Bottom